Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,059
Vema. (Ndicho nilichofanya), lakini haidhuru kitu turudie.Evidences zinajenga facts.
Katika utawala huo, shutuma za wachache ni nyingi, na ni wale wenye access na ulaji wa keki kimasihara.
Wamejenga chuki kwa kukataliwa access hiyo na sasa wanatukia access waliyonyimwa before kuwapofusha wananchi ili wao waendelee kula nchi pamoja na wenye nchi!
Weka shutuma moja, back it up na evidence!
Mfano, ukisema, awamu hii wanapiga sana, unasema ushahidi, rejea ripoti ya CAG;
- TTCL hawajui wanayemdai tzs 21.5bn
- SGR analipwa fidia ya tzs 4trillion kwa kucheleweshewa malipo
- Magari yaliyokwisha lipiwa tzs 35bn hayajulikani yalipo.
- Tzs 1.7trillion, zimekwapuliwa tu kiholela
- Tzs 900bn inayotakiwa kulipwa kama faini ya ucheleweshaji wa mradi wa Bwawa la Nyerere, hakuna anayedai kutoka serikalini na shirikani
- Tzs 1.28trillion, waziri wa fedha kakopa tu kiholela, bunge halina habari na hazijulikani ni za nini na ziko wapi!
- Tozo, hakuna muendelezo wa nini kinapatikana na nini kimefanyika kipya
Na listi inaendelea...
NB: Tunakubaliana kwamba tuhuma na majibu vijengwe na facts. Hakuna kuhamisha magoli!
Haya yote hapa chini yalitokea chini/ndani ya mwaka wa KWANZA wa Utawala wa hayati Magufuli:-
1. Januari 26, 2016 - Waziri wa Habari wa Serikali ya hayati, mh Nape anatangaza bungeni rasmi kupigwa marufuku kwa "Bunge Live". Anasema vyombo binafsi vinaweza kurusha live. Mh Nape anasema sababu ni ukubwa wa gharama za TBC kujiendesha.
2. Wiki chache baadaye, Waziri Mkuu Mh Majaliwa anasema Serikali ya Magufuli imepiga marufuku pia vyombo vyote binafsi kurusha bunge live.
3. 26 Agosti 2016, Sheria tata na kandamizi ya Habari- Media Services Act inabadilishwa kwa kuwekewa vipingele vinavyoua uhuru wa kupata na kutoa habari;
4. 07/06/2016 Serikali ya Magufuli inapiga marufuku mikutano yote ya siasa (isipokuwa ya CCM tu).
Katazo hilo lilikuwa haramu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.
Kwa hiyo msingi wa hoja yangu kuwa Tanzania haihataji rais mwingine mfano wa hayati Magufuli unatokana na mambo hayo manne juu, miongoni mwa mengi.
Sasa kwa mujibu wa hoja zako kuwa watu "wachache", "waliokataliwa ulaji" (unatuhumu bila ushahidi), ndio waliompinga Mwendazake, sio kweli wala sahihi.
Twende kuchambua facts na evidence..
1. Hebu tueleze hapa, ni nani "wengi" waliofaidika na hizo Sheria na hizo marufuku?
2. Ni kwa vipi hizo 4 zililisaidia Taifa, kuongeza pato la Taifa; kuondoa umaskini, ujinga na maradhi?
3. Ni vipi hizo zilisaidia kupambana na rushwa, ufisadi na upigaji?
4. Ni vipi ziliboresha utawala bora wa Serikali na uwajibikaji wa Serikali kwa Wananchi wa Tanzania?
5. Ni vipi zilikuza ustawi, demokrasia na utengamano wa jamii na Taifa?
Kama hazikuwa na faida na tija kwa Taifa na kesho ya nchi yetu, inakuwaje mnajaribu bila mafanikio kutetea "legacy"?
Tunaposema hayati Magufuli alikuwa mwovu, katili, fisadi, muuaji, mwizi, mwongo - tuna ushahidi kamili na mzito kuthibitisha. Tuko tayari kuupeleka kwenye Mahakama ya duniani na hata ya mbinguni.
NB: Kujenga barabara au miundo mbinu hakumsaidii wala kumkinga na tuhuma na makosa tajwa.
Kwa sasa tuanze na hizo kwanza.