Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa kupata Rais kama Magufuli mwenye makali zaidi

Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa kupata Rais kama Magufuli mwenye makali zaidi

Evidences zinajenga facts.

Katika utawala huo, shutuma za wachache ni nyingi, na ni wale wenye access na ulaji wa keki kimasihara.

Wamejenga chuki kwa kukataliwa access hiyo na sasa wanatukia access waliyonyimwa before kuwapofusha wananchi ili wao waendelee kula nchi pamoja na wenye nchi!

Weka shutuma moja, back it up na evidence!

Mfano, ukisema, awamu hii wanapiga sana, unasema ushahidi, rejea ripoti ya CAG;
  • TTCL hawajui wanayemdai tzs 21.5bn
  • SGR analipwa fidia ya tzs 4trillion kwa kucheleweshewa malipo
  • Magari yaliyokwisha lipiwa tzs 35bn hayajulikani yalipo.
  • Tzs 1.7trillion, zimekwapuliwa tu kiholela
  • Tzs 900bn inayotakiwa kulipwa kama faini ya ucheleweshaji wa mradi wa Bwawa la Nyerere, hakuna anayedai kutoka serikalini na shirikani
  • Tzs 1.28trillion, waziri wa fedha kakopa tu kiholela, bunge halina habari na hazijulikani ni za nini na ziko wapi!
  • Tozo, hakuna muendelezo wa nini kinapatikana na nini kimefanyika kipya

Na listi inaendelea...
Vema. (Ndicho nilichofanya), lakini haidhuru kitu turudie.

NB: Tunakubaliana kwamba tuhuma na majibu vijengwe na facts. Hakuna kuhamisha magoli!

Haya yote hapa chini yalitokea chini/ndani ya mwaka wa KWANZA wa Utawala wa hayati Magufuli:-

1. Januari 26, 2016 - Waziri wa Habari wa Serikali ya hayati, mh Nape anatangaza bungeni rasmi kupigwa marufuku kwa "Bunge Live". Anasema vyombo binafsi vinaweza kurusha live. Mh Nape anasema sababu ni ukubwa wa gharama za TBC kujiendesha.

2. Wiki chache baadaye, Waziri Mkuu Mh Majaliwa anasema Serikali ya Magufuli imepiga marufuku pia vyombo vyote binafsi kurusha bunge live.

3. 26 Agosti 2016, Sheria tata na kandamizi ya Habari- Media Services Act inabadilishwa kwa kuwekewa vipingele vinavyoua uhuru wa kupata na kutoa habari;

4. 07/06/2016 Serikali ya Magufuli inapiga marufuku mikutano yote ya siasa (isipokuwa ya CCM tu).
Katazo hilo lilikuwa haramu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.

Kwa hiyo msingi wa hoja yangu kuwa Tanzania haihataji rais mwingine mfano wa hayati Magufuli unatokana na mambo hayo manne juu, miongoni mwa mengi.

Sasa kwa mujibu wa hoja zako kuwa watu "wachache", "waliokataliwa ulaji" (unatuhumu bila ushahidi), ndio waliompinga Mwendazake, sio kweli wala sahihi.

Twende kuchambua facts na evidence..

1. Hebu tueleze hapa, ni nani "wengi" waliofaidika na hizo Sheria na hizo marufuku?

2. Ni kwa vipi hizo 4 zililisaidia Taifa, kuongeza pato la Taifa; kuondoa umaskini, ujinga na maradhi?

3. Ni vipi hizo zilisaidia kupambana na rushwa, ufisadi na upigaji?

4. Ni vipi ziliboresha utawala bora wa Serikali na uwajibikaji wa Serikali kwa Wananchi wa Tanzania?

5. Ni vipi zilikuza ustawi, demokrasia na utengamano wa jamii na Taifa?

Kama hazikuwa na faida na tija kwa Taifa na kesho ya nchi yetu, inakuwaje mnajaribu bila mafanikio kutetea "legacy"?

Tunaposema hayati Magufuli alikuwa mwovu, katili, fisadi, muuaji, mwizi, mwongo - tuna ushahidi kamili na mzito kuthibitisha. Tuko tayari kuupeleka kwenye Mahakama ya duniani na hata ya mbinguni.

NB: Kujenga barabara au miundo mbinu hakumsaidii wala kumkinga na tuhuma na makosa tajwa.

Kwa sasa tuanze na hizo kwanza.
 
Tunaposema hayati Magufuli alikuwa mwovu, katili, fisadi, muuaji, mwizi, mwongo- tuna ushahidi. Tuko tayari kuupeleka kwenye Mahakama ya duniani na hata ya mbinguni.
NB: Kujenga barabara au miundo mbinu hakumsaidii wala kumkinga na tuhuma na makosa tajwa.

Kwa sasa tuanzie na hizo kwanza.
Umeandika kwa vituo, nimekuelewa.

Nijibu hitimisho ambalo linabeba maana nzima ya jibu lako, zaidi inaonesha nia hasa ya hoja yako.

Umeuliza maswali ambayo hata nikitoa majibu yake, hakuna namba wala data za kuyathibitisha, hivyo nitayaacha hivyo ili kufupisha mjadala.

Hitimisho lako, linatoa TUHUMA kadhaa ambazo umedai ushahidi wake unaweza kupelekwa nje na mbinguni;
  • Ukatili, huna ushahidi bado
  • Uovu, huna ushahidi
  • Ufisadi, hujathibitisha
  • Uuaji, huna ushahidi
  • Wizi, hujathibitisha
  • Uwongo, weka ushahidi ubaoni
Vyote vinabaki kuwa hearsay kama hakuna hata mmoja aliyejaribu tu hata kwenda MAHAKAMANI sasa kushtaki kwa lolote, zaidi ni kwenda kudai pesa walizozitoa wenyewe wakitetea uhuru wao.

Kama serikali ya sasa ina tenda haki, na ni salama sana, angeanza LISU kusimama mahakamani, kisha walioonewa wote kuwa na vyeti feki, kisha walitumbuliwa kwa kuonewa, wangeenda kuishtaki serikali, kisha tukaiona NGUVU na UHURU wa mahakama kwenye serikali hii ukifanya kazi.

Ajabu ni kwamba, serikali ya viongozi wale wale, ndo inajihukumu na kuanza kushughulikia hearsay, kuwa tumewarudisha vyeti feki, Lisu kalipwa, wezi na mafisadi tumewaachia, wauza dawa tumewatoa! Wote sio wa kuganga njaa mtaani.

Kama kuna kesi za kubambikwa, unadhani wanaobambikwa ni hao wenye influence kwenye nchi tu? Kwanini hakukuwa na mfumo wa kuchunguza hukumu zote, namaanisha zote, kisha utaratibu wa kisheria ukafuatwa, tukaambiwa? Hapo mpaka waliopewa kesi za uongo kwaajili ya kugombea mahusiano watoke?

Mwisho wa siku, collectively, tuliona improvement kubwa, ambayo ni positive HASA kwa sisi walala hoi na improvement hiyo hiyo ndio ilikuwa negative, chungu sana kwa mabwanyenye.
-Leo, 10,000 haina nguvu sokoni ila tabu kuipata. Wanaoumia na hao ambao 10,000 inaweza badili maisha yao.
- Wenye kushindana kununua range, kuhonga LCs, 10,000 ni nini kwao?
 
Habari JF, Ukitaka kuliongoza taifa la Tanzania na kuliletea maendeleo ni lazima uwe in mtu mkali. maono na Mwenye msimamo. Tanzania ina asilimia kubwa ya watu wa aina 3:-

1. Wavivu - hawapendi kujituma kufanya kazi

2. Uwezo Mdogo wa kufikiri -Elimu kwa Tanzania haiwakomboi Uwezo wa alie prof ,PHD ,degree ukitoa aile kujua vitu vingi linapokuja suala la kufikiri hawatofautiana sana .

3. Wanapenda starehe sana

Sasa kuongoza watu wenye sifa hizo huhitaji sana kuwashirikisha ,unacho hitaji ni kuwaongoza njia sahihi .

Ukiachana na tuhuma alizopewa Hayati JPM ambazo hazina Ukweli wala ushahidi wowote alijitahidi sana .

Hivyo kuna haja ya kumpata mwingine Mwenye makali zaidi tuweze piga hatua zaidi .
Hizo tuhuma ni yeye mwenyewe Rais ndiye mwenye mamlaka ya kikatiba ya kuzitolea maelezo. Au hujui Rais wajibu wake mkuu ni nini? Siyo kuwa mkali. Ni kuongoza kwa mujibu wa Katiba na sheria!
 
Habari JF, Ukitaka kuliongoza taifa la Tanzania na kuliletea maendeleo ni lazima uwe in mtu mkali. maono na Mwenye msimamo. Tanzania ina asilimia kubwa ya watu wa aina 3:-

1. Wavivu - hawapendi kujituma kufanya kazi

2. Uwezo Mdogo wa kufikiri -Elimu kwa Tanzania haiwakomboi Uwezo wa alie prof ,PHD ,degree ukitoa aile kujua vitu vingi linapokuja suala la kufikiri hawatofautiana sana .

3. Wanapenda starehe sana

Sasa kuongoza watu wenye sifa hizo huhitaji sana kuwashirikisha ,unacho hitaji ni kuwaongoza njia sahihi .

Ukiachana na tuhuma alizopewa Hayati JPM ambazo hazina Ukweli wala ushahidi wowote alijitahidi sana .

Hivyo kuna haja ya kumpata mwingine Mwenye makali zaidi tuweze piga hatua zaidi .
No no no hatuhitaji dictator tena. Kidogo tuuawe wote lilikuwa swala la mda tu. Hivj kweli unamtandika binadamu mwenzio lisasi 30 bila huruma eti ndo tunataka mtu kama huyo
 
Mbona unaonyesha utoto ndugu? kweli inaonyesha hampo serious kwenye hayo madai mazito ya Tanzania kuwahi kuwepo kiongozi ambaye alikuwa muuwaji, sasa hapo kinachokufanya mtu mzima na mwenye akili timamu kucheka ni kipi?
Alizidi kuuwa......hivyo tu. Cheko nalo linaleta makasiriko
 
Vyote vinabaki kuwa hearsay kama hakuna hata mmoja aliyejaribu tu hata kwenda MAHAKAMANI sasa kushtaki kwa lolote, zaidi ni kwenda kudai pesa walizozitoa wenyewe wakitetea uhuru wao.
Katiba na Sheria zetu haziruhusu Rais kushtakiwa kwenye Mahakama zetu.

Na ndio maana hujaona Magufuli akishtakiwa ktk mahama zetu na, hata alipovunja Katiba, akaiba chaguzi za 2019 na 2020 nk nk; hakushtakiwa Mahakamani. Msitafsiri kinyume au vibaya; ushahidi upo, tena mwingi mno ila tu hakuna instruments.

Pia Usisahau wakati wa utawala wake "aliwaongeza wengine" kwenye list ya Kinga ya Kutoshtakiwa.

Ndugu, Haikanushiki kuwa Mwendazake alinuia na kujipanga kwa uovu usiomithilika, lakini Mwenyezi MUNGU akaingilia kati, akamtoa.

Narudia tena sio kwamba hakuna ushahidi, upo wa kutosha - ndio maana tunataka na tunahitaji Katiba Mpya sana.
Hearsay vs Facts vitajitenga kwa spidi ya jet.

Tukiipata hiyo Katiba Mpya mtajua uko ushahidi kiasi gani! Pia mtajua the extent ya uovu wa miaka yake 5 ya Urais 2015-March 2021.
 
Kama serikali ya sasa ina tenda haki, na ni salama sana, angeanza LISU kusimama mahakamani, kisha walioonewa wote kuwa na vyeti feki, kisha walitumbuliwa kwa kuonewa, wangeenda kuishtaki serikali, kisha tukaiona NGUVU na UHURU wa mahakama kwenye serikali hii ukifanya kazi.
Usiniwekee maneno mdomoni.
Sijasema mahali popote kuwa serikali ya sasa inatenda haki; au kwamba nakubaliana na mambo yake.

Otherwise, kwa nini kila mahali consistently nimekuwa nikidai na kuhamasisha tupate Katiba Mpya?
 
Mwisho wa siku, collectively, tuliona improvement kubwa, ambayo ni positive HASA kwa sisi walala hoi na improvement hiyo hiyo ndio ilikuwa negative, chungu sana kwa mabwanyenye.
Umekiri huwezi kujibu hoja zangu kwa facts.
Pia umekiri kuwa Serikali ya sasa ina mapungufu, kama ilivyokuwa ya Mwendazake.

Sasa hiyo "improvement" unayoisemea umeipata wapi kama sio hisia tu?
Maana biashara, uchumi, maisha viliporomoka wakati wa Magufuli kuliko ilivyo Leo. Takwimu za ndani na nje zinathibitisha hilo.
 
HASA kwa sisi walala hoi na improvement hiyo hiyo ndio ilikuwa negative, chungu sana kwa mabwanyenye.
Usikubali kuitwa mlalahoi, mvuja jasho, mnyonge na mengine kama hayo.
Hayo ni majina Wakomunist/Wajamaa waliwaita ili kuutweza utu wenu na kuwafanya pawns of evil.

Kwa fikra na mawazo yako hayo, wewe umefanyika kuwa silaha dhidi yako mwenyewe.
Ukombozi wako wa fikra ni hatua ya kwanza ili uwe huru kiuchumi, kijamii nk. Uchaguzi ni wako.
 
...I mean Shoga mwenye maono aje kumuondoa huyu Mama.
 
Ili aje kurundika wahitimu bila kuwaajiri kama MAGUFULI? Hatumhitaji na bora Mungu alivyiingilia kati.
 
Habari JF, Ukitaka kuliongoza taifa la Tanzania na kuliletea maendeleo ni lazima uwe in mtu mkali. maono na Mwenye msimamo. Tanzania ina asilimia kubwa ya watu wa aina 3:-

1. Wavivu - hawapendi kujituma kufanya kazi

2. Uwezo Mdogo wa kufikiri -Elimu kwa Tanzania haiwakomboi Uwezo wa alie prof ,PHD ,degree ukitoa aile kujua vitu vingi linapokuja suala la kufikiri hawatofautiana sana .

3. Wanapenda starehe sana

Sasa kuongoza watu wenye sifa hizo huhitaji sana kuwashirikisha ,unacho hitaji ni kuwaongoza njia sahihi .

Ukiachana na tuhuma alizopewa Hayati JPM ambazo hazina Ukweli wala ushahidi wowote alijitahidi sana .

Hivyo kuna haja ya kumpata mwingine Mwenye makali zaidi tuweze piga hatua zaidi .
Kweli Mungu fundi.
Alijua kututetea waja wake, akatenda jambo na kuturudishia uhuru wetu 17th March 2021.
Sasa imebaki misukule yake inahangaika kutafuta chakula.
Yalizoea kunywa damu za watu wanaowateka na kuwaua, kuwatesa
 
Back
Top Bottom