Tanzania bado ina uhitaji mkubwa wa kupata Rais kama Magufuli mwenye makali zaidi

Unaelewa maana ya propaganda ?
 
Pia kipindi cha Magufuli ndio uchumi wetu ulikuwa kwa spidi ndogo zaidi kuliko cha Kikwete na Mkapa, aliharibu zaidi kuliko alivyosaidia
Sahihi kabisa.

Cheki World Bank & other international reports kiwango cha ukuaji uchumi kilifikia ukuaji wa 2%! Ni aibu tupu!

Na ripoti ya kwanza tu baada ya kifo chake tukaambiwa wanajitahidi kipande kufikia 4%. Je Lini kilishuka? Magufuli wala serikali yake hawakuwahi kutuarifu.

Ina maana kilishuka lakini walikuwa wanatumia propganda na manipulations methods kudanganya wananchi. Typical of dictators.

Mfano, faida na magawio hewa ya Mashirika ya umma, Tanzania ya viwanda (hewa) nk nk
 
Pia kipindi cha Magufuli ndio uchumi wetu ulikuwa kwa spidi ndogo zaidi kuliko cha Kikwete na Mkapa, aliharibu zaidi kuliko alivyosaidia
Weka records za uchumi kabla na baada ya Covid-19...kuna inchi zilifikia negative % growth while sisi tukiendelea kua na +ve...we cant blame effect za covid on him...it was a world wide issue..
 
I support this post with a hundred bags of cement 🙌🙌
 
Naunga mkono hoja, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kuwa na kiongozi legelege na anayetanguliza democrasia ya kuombea ela za wazungu mbele.
 
Asanteeeee subscribed and noted for further references
 
Bado unatamani rais muuaji katili kama lile jitu!
The man was totally failure
Angefaa kuwa rais kabla ya Nyerere rais wa watu wasio julikana.Kwa nyakati hizi hana nafasi hata kuongoza kijiji. Ukimpima jiwe na Dr.Msukuma std7 utaona Msukuma anamzidi jiwe kwa weledi tena kwa mbali mno.
 
Makali ya ujinga kichwani
 
Mfuate
 
namba moja(1)

tupo kijiweni apa tangu saanane mchana adi saiz tunaijadiri mechi ya simba ya juzi kati
 
mfuate aliko akuongoze huko, kima lisilo na haya
 
Hata kama hayo yote uliyoyasema ni kweli - kitu ambacho si kweli- makali ya rais si suluhisho.

Kwa sababu, makali ya rais hayatatui matatizo ya kimsingi ya Watanzania, akifa rais na makali yake yatakufa.

Nchi inahitaji utatuzi endelevu, uliokaa kimfumo zaidi, si kumuangalia mtu mmoja kama rais.

Rais akipigwa na radi akajifia zake mtafanya nini?

Yani hamjajifunza tu katika kifo cha Magufuli kwamba kumtegemea mtu ni ujinga?
 
Weka records za uchumi kabla na baada ya Covid-19...kuna inchi zilifikia negative % growth while sisi tukiendelea kua na +ve...we cant blame effect za covid on him...it was a world wide issue..
Kwa nini basi hayati na wenzake hawakuweka wazi hizo takwimu mapema au kwa wakati? Why?

Unafahamu vema kuwa Mwendazake pia alikuja na sheria "yake" ya Takwimu, na ile nyingine ya Habari? Zote zilikuwa na malengo hasi na kwa nia ovu kwa Taifa.

Hivi Kazi ya Waziri wa Fedha ni nini? Kwa nini hakuweka bayana hiyo drop the whole of 2020?
Baada tu ya kifo cha hayati Magufuli, nakambuka niliwahi kusoma/kusikia maoni na makala kadhaa mwaka 2021 baadhi ya watu walidai "Magufuli kafariki, uchumi umeporomoka toka 6% hadi 4%..." Really?
 
Siyo kweli. Bali uongozi wa nchi unahitaji kipawa, busara, hekima, uvumilivu na ucha Mungu kwa matendo. Vitu vyote hivi mtu huzaliwa navyo.

Magufuli hakuwa na chochote kati ya hivyo ndiyo maana alitawala kqa UKATILI na kufanya mambo ya UKICHAA mengi hadi na yeye AKAFA kwa kulazimisha kupambana na COVID-19 kwa kujifukiza badala ya kutumia njia za kisayansi
 
Nimekuelewa vema mkuu
 
Sahihi kabisa Kiranga.

Sijui kwa nini hawataki kuona jambo la wazi na rahisi kama hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…