Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

😀😀 na serikali waseme wapitishe sheria ya kuaguza gari isiyopungua miaka 10 toka kuzalishwa kwak. Idadi itakuwa chini zaidi
 
Moja ya kipimo cha umasikini au utajiri (poverty & wealth ranking) ni kuangalia mali mtu anazomiliki kwa mfano nyumba (ya miti & udongo, ya matofali, nyasi fulu suti etc), baiskeli, Pikipiki, gari etc... Mfano kama wewe humiliki hata bodaboda au baiskeli, huna nyumba hata ya matope na nyasi wewe tayari una indicators za umasikini...
 
[emoji3][emoji3] na serikali waseme wapitishe sheria ya kuaguza gari isiyopungua miaka 10 toka kuzalishwa kwak. Idadi itakuwa chini zaidi
Sana tutapokezana za humu humu ndani maana waagizaji watakuwa wachache.
Fikiria Fuso ya mwaka 1988 kuiingiza nchini ujipange na pesa si chini ya million 75+. Je ya mwaka 2012 utailipia pesa ngapi.[emoji28]
 
Tatizo ni kodi zilizowekwa ndio hukwamisha watu wasinunue wengi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata kama ni kodi, bado haiondoi hoja ya jamaa....
Wenzetu mbona wanannunua mapya, gari ist inauzwa usd 25,000...

Kwahiyo idadi ya mdau aliyotaja, kuna watu wanamiliki gari zaidi ya moja....

Kwa kukadiria, watanzania wenye magari hawazidi 300,000
 
Sana tutapokezana za humu humu ndani maana waagizaji watakuwa wachache.
Fikiria Fuso ya mwaka 1988 kuiingiza nchini ujipange na pesa si chini ya million 75+. Je ya mwaka 2012 utailipia pesa ngapi.[emoji28]
Acha masikhara mkuu😂. Ya mwaka 1988 ni 75+m? Hatari sana
 
Hawataenda peke yao ujue, wataenda na waliowasaidia na pia hata wananchi wengine wote ambao pamoja na kuona yaliyokuwa yanatendeka hawakuchukua hatua yoooteee
Kweli kabisa embu angalia ule uchaguzi wa 2020 watu wanaiba hadharani na bado wanaongoza serikali mpaka leo kupitia wizi wa kurana viongozi wa dini wapo kimya inamaana kuiba kumekuwa halali
 
Sana tutapokezana za humu humu ndani maana waagizaji watakuwa wachache.
Fikiria Fuso ya mwaka 1988 kuiingiza nchini ujipange na pesa si chini ya million 75+. Je ya mwaka 2012 utailipia pesa ngapi.[emoji28]
Ila hela nzuri sana, ukiwa na gari ya mwaka kama 2019 au 2021 ujue ina rahaa yake .. sema ndio ivyo acha tupambane na za 2000 hizi kwenye vipato vya wengi 😀😀😀😀.. kama hiyo ya 1988 itauzwa 75 million andaa kibunda haswaaa kama unataka ya 2012
 
Mkuu umesema vizuri na uchambuzi wako ni sahihi kabisa; ila kuwa ni kipimo cha umaskini utakuwa umepitiliza
 
Hapo kwenye paragraph ya pili kwamba barabara hazitoshi sikubaliani na wewe kabisa kwa sababu Watanzania wengi zaidi wako vijijini, hivyo walio vijijini wanahitaji vyombo vya usafiri kama pick up, matrekta, Kenta, Fuso nk ili waweze kubeba pembejeo na mazao kwa urahisi. Kwenye kodi kubwa mpaka kuzidi bei ya kununua gari na kusafirisha nakubaliana na wewe. Kwa mfano ilitakiwa serikali ihamasishe ununuzi wa magari ya kutumika kwenye kilimo na ufugaji huko vijijini kwa kuweka kodi rahisi sana say 40% ya bei ya hayo magari kama pick up, Kenta, Fuso etc... Matrekta, boza za maji, mitambo mbalimbali kodi ingekuwa 10 - 15 %ili kilimo kiwe mechanized.
 
KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI KODI ABOVE ALL CCM AKILI ILE ILE MIAKA NENDA RUDI
 
Unaonaje muasisi wa jf Maxence Melo ukianzisha mchakato wa kuchangisha japo tsh elfu 2 kwa mwezi kwa kila member wa Jf, na kusaidia kutununulia magari wale tusiyonayo ili kuongeza uagizaji na pia kupunguza umaskini wa watanzania?

cc Maxence Melo
 
Ni kweli lakini huko vijijini kuna barabara? Hebu jiulize barabara zilizopo kijijini kwenu ukiwa na gari litadumu??? Utaweza kuwa na gari la kawaida kijijini kwenu?

Nchi za wenzetu wana barabara zinazoopitika vizuri mpaka vijijini ndio maana magari wanayo.

Lakini pia vijiji vya tanzania wengi wanahali duni ambapo sidhani kama wanaweza kuhimili shs 3,400 ya lita moja ya mafuta. Kimsingi uchumi wa magari upo mijini, vijijini wakinayo wachache kusafirisha wengine inatosha maana wakulima na wafugaji wengi hawawezi kumudu gharama za kumiliki gari wacha tu manunuzi.
 
Kodi

Gari nayotaka Kodi yake ni milion 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…