Tanzania haijapate Mwinjilisti Mwingine mwenye nguvu kitaifa kama Moses Kulola sababu aliondoka bila kukabidhi mtu kipawa alichokuwa nacho

Kazi ipo
 
Mchungaji Moses Magembe ana mielekeo ileile kama mzee Kulola.
Sidhani yeye kajikita zaidi kwenye doctorines zaidi za kanisa

Uteteaji wa usahihi wa doctorines za kanisa sio uinjilisti, kajikita kwenye Eneo la uteteaji wa imani ya kanisa

Anaangalia makanisa mengine au kanisa ililopo liwe lake au mengine yamepotoka wapi na kukemea huo upotofu wa ndani ya kanisa lake au mengine

Kifupi Kwa uinjilisti ni kidogo mno tu kufikia viwango vya akina Moses Kulola,Billy Graham au Renhard Bonke vya kujikita tu kwenye injili ya kuleta wokovu tu watu watubu dhambi na kuacha hajafikia huko yeye huge uza platform apewazo kuwa jukwaa la elimu ya uteteaji wa doctrines yaan apologetics platform!!!!

Yeye yuko kundi la Apologetics preachers anbao kazi yao kuwinda mafundisho.potofu yako wapi na kuyajengea mahubiri viwanja vya mikutano ya nje na ndani akipewa nafasi

Yawezekana ana hamu ya uinjilisti lakini bado haujamwingia barabara may be because ni mchungaji kuna vitu kichwani vinaingiliana .Kuchanganya uchungaji na uinjilisti kunampa shida

Uinjilisti ni ofisi inajitegemea na sio ya mchezo.Inataka full time commitment kufikia viwango vya akina Kulola sio part time.Yeye anaifanya part time
 
Ndoto tu imekukimbiza tena hata hukuiota wewe ?
hii ilisababishwa na mdogo wangu wa kike kuota ndoto nzito juu ya mwamposa.

Aiseee baada ya hapo nika relate ile ndoto na baadhi ya vitendo vya mwamposa madhabahuni

nika stop kuabudu kwake
 
Mchungaji Moses Magembe ana mielekeo ileile kama mzee Kulola.
No Magembe yuko ki doctrines zaidi za dini tofauti na Kulola mhubiri wa wokovu sio dini au Bonke au Billy Graham waamini wokovu sio dini
Magembe dini iko mbele kama tai

Kwa uchungaji yuko OK

Uinjilisti bado
 
Jmn na mahubiri ya FGBF ni injili tupu.....ila kiongozi wa hili kanisa mbona haonekani anamatatizo Gani????
 
Hacha kwenda kanisani au nyumba za ibada kwa kufata matukio. Ndio nyinyi mnaenda kanisani kuangalia Mama Fulani kaanguka mapeo ili mradi muwachungulie wa mama wanavyodondoka vichupi juuu
 
Hacha kwenda kanisani au nyumba za ibada kwa kufata matukio. Ndio nyinyi mnaenda kanisani kuangalia Mama Fulani kaanguka mapeo ili mradi muwachungulie wa mama wanavyodondoka vichupi juuu
Hoja yako haiendani na mada
 
Jmn na mahubiri ya FGBF ni injili tupu.....ila kiongozi wa hili kanisa mbona haonekani anamatatizo Gani????
Mahubiri ya FBGF ni ya kichungaji sio kiinjilisti

Uinjilisti haufanywi ndani ya kanisa ni mitaani na vijijini kusiko na waliookoka

Kanisani ni mahibiri ya kujenga waumini ambao tayari wameokoka sio uinjilisti!!
 
Niseme tu, nyakati zimebadilika sana. Leo hii hata kama angekuwepo Moses Kulola bado angepata taabu sana kuhubiri aina yake ya Injili. Baada ya kuja uchafuzi wa Injili ya wasaka afya na mafanikio, masikio ya watu wote, wapagani, Waislamu kwa Wakristo wameelekeza mioyo yao huko. Ndio maana utaona wafuasi wengi wa akina kuhani Musa, Mwamposa nk ni Waumini wa imani tofauti. Wahubiri wanaofuata maagizo ya Kristo kwa kuhubiri toba wapi ila hawawezi kuwa na mega churches, ni makusanyiko madogo mno. Matapeli wa Injili ndio wanawake, sawa sawa na Kristo alivyosema itakuwa nyakati za mwisho.

Hivyo hoja sio Kulola kutokabidhi kipawa kwa sababu afanyaye hivyo ni Roho Mtakatifu wala si mwanadamu. Tatizo hapa ni watu kupenda mafundisho ya uongo. Nakumbuka kwenye uchaguzi wa mwisho kabla ya kifo chake kulikuwa na njama za maaskofu kumng'oa Kulola. Sasa ndio uone uasi ulianzia humo humo ndani, na hao waliotaka kumng'oa ndio wameshika kijiti hii leo. Kutwa kucha mahakamani kwa kesi za wizi na kugombania madaraka. Vipofu wanawezaje kuwaongoza vipofu wenzao?
 
ulimpima vipi mwinjilisti Moses kulola ukajua ana nguvu,,,,,,,??au kwa sababu alikuwa anakugusa ww?.....walokole bhana.....watu wa ulimwengu wa roho...🤣
 
ulimpima vipi mwinjilisti Moses kulola ukajua ana nguvu,,,,,,,??au kwa sababu alikuwa anakugusa ww?.....walokole bhana.....watu wa ulimwengu wa roho...🤣
Matunda ya idadi ya wanaookoka mikutano yake

Biblia inatamka wazi mtawatambua kwa matunda yao

Mwinjilisti hapimwi kwa jina kujiita Mwinjilisti Moses aliketa maefu kwa kanisa kupitia huduma yake

Uinjilisti sio cheo ni kazi
 
Matunda ya idadi ya wanaookoka mikutano yake

Biblia inatamka wazi mtawatambua kwa matunda yao

Mwinjilisti hapimwi kwa jina kujiita Mwinjilisti Moses aliketa maefu kwa kanisa kupitia huduma yake

Uinjilisti sio cheo ni kazi
nisaidie ivi neno kuokoka lipo kwenye msitari upi ndani ya biblia na nini maana ya kuokoka maana na siku nying nafikiria hzo mambo nieleweshe kwa bible
 
Boss Yani kiufupi mzee kolola alitumwa na Mungu akutangaza miujiza ya maji Wala nini ni neno tu


Kama angetaka utajiri mzee angekuwa bilionea ila kafa na maisha ya kawaida tu apumzike kwa amani mzee wetu wa yooo yooo
 
Humjui BULUDOZA wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…