Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%


Hakuna namna, either anakuja mwingine kama JPM kurekebisha mahesabu, kubana matumizi, kuweka vipaumbele sahihi kwa nguvu za kidikteta (hakuna mbadala) au tutauzwa jumla jumla.

Options nyingine ni kama ya watu wa Sri Lanka.
 
Acha ujinga basi ndugu... Em fanya 23.3/6=...!? Jibu ndo ilibidi iwe walau to the very least nyongeza la kila mwaka.
Haki imepunjwa muda mrefuu. Alafu hizi roho mbaya !! Why!??
 
Wakati JK anakusanya mapato ya kila mwezi billion 800 na kulipa mishahara bilioni 700 aliwezaje, mwendazake aliwaingizia matope vichwani mwenu

Tuambie aliwezaje? Jaribu kuweka matusi pembeni.


Tuelezee na kutufafanulia kiundani aliwezaje?
 
EEeeeeHeeee!

Umesahau, si watakwenda kukopa?

Wanakutangazia kila siku hapa kwamba bado tunao uhimilivu wa kukopa! EEeeeHEeeHeee!

Uhimilivu, uvumilivu wao utafikia kikomo. Wakiangalia speed ya tunavyokopa na uwezo wetu wa kuwalipa, matumizi mengi tunayoyaongeza kila siku, ufisadi.

Ni swala la muda.
 
Kuongezeka kuna cha chini maana yake bima vingine vinaongezeka.lakini calculation za PAYE zinatofautiana kwa kima cha chini na juu. Hii itawasaidia sanasana walio na kima cha chini. Hivyo lazima tufahamu kima cha chini na cha juu ni kiasi gani
 
Unapingana na hoja ya mheshimiwa Rais...?, Ubongo wako umejaa makamasi

Rais ni mtumishi wa Watanzania. Tumemuajiri kama unavyoajiri mfanyakazi kwenye kampuni yako.

Mfanyakazi wako asipofanya kazi yake vizuri, utabaki kimya, biashara yako ifilisike?
 
kwani 23.3% kwakima cha chini ni sawa na sh ngapi?
 
Mkuu
Mi Binafsi sioni tena kutangazwa bkwa miradi ile mikubwa ya kimkakati!
Sijui nini kumetokea hadi sasa!
NAJIULIZA
Mwenye majibu naomba!!
Miradi gani tena?kwani aliyoiacha meko inaendelea, ambayo mingi aliianzisha kwa pupa, sasa kazi kubwa ipo kwenye kuitafutia pesa, na màma anajitahidi, inaendelea, bora huyu ana sema wazi kuwa nina kopa kuliko yule muongo kila siku anasema tunaijenga kwa pesa zetu kumbe uongo tupu.MUNGU FUndi
 
Wewe ilivyo kichwa maji unahisi Serikali huwa inaweka wazi mikopo yote! Huyo mama ameshakopa hela nyingi sana tokea aingie! Na kwa taarifa yako yale makusanyo ya TRA ni uongo ndo maana saizi wanakazania matumizi ya EFD lakini kipindi anaingia aliwaaminisha wafanya biashara wawe huru kuonesha yeye ni mshikaji! Na kingine umeona kwenye mafuta wameingiza bilioni 100 kushusha inflation lakini imeshuka sh 29 tu kwa lita! Imaonesha Serikali haina pesa! Brabra za wanasiasa tu!
 
Acha ujinga basi ndugu... Em fanya 23.3/6=...!? Jibu ndo ilibidi iwe walau to the very least nyongeza la kila mwaka.
Haki imepunjwa muda mrefuu. Alafu hizi roho mbaya !! Why!??
Unaweza tu kumsahihisha mtu bila kuhamaki.....hii ni public forum...kila mmoja yupo huru kutoa maoni yake......lakini kusahihishana kupo.....
 
Uhimilivu, uvumilivu wao utafikia kikomo. Wakiangalia speed ya tunavyokopa na uwezo wetu wa kuwalipa, matumizi mengi tunayoyaongeza kila siku, ufisadi.

Ni swala la muda.
Punguza kuwa nabii wa majanga (prophet of doom). SSH ameamua kuongeza mishahara ni suala zuri kuliko kuumiza mamilioni ya watu wakaishi kwa vinyongo wakati maisha haya ni mafupi.
 
Kikwete alikuwa anakopa ili alipe mshahara! Msidanganye watu hapa kikwete watu walikuwa wanapokea mshahara mpaka tarehe 4! Yule bwana alikuwa zungukuku mkubwa sana!
Wakati JK anakusanya mapato ya kila mwezi billion 800 na kulipa mishahara bilioni 700 aliwezaje, mwendazake aliwaingizia matope vichwani mwenu
 
Ni kawaida dunia nzima iwe wafanyakazi wa serikali au private ndio mfumo juu anaweza kupata 2% tu hata 0% na inakubalika.
Kwa mpangilio huu wa nyongeza za mishahara.Kima cha juu hakuna mfanyakazi atapata zaidi ya laki nne.
 
Endelea kuandika nadharia zako wakati wenzio wanakunja 23%. Haya mawazo ya KIFALA sana na ndiyo alikuwa nayo yule DIKTETA wa Chato.

Hebu tupisheni tunajuwa tutapata wapi hizo fedha za kuwalipa wafanyakazi
Msikilize na umtizame mmoja wa washiriki wa mchakato wa upandishwaji mishahara. Anaseme si kwa kila daraja watapata 23% japo mama samia amejitahidi sana kuanxia mwaka jana mambo ambayo ameyafanya kwenye vipato vya watumishi si madogo
 

Attachments

  • VID-20220515-WA0000.mp4
    11.9 MB
Ukumbuke Budget ya Mishahara imeongezeka kwa asilimia 19 hivyo tukiacha ajira mpya wafanyakazi wote wanaweza kupata in average 19% ya mishahara yao ya sasa. Lakini kwa sababu kuna ajira mpya na kuna watakao staafu Nadhani wanaweza pata chini ya hapo kidogo. Kwa kuweza kuongeza 19% ya budget ya Mishahara lazima tukubali Raisi Kaupiga mwingi.
 
Jana nilimsoma sana jamaa mmoja wa kuitwa DINHO, nikaijuliza serikali ina mapato gani ili kuweza kuongeza 23.3% flat rate. Yaani anywpata 3,000,000 aongezewe 23.3% sawa na yule wa 270,000? Kwamba mtu wa 3mil aongezewe almost 700k kweli? Kwa uchumi gani tulionao.

Mleta mada naamini upo sahihi kabisa. It'll never be flat rate, lakini pia huo uchumi wetu ni mdogo sana.
 
Mpangilio huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…