Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Chochote kitakachofanywa na serikali wa kulalamika mtakuwepo na wa kupongezwa na kufurahia maamuzi watakuwepo pia. Hakuna wa kumfurahisha kila mtu.
Utalipia vipi, issue sio kufurahishana, ni kuweka bayana mikakati yenu jinsi mtakavyoilipia. Nchi zote zinafanya hivyo. Zinaongeza matumizi ila zinakuwa waxi kuhusu wapi watapata, kuchukua hizo pesa.
 
Muulize waziri haya maswali yako, ingawa atakushangaa tu.
Huyu huyu wa sasa! Nilikuwa na imani na Dr Mpango, yeye na JPM walipanga vitu vyote. Ila yuko kimya.

Huyu wa sasa atasema lolote, sababu hayuko vizuri kwenye practical, amesahau maisha ya Watanzania wengi. Japo hata yeye ametokea familia maskini sana. Lengo lake kuu ni kukaa madarakani.

Unafikiri nchi zilizoendelea unaweza kusema hivi bila kusema utatoa wapi pesa za kulipia mipango yako.
 
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.

Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.

Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.

Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.

Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!

Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!

Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!

Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!

Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!

Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!

Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!
Mapunguani huwa hamuwezi kuisha,unavyoropoka sasa utadhani uchumi uko stagnant..

Unapayuka utadhani huwa hufuatilii hata taarifa za mwenendo wa Uchumi,mapato nk wa Serikali..

Ndio maana Samia aliwahi kuwaambia watu dizaini yako mna akili ndogo Sana. 👇

Screenshot_20220406-163449.png
 
Ndugu mtoa mada una point ya msingi ingawa bahati mbaya mada yako imevamiwa na waimba ngonjera.......lakini kimantiki hili ongezeko halipatani na uhalisia....nadhani ni muendelezo wa wanasiasa wa nchi kujiandalia mazingira ya uchaguzi ujao......bila kuangalia matokeo ya maamuzi yao.......haya ni moja ya matokeo ya kuwapa nafasi ya kufanya maamuzi watu wenye uwezo mdogo wa akili kwa niaba ya taifa kwa ujumla......
Una akili timamu kweli? Average ya makusanyo kwa mwezi ni zaidi ya Til.1.8 ,mtoa mada kasema ni til.1.5 unaona yuko sawa?

Pili je Uchumi umesimama au unashuka au uko stagnant?

Muwe mnafikiria kabla ya kuropoka.
 
Lakini nakubaliana na wewe kwenye eneo la uzalishaji na kuongeza fedha za kigeni bila kutegemea utalii, mikopo na misaada peke yake.
Watu watasema tumeachwa kiteknolojia.
Lakini kuna maeneo tunaweza. Kwa mfano kuna vitu vina soko sana humu nchini na tunaweza kuzalisha badala ya kutumia akiba ya fedha za kigeni kununua. Kuna vitu kama vile:
1. Ngano
2. Alizeti
3. Mafuta ya chakula
4. Sukari
5. Samani za maofisini na majumbani
6. Pombe/Vileo za aina mbali mbali
Hivyo vyote Serikali ya mama imeshaanza kuvifanyia Kazi ..

Hiyo mipango sio ya overnight
 
Huyu huyu wa sasa! Nilikuwa na imani na Dr Mpango, yeye na JPM walipanga vitu vyote. Ila yuko kimya.

Huyu wa sasa atasema lolote, sababu hayuko vizuri kwenye practical, amesahau maisha ya Watanzania wengi. Japo hata yeye ametokea familia maskini sana. Lengo lake kuu ni kukaa madarakani.

Unafikiri nchi zilizoendelea unaweza kusema hivi bila kusema utatoa wapi pesa za kulipia mipango yako.
Ndio maana nimekwambia ongea na wenye mamlaka watakwambia pesa watatoa wapi.
 
Kwa ivyo unapambana na inflation ambayo chanzo chake mafuta kwa kuongeza mishahara.

Wakati wakandarasi washaanza kulalamika gharama za kutekeleza miradi zimeongeka kwa sababu ya kupanda kwa mafuta, hiyo inakwenda kuongeza gharama za serikali kwenye kulipia miradi.

Mishahara inaenda kuongeza gharama za admin costs za serikali.

Bei za bidhaa zimepanda maradufu kwenye kila kitu ongezeko la mishahara italeta unafuu kiasi lakini fall in government collection zitakuwepo tu ambazo unategemea kulipia hiyo nyongeza ya mishahara.

Kutokana na hiyo vicious circle ndio maana kila nchi duniani inapambana na bei ya mafuta kwa sababu ndio tatizo la msingi.

Hili sakata la kupambana na inflation mtu ambae kalitolea majibu mazuri ni Zitto nadhani ile ndio direction sahihi.

Hili la kuongeza mishahara ni kujichimbia shimo zaidi na kuacha agenda muhimu. Ufungui nchi kwa kuzurura bali unafungua nchi kwa kuweka easy access ya watu kuweza kuwekeza popote na accesss za kufikia masoko kirahisi au bandari kama ni for exportation.

Swala la uwekezaji wa miundombinu ni chungu lakini hakuna shortcut hakuna nchi duniani iliyokuwa bila ya kufungua access za sehemu mbalimbali nchini kwake; ukisoma historia ya US ni interconnection ya railway ndio iliyopaisha uchumi, ukienda UK canals na baadae railway na nchi nyingine nyingi ni mabarabara; hakuna uchumi unaokuwa bila ya interconnection ya kufikia masoko kirahisi.

Swala hapa kupanga ni kuchagua agenda yako ya kitaifa ya muda mrefu ni nini; sera za awamu ya tano zilikuwa za muda mrefu na maendeleo yanataka sacrifice.

Ni bora utumie tsh1 kupambana na inflation kwa ku stabilise bei ya mafuta which you know is a temporary measure kuliko ujiongezee full time commitments za tsh2 trillion kila mwaka wakati mapato yenyewe wasiwasi.
Umeandika hadithi nyingi za kipumbavu..

Salary increase inakuaje kujichimbia Nchi?

Ukishaweka hayo unayoita mazingira Bora ya kuwekeza then investors wanajileta tuu sio?

Mburula wa uchumi mko wengi ila mnajitia kujua , uchumi sio ushabiki wa Yanga na Simba..

Kwa hivyo huu uwekezaji wa bil.8 ulifikaje Nchini? 👇

Screenshot_20220512-130134.png
 
Kama ni shabiki wa formula1 racing basi unaelewa ule mfumo wa tyre choices ni kama ukuaji wa uchumi na infrastructures investment.

Kwenye race ukiweka hard tyres utaenda polepole lakini utafika mbali ivyo kukupunguzia pit stops.

Ukiweka soft tyres utaenda kasi lakini ufiki mbali ndio maana mara nyingi wanazitumia kwenye qualification tu.

Jamaa anaweza kuwa mbele yako sekundu 20 ukienda kuweka new tyres especially soft au medium unamkata kama kuna laps za kutosha zimebaki.

Same thing kwenye infrastructure project na ukuaji wa uchumi unataka kukua kwa kasi gani ya haraka ndio utakavyowekeza kwa kasi sambamba na infrastructures projects.

Mtu anaweza jenga kiwanda kikubwa Shinyanga kwa target za Tabora, Geita, Musoma, Bukoba na Mwanza kwa sababu kuna easy access ya kufikia masoko yake huko na kwa gharama nafuu. Na uwekezaji unaenda sambasamba na kutengeneza ajira na ongezeko la makusanyo kwa serikali.

Ni hivi ili kuchangamsha Tanzania kiuchumi miradi ya infrastructures sio luxury ni lazima; na kwa hatua za hii serikali inayojiita ya awamu ya hiyo miradi itasimama kwa sababu wanajipa commitment kubwa za kuongeza gov admin expenses badala ya kuangalia bigger picture.
Mna reason kitoto Sana utadhani investment kwenye infrastructure imesimama au haifanyiki..

Pili ,kama investments kwenye infrastructure inachangamsha uchumi,wimbo wa vyuma kukaza ulitoka wapi?

Uchumi hauendeshwi kwa single industry
 
Tafsiri rahisi ya ongezeko la 23% maana yake serikali ina chanzo cha makusanyo ambacho kina zaidi ya 23% ili kukidhi kuhudumia mishahara, posho na malimbikizo ya mshahara toka kwa watumishi wa umma.

Swali, je uwezo wa watumishi wa umma umekuwa na tija kiasi cha ukipita ongezeko la ukuaji wa pato la serikali, unalazimu watumishi kupokea 23% ya kile wanachopokea sasa.

Je, hazina ina mkakati gani wa muda mfupi na muda wa kati ili kuchochea uzalishaji wa sekta binafsi ambapo ndipo kwenye upanuzi wa tax base. Ng'ombe (privately sector) ili atoe maziwa, kuna mazingira ya kulishwa quantitative and qualitative dietary ili atoe maziwa ya kutosha?

Kama ni nyasi kavu msimu wa kiangazi, mmh, tax base utaendelea kuwa finyu sana na tutaendelea kuwa na narrow scope kuwa na tozo chungu mzima kwenye petroli.

Basic assumptions kama ngano tunayoagiza toka Russia na inasafirishwa kwa meli mpaka Tz ni takribani 90% ya mahitaji ya soko la ndani, kwanini hazina na wazara ya kilimo tusiwekeze kwenye commercial farming ya ngano kwa soko la Tz na nchi 8 majirani, ili inapouzwa, say serikali itatoza sh 200 kwenye kila kg inayouzwa ndani na nje ya Tz (Congo, Zambia, Malawi, Uganda, Burundi, Rwanda Madagascar, Comoro)

Likewise, kwanini pamba, korosho, chai, kahawa, cocoa, katani zisiuzwe kama constables products kwa kuchochea industrial processing ili ku-tax kwenye sales ya funal products?

Vinginevyo, mama atapata sifa za kisiasa ila baada ya muda Serikali itashindwa kujiendesha.

Tax revenue ya 1.5tril-2.3 ni ndogo sana.

Lazima serikali iwe sehemu ya kujenga financial instruments/leverage ambazo zitapelekea kununua technology ambayo itaogenza tija na ufanisi kwenye uzalishaji ambako ndipo kwenye vyanzo vya Kodi na kuongeza mzunguko wa fedha.

Weekend njema.
Aliyewadanganya kwamba mapato ya serikali yanatokana na tax revenues pekee ni nani?

Pili namba ndio zinaongea sio maneno,mfano mdogo tuu 👇

Screenshot_20220514-080641.png


Screenshot_20220514-080702.png


Screenshot_20220515-073444.png


Screenshot_20220515-072753.png


Screenshot_20220511-202149.png


Screenshot_20220415-064911.png


Screenshot_20220410-090506.png


Screenshot_20220410-085948.png
 
Inawezekana wale wanaopokea kimya Cha chini ndo wameongezewa izo asilimia ila kadri unavyopanda juu asilimia zinapungua
Lakini pesa yake inayongezeka ni kubwa kuliko Ile ilioongezeka kwenye kima Cha chini.
 
Ukikuta deni la nchi $42.1 billion na tumewekwa as moderate risks kwa zaidi ya miaka 10.

Ukalishusha deni ndani ya miaka mitatu mpaka $37.4 billion kupewa hadhi ya low risk.

Katika muda wako ukakopa labda $5 billion na ukalipa $5 billion na mpaka unafariki deni la nchi lipo $37.4 billion; maana yake ume maintain the level of debt.

Ni rahisi sana kuwaambia watu, jamaa alikuwa anakopa sana lakini awakwambii katika alichokopa alilipa kiasi gani ndani ya muda wake.

Kwenye uongozi wa Magufuli deni la taifa lilikuwa stable baada ya kulishusha na kuitoa nchi from moderate risk to low risk.

Mwaka mmoja wa maza tumerudi tena kwenye moderate sasa hayo maamuzi yakupanda au kushushwa yanaenda sambamba na dept payments to revenue collection ata wakiongopa makusanyo yameshuka, halafu bado wanajiongeza admin costs.

The nonsense is beyond hivi vitu huwa vinakuja kuumiza mbeleni uwezi vificha vikianza kuuma tupo hapa.
Unaporopoka uwe unaweka na namba.

Makusanyo yameshika kutoka ngapi na kuwa ngapi maana Takwimu za serikali ni kwamba makusanyo yameongezeka sio tuu ya TRA bali hata ya vyanzo vingine..

Ujue chuki zinawasumbua Sana,mimi nakupa Takwimu na wewe nipe za kwako 👇

Screenshot_20220406-164902.png


Screenshot_20220406-164933.png


Screenshot_20220406-163449.png
 
Wewe hujui kitu, tulia ! Hata maana ya bilioni huijui!
Angalia kupunguza Tshs.29 tu ya bei ya Lita Moja ya petroli ambapo zitahitajika Tshs.bilioni 100 imebidi Serikali kuomba mkopo WB.
Sasa itakuja kuwa 250 bilioni kila mwezi!!!
Nasisitiza HUJUI KITU, TULIA!
Serikali haijaomba mkopo specifically kwa ajili ya kulipia mafuta bali ni kujiandaa na budget deficit in case itatokea kwa hiyo wewe ndio hujui kitu.
 
Mkuu 'Fumadilu Kalimanzila', huo mstari huo ndio unaotuua kabisa Tanzania.

"...watu wenye maarifa na taasisi imara."

Binafsi, naamini kwa dhati ya moyo wangu wote, kwamba "watu wenye maarifa" wapo, labda kama unayo maana nyingine ya watu hawa. Kinachokosekana ni uongozi wenye uwezo wa kuwapanga vizuri watu hawa wayartumie vizuri maarifa yao kwa faida yao na nchi yao.

Nitakupa mfano: leo hii tunalilia wawekezaji waje kutoka Malaysia waje hapa kuwekeza ili tupate mafuta ya kula (mawese?). Tunawakimbilia hawa Malaysia kwa sababu wao walikuja kuchukua mbegu hapa za michikichi, wakaenda kwao na kutumia maarifa yao na kuwa wazalishaji wazuri wa zao hilo. Hawa hawakwenda kutembea duniani kutafuta watu waende kuwafanyia walichoweza kufanya wao wenyewe.

Huu ni mfano mmoja tu tena rahisi sana kuuelewa; lakini ni mmoja kati ya mengi ambayo sisi tunashindwa kuyafanya kwa maarifa yaliyopo hapahapa, lakini tunasubiri kwenda kutafuta maarifa huko nje. Hii ni kukosa uongozi wa kusimamia vyema kuwaongoza wananchi wafanye kazi zao kwa maarifa waliyonayo kwa ufanisi.

Nisikuchoshe, lakini yapo mengi yanayoumiza roho kuona jinsi nchi yetu hii inavyozidi kudidimia.
Ndio wameshaendelea na ni sahihi kujifunza kwao
 
Hili la Mwigulu umesema kweli. Mwigulu Ni empty head, chokoraa la singida. Sina ukabila au kidharau Kabila fulani, lakini singida hakuna mtu wa weledi wa level hiyo kushika nafasi nyeti Kama hiyo. Exception Ni Lisu Basi!
Shika hili,so far hakuna Waziri wa Fedha amefanikiwa kama Mwigulu..
 
Back
Top Bottom