Tanzania haitambui ushindi wa Mugabe - Membe

Tanzania haitambui ushindi wa Mugabe - Membe

Jokaa Kuu, uwezekano wa kumove forward bila Tsvangirai ni mdogo, maana jamaa ndo kapigana mpaka last nail wakati wapambe wa Mugabe wakimuona kibaraka. Ukweli ni kwamba Mugabe na supporters wake wameishiwa hoja. na effectively wameona kumlink Tsvangirai na wazungu ndo ONLY means ya kumdscredit! A link to a western powers is the only winning card! Hatuwezi kuishi kwenye politics of fear za miaka ya nyuma. Nani kasema Tsvangirai anarudisha wazungu au Mashamba? JAMAA ANASEMA POLICY YAKE NI FAIR DISTRIBUTION OF LAND. PERIOD.Jamaa anaweza kuwa na matatizo yake. Fine, sasa kwa nini usiwaache wananchi waamue? au unataka waamue wewe unavyotaka tuu na si wao?

Who is AU? It needs couragious people like Membe ionekane ina relevance..otherwise..itaendelea kuwa moribund na irrelevant as it has been. By the way no body takes serious AU so is the UN....consensus ya mataifa haipatikani hivi hivi..kuna wale watakaopinga tuu! hata kama utawapa nini! Ndo maana Bush au Clinton walilijua hili..wanaamua kuiruka UN...wanafanya wanalolitaka as long as hawamtegemei mtu..harafu huko UN mtabaki mnalia na international law!

Waafrika hatuwezi kuendelea kulalama kwa kutumia historia. Ni kweli tumenyanyasika na kuonewa, lakini huwezi kuua watu wako ukasingizia western countries. NO way. Kwa hiyo hata Darfur, Comoro, Congo tuache kwa sababu hata kwetu yanafanyika?

Hivi unaweza kuniambia kwamba kwa sababu babu yangu hakusoma, kwa hiyo hana haki ya kunichapa makofi au kunihimiza niende shule? au kwa vile hakusoma hajui umuhimu wa elimu?

FMES, yes Zenji tulilikoroga, lakini hebu nikuulize..daktari anayechukua "malaya" pale kilitime..ukienda ofisini kwake asubuhi akakwambia kwamba kuchukua malaya ni hatari unaweza pata ngoma au magonjwa mengine, utakataa ushauri wake kwa sababu ulimuona na yeye anachukua mzigo pale Kilitime?

International politics haziendi hivyo. Leo Bush akikemea Human Rights violations Darfur, siyo kwamba yanayotendeka Guantanamo hayaoni! Leo Australia akikemea yanayotokea Congo siyo kwamba yanayotokea kwa aboriginals hayaoni....

Ukweli ni kwamba kama international diplomacy ingekuwa inaendeshwa hivyo kama injili ya YESU (asiye na doa na awe wa kwanza kurusha jiwe)..basi hii dunia ingekuwa kitu kingine kabisa.
 
..AU wamemtambua Mugabe. statement yao inaelekeza hivyo.

..so far nimeona Tanzania na Botswana kutoa statements kwamba hawamtambui Mugabe.

..tamko la Membe ni moja ya hatua za kuvunja uhusiano wa kibalozi na Mugabe.

..nitashangaa sana kama Balozi wetu ataendelea kuwepo Harare.

..hatuwezi kukubaliana kuhusu nani yuko responsible na, au chanzo cha, matatizo ya Zimbabwe.

..kwa kweli sijui mgogoro huu unaelekea wapi na utatatuliwa vipi. time is running fast.


Statement ya AU iko wapi? Nitashangaa sana kama AU wamemtambua Mugabe halafu Tanzania ambaye ndiye mwenyekiti wasimtambue!! Hiyo maanake itakuwa kwamba uenyekiti wetu hauna maana kabisa maana hatuwezi kabisa ku-influence mambo. Please post the AU statement here.
 
AU Summit Resolution On Zimbabwe


African Union (Addis Ababa)

Posted to the web 2 July 2008

Sharm El Sheikh, Egypt

The African Union Assembly, meeting in its 11th Ordinary Session held on June 30 to July 1, 2008 in Sharm El Sheikh, Egypt,

DEEPLY CONCERNED with the prevailing situation in Zimbabwe;


DEEPLY CONCERNED with the negative reports of SADC, the African Union and the Pan-African Parliament observers on the Zimbabwean Presidential run-off election held on June 27, 2008;

DEEPLY CONCERNED about the violence and the loss of life that has occurred in Zimbabwe.

CONSIDERING the urgent need to prevent further worsening of the situation and with a view to avoid spread of conflict with the consequential negative impact on the country and the sub-region;

FURTHER CONSIDERING the need to create an environment conducive for democracy, as well as the development of the people of Zimbabwe;

EXPRESSING its appreciation to SADC, and its Organ on Politics, Defence and Security Co-operation, as well as the Facilitator of the intra-Zimbabwe dialogue, His Excellency Thabo Mbeki, President of the Republic of South Africa, and His Excellency Jean Ping, Chairperson of the African Union Commission for the ongoing work aimed at reconciling the political parties;

RECOGNISING the complexity of the situation in Zimbabwe;

NOTING the willingness of the political leaders of Zimbabwe to enter into negotiations to establish a Government of National Unity;

NOTING FURTHER the preparatory discussions on this matter had already started, under SADC facilitation;

Hereby decide:

1. TO ENCOURAGE President Robert Mugabe and the leader of the MDC Party Mr Morgan Tsvangirai to honour their commitment to initiate dialogue with a view to promoting peace, stability, democracy and the reconciliation of the Zimbabwean people;

2. TO SUPPORT the call, for the creation of a Government of National Unity;


3. TO SUPPORT the SADC Facilitation, and to recommend that SADC mediation efforts should be continued in order to resolve the problems they are facing. In this regard SADC should establish a mechanism on the ground in order to seize the momentum for a negotiated solution;

4. TO APPEAL to states and all parties concerned to refrain from any action that may negatively impact on the climate of dialogue;

5. In the spirit of all SADC initiatives, the AU remains convinced that the people of Zimbabwe will be able to resolve their differences and work together once again as one Nation, provided they receive undivided support from SADC, the AU and the world at large.


Kitila Mkumbo,

..labda nimekwenda mbali kidogo kwa kusema AU "wamemtambua" Mugabe.

..lakini sielewi kitendo chao cha kumu-address kama President Mugabe kina maana gani.

..halafu kama hatutambui uchaguzi uliofanyika na 'ushindi' wa Mugabe, je Zimbabwe ni nchi isiyokuwa na serikali sasa hivi?

..kwa wale wanaotambua 'ushindi' wa Tsivangarai wanafanya hivyo kwa kufuata katiba gani?
 
Mugabe usikubali mpaka wananchi waulizwe kwanza kama wanataka serikali ya umoja wa Kitaifa au hawataki.
 
FMES, yes Zenji tulilikoroga, lakini hebu nikuulize..
International politics haziendi hivyo. Leo Bush akikemea Human Rights violations Darfur, siyo kwamba yanayotendeka Guantanamo hayaoni! Leo Australia akikemea yanayotokea Congo siyo kwamba yanayotokea kwa aboriginals hayaoni....Ukweli ni kwamba kama international diplomacy ingekuwa inaendeshwa hivyo kama injili ya YESU (asiye na doa na awe wa kwanza kurusha jiwe)..basi hii dunia ingekuwa kitu kingine kabisa.

Mkuu Masanja,

Wewe ninajua kuwa ni kichwa sana, lakini jaribu basi kuniheshimu kidogo kwa sababu haya uliyosema hapo juu ni an insult kwa my intelligence.

kwa sababu hayana ushusiano wowote na wizi wetu wa kura na uchaguzi, na kujaribu kwasomesha wengine wasiibe kura na uchaguzi kama sisi.

Ahsante Mkuu
 
Hivi kina Membe kumtaka Mugabe ashirikishe upinzani hawaoni kwamba ni jambo kubwa sana ambalo linahitaji kura ya maoni kwanza?
 
Membe and company, kwanza siamini kama Tanzania tumetoa hilo tamko, lakini kama ni kweli basi inabidi wafahamu, michezo yao itakuwa mauti yetu na wajukuu zetu.
 
Kitu ninachoshindwa kukielewa ni kwanini matamko makubwa kama haya anaachiwa kuyatoa waziri? Kwa nini Rais asitoe matamshi haya yeye mwenyewe?
 
unajua imani ni kitu kimoja kizuri sana kwetu sisi wanadamu..........na hizi imani inategemea mtu unazielewa vipi ili kuijenga imani yako vilivyo, imani hizo hizo wengine huzitumia kufanya maovu na wengine hutumia busara ili kujudge na kutenda yaliyo mema.

.........ni imani yangu kuwa whatever the case may be the fact will remain to be the fact....na asiye liona hilo.......eti kwa kuwa ana boriti....im sorry.......siwezi kumsaidia........endelea kuwa na boriti milele......

Binafsi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo wa kuona japo facts kidogo na hizo ndizo ninazo na nitakazosimamia.......unless proven otherwise

Kuamini au kutokuamni kwako hakuifanyi/hakumfanyi.......Serikali/Membe kutosema yaliyosemwa............na kama kutokuamini kwako kunakufanya uone its a big joke....so be it...thats you,...........kuna wengine wameona/tumeona otherwise....and that is the fact.

Narudia tena, kama hili jambo limesemwa na Membe and for that matter serikali yetu.......NAWAPA PONGEZI
 
Kitu ninachoshindwa kukielewa ni kwanini matamko makubwa kama haya anaachiwa kuyatoa waziri? Kwa nini Rais asitoe matamshi haya yeye mwenyewe?

..mbona dr rice naye hutoa matamko makubwa na si bush pekee.

..hiyo ni misimamo ya sera au mahusiano ya kimataifa. anahusika kusema.
 
..mbona dr rice naye hutoa matamko makubwa na si bush pekee.

..hiyo ni misimamo ya sera au mahusiano ya kimataifa. anahusika kusema.


Huwezi kufananisha muundo na utendaji wa serikali ya Marekani na Tanzania.
Kiprotokali matamshi ya kumpongeza au kutokumtambua Rais huwa yanatolewa na Rais mwenyewe. Kutolewa na waziri ni ishara tosha kuwa serikali inatoa matamshi haya kwa shingo upande.
 
Viongozi waliokuwa Misiri walipomuona MUGABE amefika kule wangemkatalia kuhuthuria kikao hawamtabui
kulekukubali kuka kwenye kikao wamemkubali kuwa ni raisi wa Zimbabwe
halafu huku wanakuja na hoja tofauti NI UNAFIKI
 
Duh! Tanzania tuna ubavu wa kutoitambua serikali iliyochaguliwa Zimbabwe, lakini tunawatambua watawala wa Zanzibar?

Yaani kweli tunayo hiyo moral authority ya kutotambua wengine? Halafu humu JF kuna wanaounga mkono haya? Mbona makubwa sana haya wakuu, ni kweli hatupendi sana yanayoendelea huko Zimbabwe, lakini sisi Tanzania tukae kimyaa kwanza tuachie wengine kama Botswana, Malwi au Zambia, maana ndio wenye ubavu na authority ya kusema haya, sisi tunyamaze tu as a nation.

Hatupendi huu unafiki wa hali ya juu sana tena ni aibuuu!kuanzia taifa letu mpaka sisi wote wananchi, Membe afute hiyo kauli mara moja!

Mkuu Zanzibar ni Tanzania na matatizo yaliyotokea naona unayakubali kama unavyoyakubali ya Zimbabwe( kutokana na nukuu yako) Sasa ilikuwa ni wajibu wa Nchi nyingine za SADC kuisimikia Tanzania. Kwa hiyo mkuu unataka pia kusema kuwa kutokana na matatizo ya Zanzibar, Tanzania kwa sasa hakuna serikali? Kama serikali ipo then wanawajibu wakutoa tamko kuhusu Zimbabwe hata kama wao hawakutolewa tamko kwa uchaguzi wa Zanzibar.
 
Kutokuona kundule lako haisababishi lamwenzako liwe zuri, kama kweli ni baya sawa na lako.

...absolutely.........kwi kwi kwi kwi kwi..........tena ukiliona la mwenzio ni baya, la kwako likalie kweli kweli ili wasije wakaliona wengine..........kwi kwi kwi kwi kwi
 
Nyangumi,
Nafikiri huyafahamu ya huko kusini ndio maana unasema kuwa wa Zimbabwe walioko SA walimkimbia Mugabe. Sijui na wa TZ, waMozambique, Nigeria, Kenya n.k. walioko huko wote pia wamekimbia maraisi wao?

Uchaguzi Zimbabwe umekuwa wa mtu mmoja kwa vile Tsvangirai aliamua kujitoa dakika ya 90 kinyume na sheria maana pengine alihisi kushindwa, who knows. Awamu ya kwanza matokeo yalikuwa 47% MDC, 42% Mugabe, niambie hata kama ni wewe tena baada ya kukimbilia SA utakuwa na uhakika kweli wa kushind re-run?

Ni kweli vurugu zilikuwepo hapa na pale na waliokumbwa nazo hata elfu hawafiki, hii ni kwa taarifa ya MDC. Wewe umeng'ang'ania na picha za propaganda za kwenye net, mbona hazikuonyeshwa kwa maelfu kama ilivyokuwa vurugu za SA, au kuonyeshwa video, zaidi ya ile ya wale vijana wanaokimbizana waliovaa vilemba vya ZANU-PF??

Swali kwenye free election ni kuwa je watu walishindwa kupiga kura ingawa walitaka kufanya hivyo? Ukweli ni kuwa hata baada ya Morgan Tsvangirai kuwataka watu wakae nyumbani, bado wengi walijitokeza kwenda kumpigia Tsvangirai kura au kuziharibu. Hii inaonyesha dhahiri kuwa access ya kupiga kura ilikuwapo na ndio maana nasema uchaguzi ulikuwa FREE, lakini kuwa FAIR kunaweza kuwa discussed kutokana na vurugu za awali.

Tuachane na kudance hizi ngoma tunazopigiwa kwa vile sauti zao ni kubwa. Mambo Zim ni kweli hayaendi sawia, lakini tusijiunge tu na kwaya hii inayotuambia kuwa sababu tu ni Mugabe, kwa vile wao wana vita naye basi na sisi tujiingize. Historia itatuadhibu kama hatuisomi ipasavyo hivi sasa. Zidumu fikira za Mwalimu.

Huwa situmii muda wangu kubishana na mtu namna yako kwa kuwa fact zipo ila unataka kupindisha, ukweli. hakuna asiyejua raia waliokwenda kuishi huko, ila kuna waliokimbiloia huko kipindi cha uchaguzi.
 
Unajua ni wajibu wa kila mwanadamu kuona na kusema aonavyo, hiyo ni haki kwa kila mwananchi, lakini tatizo ni ukweli ulipo na huonyehswa kwa hoja tu,

Ninarudia hivi Tanzania, hatuna moral authority ya kuu-question uchaguzi wa Zimbabwe, kwa sababu uchaguzi wetu wa Zanzibar ulikuwa ni sawa kabisa na ule wa Zimbabwe, no wonder Mugabe anaonekana kutojali kwa sababu anajua kuwa karibu viongozi wengi wa Afrika wanaompigia kelele hawana hiyo moral authority na wale walionayo kama Malawi, wamenyamaza kimyaa,

Unafiki mtupu na ndio maana hata huko nje hakuna anayeujali, yaani wewe umeiba uchaguzi halafu tena una nguvu ya kumwambia mwingine aliyeiba uchaguzi kama wewe kuwa humtambui, jamani kweli siasa zimegeuza ukweli kiasi hiki?

Kwanza tutoe boriti machoni kwetu, ndio tutakuwa na sauti ya kuoa maboriti kwenye macho ya wengine, hii ni fact na ni ukweli ambao hauwezi kubadilishwa na maneno mengi ya kuokota kwenye dictionary na kujaribu kufikiria kwa masaa mengi, hapana ukweli ni ukweli na siasa bado ziko pale pale, Tanzania hatujui maana ya uchaguzi wa haki sasa hatuwezi kuwa waalimu wa wengine maana tutawaponza na kuishia kuwa kama sisi,

no wonder hawatusikilizi kabisaa kama walivyokuwa wakitusikiliza zamani!.
 
Hivi kwa nini kila kitu tunakihusisha na wazungu???? Mugabe is just a waste and Membe said so, jamani does it need Sky News or CNN kutwambia madudu na madhambi ya Mugabe? sisi hatuyaoni? sasa kwa nini akitokea Muafrika akayasemea..tumuone kibaraka?? Na bado tunasema Africa tusolve matatizo yetu? Ok, TZ na sisi tuna yakwetu, so is Kenya, so is Sudan..and on and on..lakini we need to start from somwhere...(kwa vile wewe hukwenda Universiti..utakataa kumpeleka mtoto wako..just because wewe hukusoma? Hapana kwa hili Membe na JK wako RIGHT kabisa! ..asingesema wengine tungeendelea kumlaumu..kasema ndo hivyo tena anaambiwa kibaraka! na hiyo ndo demokrasia..

Membe for the first time, you made me proud of you! We live in an imperfect world though, but you have shown the way... Ila atleast you are on record! Go Benard! Iam really happy atleast...My dear friends..hata mtoto akizaliwa haanzi kutembea siku hiyo hiyo..we have to start from somewhere..

Thanks Benard Camillius Membe!

You have made my day, Mkuu sina la kuongeza.
 
Back
Top Bottom