Demokrasia si tu uchaguzi, bali ni mfumo unaohakikisha uwajibikaji, usawa, haki za binadamu, na uhuru wa kujieleza — mambo ambayo ni msingi wa maendeleo ya kweli na endelevu. Kukiwa na demokrasia, wananchi wana nafasi ya kuwawajibisha viongozi, kushiriki katika maamuzi, na kulinda haki zao — hali inayochochea maendeleo jumuishi.
Hii ni dichotomy (mgawanyiko wa bandia). Haipaswi kuwa maendeleo badala ya demokrasia, bali maendeleo kupitia demokrasia
Wewe umekuwa brain-washed na CCM ili wapate kukutawala vizuri na watanzania wenye mawazo kama yako wako wengi kweli.Wananchi wanahitaji maendeleo na demokrasia. Hili si suala la kuchagua moja. Maendeleo yanapaswa kuja kwa njia inayowahusisha watu, siyo kwa kuwafumba midomo. Hivyo, kauli hiyo inapuuzia umuhimu wa uwajibikaji wa kidemokrasia na inaweza kutumiwa vibaya kuhalalisha utawala wa mabavu.