Tanzania hatupo salama, Maadui wamepenya hadi Ikulu

Tanzania hatupo salama, Maadui wamepenya hadi Ikulu

Hata mimi nimeshangaa sana kuona taarifa nyeti kama hizo ambazo zinamhusu Mkuu wa Nchi zinazagaa mitaani?
Bila shaka kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi ili kuona ni nani anahusika zaidi na utoaji wa siri.
Hapo inahitaji akili sana kubaini watu wanaovujisha siri.
Tunaweza tukadhani tumefichama kumbe tupo eneo la wazi kabisa kiasi kwamba kila mtu anatuona. Hii ni hatari sana.
Mwisho, Namshukuru Mungu mwenye nguvu kwa kutuletea CHUMA, SHUJAA, MSHINDI, MZALENDO WA AFRIKA, JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
Ametufundisha mengi, mengi, mengi sana. Kwa pamoja tukiyafuata na kuyaishi kwa vitendo, tutashinda.
JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, uliombee Taifa hili liweze kushinda mitihani yote. Amina.
 
Mkuu kwa mfano kuna yale magari ya jeshi ambayo hutumika kwenye sherehe za uhuru au kuapishwa kwa marais au kubeba miili ya marais waliofariki... hayo magari yalionekana tangu jumanne wiki hii inayoisha yakitoka lugalo jeshini kuelekea mjini sasa wenye akili walipoyaona hayo magari wakaunga dots kwamba kuna jambo kwa sababu yale magari huwa hayaonekanagi hovyo tu mitaani.....
Kama hili lilitokea basi ni dhahiri kwamba wale watu wanaodai kupata taarifa kutoka ndani(serikalini) walizitengeneza tu baada ya kudokezwa kwamba hayo magari yameonekana mtaani.

Nipo hapa kujifunza.....nielimisheni.
 
Ndo jua sasa wale jamaa na misuti yao myeusi na miwani na microphone kumbe hamna kitu .TISS inatakiwa kuundwa upya na sio kuokota okota tuu.
Fikiria Kama ole 7 baya n TISS unategemea nn huko ndan mkuu

Sifa ya TISS kuwa kada wa chama tawala imetosha elimu utaijua hukohuko mkuu nan atashindwa kuvaa miwan nyeusi na kaunda suti kwa Sasa hvyo n vigezo
 
Hakika,hii ni taasisi nyeti sana,inahitaji watu makini.Zamani hawa jamaa tulikuwa tunaishi nao mitaani miaka kumi lakin huwezi jua ni mtu wa TIS,lakin hawa wa siku hizi aaah tunawajua kabisa na ndio wanaotoa taarifa za ndani za Serikali. Kwa vyovyote vile ukiona taarifa za ndani za ikulu zinasambaa ujue hatuko salama.
Mzazi alikuwa hawezi kujua kazi ya mwanaye, ndugu wengine na majirani ndiyo kabisaa.
Lakini leo hii wanatamani wajulikane hata kwa wasiotaka kuwajua.
Imefika hatua hata wajinga tu kwa kutumia mwamvuli wa ukada na walioaminiwa wanajiona nao ni watu wa vitengo.

Shida sana hii.
 
Tecnojia ndio inafanya mambo yavuje haraka, zamani mambo mengi yalikuwa kwenye makaratasi.

TISS walizuia kabisa watu kupiga picha mwili wa Magufuli lakini leo kuna video inasambaa ikionyesha mwili wa Magufuli ukiwa kwenye jeneza.

Jamaa inaonekana alivaa kamera kwenye miwani ,kofia ama koti.

Tecnolojia imekuwa juu Sana Hadi USA wanalia Kila siku kudukuliwa na Uruss.
Marekani kudukuliwa na Urusi sawa
Sasa hawa Tiss pale taifa wamezidiwa kete na akina Shomari wa tTemeke Mikoroshini
 
Alafu kuna wajinga wanasema jpm alikuwa analidwa na wanyarwanda mimi nakataa
FB_IMG_16162636744547528.jpg


Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
..TISS pia walivujisha video ya mazungumzo ya Tundu Lissu alipotembelewa na Mama Samia Nairobi Hospital.

..Usisahau waliodukua mazungumzo ya kina Nape Nnauye, January Makamba, Bernard Membe, na Abdulrahman Kinana.

..Sasa jiulize aliyekuwa aki-direct mambo hayo ya hovyo ni nani?
Mmmh!
 
Back
Top Bottom