Tanzania hatupo salama, Maadui wamepenya hadi Ikulu

Hii inanifanya niamini sasa hata taarifa za kuugua na kifo cha Magufuli huenda Lissu alipewa na wasaidizi wa mama Samia?
..Utakuwa umekosea.

..Waliovujisha clip ya Mama Samia na Lissu akiwa Nairobi Hospital walifanya vile kwa nia mbaya.

..Wale hawakutumwa na Mama Samia, na vilevile hawakuwa na ridhaa ya Lissu.

..Lile lilikuwa tukio la baya na la kihuni kufanywa na watendaji wa Ikulu na naamini lilimuumiza hata Mama Samia.
 
Mataga bana,shujaa wa Africa.Lol
 
Clip hiyo ilihusu nn Mkuu? Ikikupendeza naomba unijuze,nilipitwa.
 
Clip hiyo ilihusu nn Mkuu? Ikikupendeza naomba unijuze,nilipitwa.
..Mama Samia alikuwa amekwenda Nairobi kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi Uhuru Kenyatta.

..Baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa alimtembelea Tundu Lissu aliyekuwa amelazwa Nairobi Hospital.

..Sasa Mama Samia alipokuwa akizungumza na Tundu Lissu na mkewe wako watu wa Ikulu ambao waliwapiga picha na kurekodi mazungumzo yao.

..Baada ya Mama kurudi Tanzania ikarushwa clip fupi sana yenye headline " Tundu Lissu amshukuru Raisi Magufuli. "

..Lissu alimshukuru Raisi kwasababu Mama Samia alisema ametumwa kwenda Nairobi Hospital na Raisi.

..Ukweli ni kwamba Lissu na Mama Samia walizungumza mambo mengine, na Lissu alisisitiza kuhusu stahiki zake alizokuwa amenyimwa na Bunge.

..Baada ya hapo, ikabidi Lissu afanye interview na vyombo vya habari ku-clear upotoshaji wa video clip iliyotumwa na watu wa Ikulu.

NB:

..Mama Samia angeondoka Nairobi bila kumtembelea Lissu hospitali serikali ya Tanzania ingekuwa imejichafua kidiplomasia.

..Pia Raisi Magufuli alikwepa kwenda Nairobi kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi Uhuru Kenyatta ili kukwepa kulazimika kwenda kumsabahi Tundu Lissu aliyekuwa amelazwa hospitali.
 
TISS siku hizi wanatambukishwa majukwaa ya siasa .ni Nina Sana
 
Leo nilipokuwa uwanjani kumuaga hayati Mhe. Dk. J.P.M kuna msista alikuwa kakaa mbele yangu sasa akawa anachati na kiswaswadu chake namba kaisevu Mr. ...

Sasa Kila kitu kinachoendelea mule uwanjani yule msista anamuuliza huyo jamaa..mfano Helicopter ikawa inazunguka uwanja akamuuliza inafanya nini? yule Mr. ... anafu guka anaelezea kila kitu cha kiusalama, yule dada anamuuliza jamaa.

SASA Nikaprove huyo Mr ni usalama maana kuna sms alimtumia msista analalamika "Dah dear nimechoka ila inabidi niondoke kesho maana jina langu limetoka kwa wanaoenda kuhakikisha usalama chato"

Keep in mind huyu msista alikuwa anachati anajiona anaficha simu wakati mimi Reddington niko ngazi tatu juu yake.

Funzo: Usalama wa siku hizi watoto, hawajaiva.
 
Mmmmhhh!
 
acha kutupotosha mh. ni TISS ambayo unamaana ya TANZANIA INTELLIGENCE and SECURITY SERVICE

siku nyingine kua making kabla ujakosoa maana utakosololewa wewe mwenyewe tena vibaya mno
Sasa kwani Mimi nimeàndikaje KADA?
 
Tulionya kwamba wale UVCCM duni mnaowajaza TISS iko siku watawafanyizia lakini mkatupuuza , nadhani sasa mmeanza kutuelewa

Mngekua na Nia njema kwa nchi na wananchi basi hata taarifa zao (wale waliovujisha kuwaletea through Lissu) mngewakatalia na kuwataja hadharani!

When you use the weakness of your opponent/rival as a weapon against them, you are no more or less low than them!
 
Mtanzania wa kweli na mwenye uchungu na Tz hawezi kumkumbuka huyu mtu;
Mauaji,
Utekaji,
Ajira za upendeleo wa kichama,kiukanda,n.k,
Kuhamishia mali za nchi Chato,
Kuminya Uhuru wa vyombo vya habari,
Udikteta kwa vyama vya upinzani,




Acheni unafiki.
Mnajua maana ya "mtanzania wa kweli na mwenye uchungu na Tz"?
 
Mungu awajaalie Vigogo 14 woote kwa unyetishaji wao uliotukuka

Unfortunately katika hili la hayati na yote yanayomuhusu kuanzia maradhi mpaka kifo hawafiki wala kunusa 10! Hao 14 it’s a dream!

Kibaya zaidi it’s easy to identify all those that were there during admissions at JK insititute and later Mzena!

Tujipe muda na akiba ya kauli, tutayashuhudia!
 
Hii ni kweli hiyo video nimeiona nikajiuliza huyu mtu aliwezaje ku record video ya rais akiwa kwenye jeneza? Nikawaza au aliweka simu kwenye mfuko wa shatiakageuza camera ikarecord?
Nikakumbuka movie moja ya kokorea video inarecodiwa kupitia miwani miwani dah.
 
Hata wazazi wanaanza kumtangaza mtoto wao kabla ya hata taratibu za ajira kukamilika
 
Sorry, kama hutojali naomba unirushie Pm au hata unitumie link pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kuwa salama kwenye jambo lolote wekeza kwenye mambo makuu mawili tu, toa haki na wekeza kwenye akili.
CCM ilijitahidi kuwekeza kwenye maneno badala ya akili, wamewapa majukumu makubwa vijana wao wenye akili ndogo na kuzichukia akili kubwa madhara yake ndio hayo. Pia kitendo cha kuminya haki na uhuru matokeo yake ni usaliti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…