Kama Taifa hebu tutafakari haya,
1. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayeongeza kwa mkupuo wanafunzi wapya elfu 29 kwenye HESLB simnakumbuka mtangulizi wake yeye ilimchukua miaka mitano kufikisha wanafunzi wapya 32,
2. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekusanya kodi kwa wastani wa TZS 17.2Trilioni kwa mwezi bila ya kukimbiza wafanyabiashara wala kuwadhulumu chochote,
3. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine anayewahurumia na kuwarejesha shuleni watoto wa masikini waliopata mimba wakiwa shuleni kwa kurubuniwa kwa chips na bodaboda,
4. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayekuza uwekezaji wa nje FDIs mara sita zaidi kwa miezi sita tu yaani kutoka $510M hadi $3BL ,
5. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine kwa miezi saba tu ataongeza hifadhi yetu ya fedha za kigeni kwa TZS 4.4Trilion yaani kutoka $4.8BL mwezi March hadi $6.7BL mwezi September 2021,
6. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua ambulance 395 na magari 214 kwaajili ya chanjo wakati mtangulizi wake kwa miaka mitano alinunua ambulance 117 tu bila magari ya chanjo,
7. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayenunua CT SCAN kila mkoa mtakumbuka tangu uhuru zilikuwepo CT SCAN mbili tu bara na visiwani,
8. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetununulia MRI kwenye kila hospitali ya kanda nchi nzima sina historia kama tulikuwa na MRI yeyote kabla ya hizi mpya za mama Samia,
9. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakaye nunua "Water drilling holes machines " 25 toka mashine moja ya Halmashauri ya Tarime tuliyokuwa nayo,Rais anakwenda kumaliza shida ya maji kwa vitendo,
10. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayetujengea madarasa elfu 15 ya sekondari na mengine elfu 3 ya shule shikizi, Sawa na wastani wa kila shule moja ya sekondari ya serikali madarasa mapya manne ( 4 )
11. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayewapanga wamachinga wetu kwenye Permanent Premises ili watambulike na kupewa mikopo na huduma zingine za kibiashara kama Semina na mafunzo kirahisi badala ya kuwatumia kama mtaji wa kisiasa na kuwaacha wakiogelea kwenye umasikini mwaka wa Uchaguzi hata mwaka wa Uchaguzi,
12. Nilini tena baada ya huyu tutampata Samia mwingine atakayefuta wasiojulikana na walevi wa madaraka na kuwafanya watu waishi kwa Uhuru na kujiamini ndani ya nchi yao na kulifungua Taifa kimataifa,
Nitaendelea na tafakuri yangu
View attachment 2023684