Tanzania ili tuendelee tujiunge na Marekani

Tanzania ili tuendelee tujiunge na Marekani

Mbaka Sasa china na urusi ndio waneiboost Africa huyo marekani huwezi hata kufanya nae biashara kabla ya uchina kukua tumeishi maisha duni mno Mfano mchina anatuuzia vitu Kwa bei nafuuu mno vinatusaidia sana kwenye biashara viwanda kilimo. We angalia Mfano nimeshuhudia watu wakichana mbao Kwa msumeno wa mkono lakini mchina kaleta amec Sasa watu wanachana mbao nyingi sana Kwa hiVyo uzalishaji unakua. hata kwenye madini wabongo nao wanaweza kufungua migodi Kwa sababu mchina ana vifaa vya bei nafuu
 
Ningekuwa na muda ningeandika paragraph ndefu sio kupinga bali kuonyesha uhalisia ambao wenyewe ni kipingamizi tosha.

Mkuu hivi unajua/umeona jinsi gani Black Americans wanavyoishi kwa tabu Marekani?
Ndio wana uhakika wa kula na kulala vizuri, miondombinu mizuri na wapo kwenye taifa lenye nguvu duniani, kwa wale wenye status kubwa basi usalama wa uhakika vilevile.
Lakini wanakosa kitu kimoja ambacho ndio kinadefine binadamu na kuleta amani ya ndani ambayo ndio ya msingi kuliko usalama na amani ya nje. Thamani ya Utu.
Ndio, Utu. Binadamu asiyethaminiwa utu wake waziwazi ni anaishi kwa tabu zaidi ya mnyama zaidi ya hapo kuna Ukandamizaji kifursa, Ubaguzi wa rangi, Police-brutality, Genocide n'k...
Kama hayo yote yanafanyika kwa waliozaliwa hukohuko unadhani itakuaje kwa mtu aliyetoka nje kabisa?

Na sio hapo tu, bali umeona ni jinsi gani Caucasians wanavyodispise na kudharau Waafrika? Hapo haujafika kwao sasa unadhani itakuaje ukienda kwao?
Kama hata hao weusi waliozaliwa huko wanawafanyia yote hayo. Je unadhani watakubali kuona Taifa lao linaungana na nchi wanayoiita third world country? Tena iliyojaa watu weusi?
Hiyo haitoshi, hata hao Black Americans wenyewe wanawadharau waafrika vilevile, Kama kwa idadi yao ndogo na wanakosa vingi, je unafikiri watakubali kuona wengine kama wao tena million 60 waongezeke kwenye nchi yao?
Bado haitoshi, watafuja rasilimali zetu zote ambazo hata wenyewe million 60 hazitutoshi na kwenda kujinufaisha wao million 300, rasilimali ambazo sasa hivi wanangaika kila namna kuzipata kwa malipo ya kijiko. (Ukisikia mbuzi kafia kwa muuza bucha ndio hii)
Na hiyo bado haitoshi, hapohapo watataka kupitisha propaganda za ajabuajabu ili kucontrol population sababu rasilimali hazitoshi. Kubomoa maadili mubashara na kuharibu vizazi vyote vijavyo kwa sababu zao nyingine zisizojulikana.

Caucasians wanasema "Waafrica ni wavivu wanaopenda vya vikubwa na vya bure bila kufanya kazi, wanashindwa kuendeleza mataifa yao wanaenda kwao kutumia vyao walivyotafuta kwa kuhangaika na jasho.
Hivyo Waafrica wabaki barani kwao kila mtu abaki nchini kwake." Mimi nasema wako sahihi na hawajakosea.
Mkuu hicho ulichoandika hakiwezekani na ni ndoto.
Na kuliko kupitia yote hayo na kuishi kama mnyama na kuwa muoga kama kunguru kwa kutukanwa, kudharauliwa kubaguliwa na wamagharibi ni vizuri kubaki nyumbani kwenye amani ya kweli na kuhangaika na kuboresha nyumbani sababu nyumbani ni nyumbani tu.
Ni vizuri Tanzania iwe moja ihangaike na isimame yenyewe kama yenyewe kwa jasho lake lenyewe kama mataifa mengi makubwa duniani. Wananchi wa Tanzania waache Ujinga, Uvivu, Ukabila na Udini na wasimame kuwa kitu kimoja na kuendeleza taifa kama taifa moja. Ikiwemo kuchagua viongozi bora na kuweka mifumo imara, sababu hapa ndip kikwazo na tatizo kuu lilipo.
Na siku zote kumbuka mtafuta kwa jasho na kula jasho lake mwenyewe hueshimiwa.

Mkuu hakuna mtu mweupe anayempenda mtu mweusi. Hizo International Relations na Public Relations zisikuongepee na kukuchanyanganya mpaka kufikia kuficha na kushindwa kuona uhalisia. Moyo wa binadamu ni kichaka lakini moyo wa mzungu ni msitu.
Sijui unaongea nn ila numbers hazidanganyi isee dunia zima watu wanamiminika USA sasa km unayoyasema yapo basi si makubwa km yaliyopo kwenye nchi zetu hizi zinamatatizo zaidi kuliko huko USA.
 
Back
Top Bottom