Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta

Ùzuri wanaoumia walio wengi ni CCM hao hao, upinzani wengi wetu tuna maisha mazuri, maisha yatakapozidi kuwa mabaya tutawatanguliza mbele kwenye maandamano CCM hao hao

Kuna kweli hapa. Wafuasi wengi wa upinzani ni watu above average na maisha yao yako juu kidogo.
 
Zitto mbona kila siku mnatuambia Kagame ni dikteta na Zenawi alikuwa dikteta?
 
Leo umeongea jambo la kuwaaamsha wapinzani.

Shida wapinzani wa Tanzania wanajishughulisha na matukio na mtu mmoja mmoja badala ya mfumo.

Ni kama ile HardTalk bwana yule aliambiwa anaongelea vitu specific badala ya mfumo.

Kazi ipo hadi kuitoa CCM madarakani, huenda watakaokuja kuitoa sio hawa wa sasa, wanaweza kuwa watoto wetu wa darasa la kwanza na la pili wa shule ya msingi.
 

Umetulia, umeandika point kubwa sana. Ila kwa kuongezea ni kwamba ccm pia iwe makini. Upinzani ukifeli kwa asilimia mia ni hatari zaidi kwao kuliko kwa upinzani wenyewe. Lazima watafute kabalance flani hivi upinzani halisi uendelee kuwepo. Upinzani halisi na si upinzani tiifu kwa chama tawala.

Waafrika,wamarekani, ulaya na Waasia tupo tofauti na tuna upinzani sababu hawajatokea viumbe kutoka sayari nyingine kujaribu kutudhuru. Wakitokea utaona namna ambavyo tunaweza kukaa pamoja kama familia.

Ni hatari sana kwa ccm ya sasa tofauti na ccm ya nyerere kutokuwa na mpinzani kabisa.
 
Wewe hata toothpick una import nje sijui viberiti na hii elimu yenu ya watoto wanaofaulu la saba hawajui kusoma na kuandika
Unataka ujifananishe na Putin ?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
There you are, speech zake za mwanzo zilionyesha real patriotism, kama huyu wetu, watu wakamuamini, unajua speech ya yule padri ambayo ni quote ya watu wengi wenye ufahamu, they came for Jews I was silent for I wasn't a Jew........ They came for me no one rised a voice for me!

Hata kwako itakuwa hivyo muda si mrefu, tabia za madikteta hushabihiana hufanya mambo haraka kwa kukurupuka, maumivu yake ni baada ya kipindi kifupi tuu!

Just wait and see or otherwise tumekosea si dikteta!
 
Wacha uvivu; siyo ndefu hata kidogo. Mimi nimeisoma kwa dakika tatu tu! Labda kama hutaki kusoma maoni ya Zitto.

Kuna watu lazima post zao nizisome kwa makini sana Zitto, Lissu, Ole Mushi hata kwinyara na madada wa taifa nikimaanisha Fatuma, Maria Sarungi na MANGE KIMAMBI
 
Unaishi ili ule na uende chooni.
Hongera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lunch time na mimi ndio nimemaliza kusoma.

Zitto asante kwa ushauri laiti wangeyajua haya.............. hapo ndio unapojua akili ndogo kuongoza akili kubwa...
 
Kuwa GENIUS na kuwa DICTATOR ni vitu viwili tofauti na Unaweza kuwa GENIUS na pia ukawa na tabia za UDIKTETA at a same time!
So sijaelewa ur point mkuu ya kupinga hoja ya zitto kwa kuleta habari ya Ugenius..!
 


Haulewi unachokiandika, Hitler alifwata nazism ideology kabla hata ya kushinda Uchaguzi hata kitabu chake ,,Mein Kamp” ambacho alikiandika kabla ya kushinda Uchaguzi kilionyesha ideology yake, Kampeni yake na Chama chake ilikuwa wazi walisimamia nini na walisema wangeshinda wangefanya nini wakachaguliwa kwa kura nyingi na kufanya kama walivyoahidi na kama alivyoandika kwenye ,,mein kampf “ , hivyo Hitler hakubadilika baada ya kushinda Uchaguzi bali alitimiza aliyoyaahidi yote na wananchi walitegemea na kutaka hivyo na ndo maana walimchagua, ilikuwa kwenye campaign manifesto ya chama chake.
 
...Tofauti yao na Sisi ni kwamba Madikteta wao ni wanazuoni wenye uwezo wa kutumia akili na utulivu kufanya maamuzi...
Aisee! Aliyeelewa hapa naomba asaidie kunifafanulia
 
Wakuu wa mikoa ipi hawahojiwi ilhali juzi tu Makonda na Mnyeti mliwahoji hapo Dodoma kupitia kamati yenu?
 
Unachonifurahisha unasema sielewi huku nimekupa the most famous speech uisikilize,, kwa maelezo yako haya Hitler alikuwa dictator kabla ya kupata madaraka!
 
Unachonifurahisha unasema sielewi huku nimekupa the most famous speech uisikilize,, kwa maelezo yako haya Hitler alikuwa dictator kabla ya kupata madaraka!


Hitler alieleza yote ambayo angeyafanya kama angeshinda, aliandika kwenye Kitabu chake na hata alikampenia hiyo nazism ideology hivyo waliomchagua walitegemea aliyoyafanya kwani ndivyo alivyoahidi, mfano aliahidi akiingia atamua yule aliyesaini makubaliano ya Versailles ambaye Wajerumani walimuona kama Msaliti na kweli alivyoshinda na kukabidhiwa Dola yule msaliti aliyesaini makubaliano ya Versailles alipigwa risasi live na Serikali ya Hitler kama alivyoahidi!
 
Ubaya huu ushauri umetoka Nazareti na kwavile wapo waliokariri kuwa jambo jema haliwezi kutoka Nazareti watakupuuza .

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna ukweli mdogo ndani yake lakini yote siyo kweli. Kikwete hajawahi kuwa role model ya kiongozi bora wala Mwinyi. Wote hao wawili walikuwa viongozi dhaifu lakini waungwana, wastaarabu, wenye utu na wavumilivu. Baadhi ya mambo ya hovyo waliofanya kama kuvuruga mchakato wa katiba mpya yalitokana na huo udhaifu wao na wala siyo uovu binafsi kama binadamu. Bila shaka Kikwete sasa hapo alipo atakuwa anajutia kitendo cha kuikosesha nchi katiba ambayo leo ingeinusuru kwa baadhi ya maamuzi yanayofanyika jikoni badala ya kwenye vikao rasmi. Mkapa alikuwa kiongozi jeuri (arrogant) lakini siyo katili wala mwovu. Anao upeo mkubwa na uwelewa mkubwa wa uongozi, utawala wa sheria na uhusiano wa kimataifa. Ccm pia tuanaifahamu; tumekuwa nayo miaka yote. Ni chama chenye misingi mizuri, historia nzuri lakini uimara wake na udhaifu wake hutegemea kiongozi wake. Imeanza kuyumba awamu ya 4 kutokana na udhaifu wa kiongozi. Leo hii ipo kwa jina tu! Wako wapi siku hizi wazee wengi wa nchi hii? wamenyamaza kimya kwa sababu ccm ya sasa ni aibu na chukizo kwao. Wanasubiri muda upite waanze upya. Watu hawahangaiki na ccm kwa sababu wanajua yanayoendelea sasa siyo sera yake wala maamuzi yake. Sana sana wana-ccm nao wanaona shida ambayo kila mmoja anaiona. Baadhi ya na ahadi zake zimepigwa marufuku! Huku mtaani tuko nao; wazee wetu wa ccm siku hizi hawataki hata mazungumzo kwenye simu kwa hofu ya kudukuliwa! Mkikutana ana kwa ana wanasikitika sana; wanajuta. Wengine wana uchungu mioyoni mwao. Lakini yote haya ni mpango wa Mungu. Mungu ameamua kuonyesha watanzania kuwa kiongozi ni katiba; siyo Nyerere. Watanzania wamekuwa na kuamini kuwa kiongozi siku zote atakuwa mcha Mungu na mwungwana kama Nyerere. Kikwete na waliomshauri waliona kuliko kukubali katiba ya Warioba afadhali ya zamani! Iko wapi leo ile ya zamani?
 
Mwalimu Nyerere alitufundisha kuwa maamuzi ya wengi ni faraja hata kama yana walakini.
Na waswahili wakamalizia kuwa wengi wape.
Mh.Zitto kama anayodai hapa yatatupunguzia uhuru wa kuamua mambo yetu wenyewe,au kama yatatuondolea utu,au kama yanajenga tabaka za watawala na watawaliwa basi huo ni udikteita haukubariki.
Lakini kama ni ghiriba,ni sawa ramli chonganishi,yaani divide and rule.
 
Sawa utakula miundombinu...tafuna madaraja, hamia kwenye fly over na umalizie ndege. Utakuwa umeshiba maendeleo
 
Athene ya Ugiriki iliendelea kwasababu ya Demokrasia, hadi kufikia hatua ya kutishia nchi za kidikteta zenye nguvu kubwa za kijeshi kama Sparta: Wasparta hawakupenda Demokrasia na mifumo ya Athene na wakaamua kuivamia kwenye vita ya Peloponnesian ya Mwaka 431 BC. Unachokisahau ni kwamba waathene walienda mbali na kutengeneza mfumo wa Demokrasia wa moja kwa moja (Direct Democracy)

Roma ya kale lilikuwa ni dola la kifalme lakini kimsingi ndiyo dola ambalo tunaiga mifumo yake ya kidemokrasia katika dunia yetu ya leo. Kaisari na nguvu zake zote zile ilikuwa ni lazima atii matakwa ya Seneti ya Roma na aliposhindwa kufanya hivyo alishughulikiwa. Kaisari Julius alipigwa visu baada ya kutaka kushindana na Seneti ya Roma. Ile nchi ilikuwa inaheshimu sana utawala wa sheria.

Wanafalsafa wakubwa wengi ambao tunawasoma ni aidha walitoka kwenye nchi ya Ugiriki au Roma, ambazo zilikuwa ni za kidemokrasia na zilitawala dunia kwa muda mrefu. Roma ilitawala dunia kwa miaka zaidi ya elfu moja kwasababu ya mfumo wake wa kidemokrasia.

Pengine hujasoma vizuri, Ufalme wa Uingereza ilipata mafanikio makubwa sana baada ya kutengeneza kuruhusu mifumo ya kidemokrasia. Walipitisha The Magna Carta mwaka 1215 iliyotoa mashauri makubwa ya haki za raia wa Uingereza. Wakatengeneza The Common Law ambao ni mfumo wa kisheria unaoruhusu Demokrasia. Wakaja wanafalsafa kama wakina A.V Dicey wakazungumzia The Rule of Law na mengineyo.

Huu mfumo wa kidemokrasia ndiyo uliyoifanya Uingereza kuwa taifa la kwanza duniani kuleta mapinduzi ya viwanda mwaka 1776. Akawa na nguvu sana na ndiyo ukawa mwanzo wa PAX BRITANNICA na Uingereza likawa taifa lenye nguvu duniani lililomiliki makoloni barani Marekani, Asia na Afrika.

Uchina yenyewe ya leo imebadilika sana. Baada ya kuona Mao Zedong kafariki wakaamua kuachana na falsafa za kidikteta zisizokuwa na kichwa wala miguu. Deng Xiaoping aliruhusu uhuru wa kiuchumi na mfumo wa masoko. Ambao mpaka leo hii Maraisi Jiang Zemin, Hu Juntao na Xi Jinping wanauheshimu.

Hoja ya mkuu Zitto iko katika nyanja kuu mbili. Mosi, Uhuru wa kisiasa ambao kwa lugha ya kiingereza ni Civili and Political Rights. Pili, Uhuru wa Kiuchumi ambao kwa lugha ya kiingereza ni Economic, Social and Cultural Rights. Unaweza kubana uhuru wa kisiasa lakini ukaachia uhuru wa kiuchumi. Ametoa na mfano hai kabisa wa Meles Zenawi, Vladmir Putin na Paul Kagame: Wanabana siasa lakini Uchumi uko wazi, kwasababu Uchumi ni masoko na namba.

Raisi wetu ametuvuruga kote, kwenye Siasa na kwenye Uchumi. Huyu ni mtu wa aina gani aisee ??? Uchumi ni namba mzee: Hauna morality, hela hata itoke kwa shetani kama tu inaongeza mzunguko then its all good for the economy. Sema cha muhimu tu ni kusimamia mgawanyo wa keki ya taifa pamoja na ushindani.

Sisi tumebugi kote na hatujui hata tunakoenda. Hivi mkuu chige wewe unaelewa sisi tunaenda wapi ?? Hebu mje na mkuu JokaKuu mtusaidie hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…