Zitooooo! Tatizo lako Mh. huwa huangalii kama ufahamu wako ni wa kweli. Najua sasa hivi una presha ya uchaguzi wa mwakani na huenda ungeomba haraka ya mageuzi ili mwakani yasikukute. Tatizo uliifanya siasa kama taaluma kumbe sivyo, na sasa unaanza kuona mwisho wake. Just be calm!
Nikuulize swali la tangu zamani; Ni nchi gani iliendelea kwa sababu ya demokrasia? Nitajie moja tu, ili nasi tuone unatumia ubongo wako. Sasa angalia unatumia historia iliyopindishwa. Hitler hakuwachukia wayahudi kwa sababu ya utajili wao kama unavyodanganya. Wapi uliona uongo wa aina hiyo au unasikia hadithi za mtaani? Ipo sababu moja muhimu kabisa ya Hitler ambayo si yeye peke yake kuwahi kuitumia, ilitumika na nchi nyingi za ulaya iliyostaarabika leo hii.
Pia, elewa kwamba Vyama vingi vya siasa ni muhimu lakini siyo lazima viwepo, na kutokuwepo siyo udikteta. Au kutokuwepo siyo kwamba maendeleo hayatakuja. China kuna vyama vingapi, Mheshimiwa? Nchi gani ina uchumi unaokuwa kwa haraka kuliko China? Unaleta nadhalia ya kianazuoni wakati huiwezi. HUna uzoefu wa hoja kama hizi, braza!
Athene ya Ugiriki iliendelea kwasababu ya Demokrasia, hadi kufikia hatua ya kutishia nchi za kidikteta zenye nguvu kubwa za kijeshi kama Sparta: Wasparta hawakupenda Demokrasia na mifumo ya Athene na wakaamua kuivamia kwenye vita ya Peloponnesian ya Mwaka 431 BC. Unachokisahau ni kwamba waathene walienda mbali na kutengeneza mfumo wa Demokrasia wa moja kwa moja (Direct Democracy)
Roma ya kale lilikuwa ni dola la kifalme lakini kimsingi ndiyo dola ambalo tunaiga mifumo yake ya kidemokrasia katika dunia yetu ya leo. Kaisari na nguvu zake zote zile ilikuwa ni lazima atii matakwa ya Seneti ya Roma na aliposhindwa kufanya hivyo alishughulikiwa. Kaisari Julius alipigwa visu baada ya kutaka kushindana na Seneti ya Roma. Ile nchi ilikuwa inaheshimu sana utawala wa sheria.
Wanafalsafa wakubwa wengi ambao tunawasoma ni aidha walitoka kwenye nchi ya Ugiriki au Roma, ambazo zilikuwa ni za kidemokrasia na zilitawala dunia kwa muda mrefu. Roma ilitawala dunia kwa miaka zaidi ya elfu moja kwasababu ya mfumo wake wa kidemokrasia.
Pengine hujasoma vizuri, Ufalme wa Uingereza ilipata mafanikio makubwa sana baada ya kutengeneza kuruhusu mifumo ya kidemokrasia. Walipitisha The Magna Carta mwaka 1215 iliyotoa mashauri makubwa ya haki za raia wa Uingereza. Wakatengeneza The Common Law ambao ni mfumo wa kisheria unaoruhusu Demokrasia. Wakaja wanafalsafa kama wakina A.V Dicey wakazungumzia The Rule of Law na mengineyo.
Huu mfumo wa kidemokrasia ndiyo uliyoifanya Uingereza kuwa taifa la kwanza duniani kuleta mapinduzi ya viwanda mwaka 1776. Akawa na nguvu sana na ndiyo ukawa mwanzo wa PAX BRITANNICA na Uingereza likawa taifa lenye nguvu duniani lililomiliki makoloni barani Marekani, Asia na Afrika.
Uchina yenyewe ya leo imebadilika sana. Baada ya kuona Mao Zedong kafariki wakaamua kuachana na falsafa za kidikteta zisizokuwa na kichwa wala miguu. Deng Xiaoping aliruhusu uhuru wa kiuchumi na mfumo wa masoko. Ambao mpaka leo hii Maraisi Jiang Zemin, Hu Juntao na Xi Jinping wanauheshimu.
Hoja ya mkuu
Zitto iko katika nyanja kuu mbili. Mosi, Uhuru wa kisiasa ambao kwa lugha ya kiingereza ni Civili and Political Rights. Pili, Uhuru wa Kiuchumi ambao kwa lugha ya kiingereza ni Economic, Social and Cultural Rights. Unaweza kubana uhuru wa kisiasa lakini ukaachia uhuru wa kiuchumi. Ametoa na mfano hai kabisa wa Meles Zenawi, Vladmir Putin na Paul Kagame: Wanabana siasa lakini Uchumi uko wazi, kwasababu Uchumi ni masoko na namba.
Raisi wetu ametuvuruga kote, kwenye Siasa na kwenye Uchumi. Huyu ni mtu wa aina gani aisee ??? Uchumi ni namba mzee: Hauna morality, hela hata itoke kwa shetani kama tu inaongeza mzunguko then its all good for the economy. Sema cha muhimu tu ni kusimamia mgawanyo wa keki ya taifa pamoja na ushindani.
Sisi tumebugi kote na hatujui hata tunakoenda. Hivi mkuu
chige wewe unaelewa sisi tunaenda wapi ?? Hebu mje na mkuu
JokaKuu mtusaidie hapa.