Tanzania imetimiza hatua zote 4 kuwa nchi ya kidikteta


Udikteta siyo relative term. Hii revisionism yenu ya Chuo Kikuu cha Mlimani na maprofesa wake inawadanganya. Kisheria na Kisiasa Udikteta ni utawala wa kiimla katika ngazi ya kitaifa tu (No exceptions). Kwenye ngazi ya kichama huwaga hakuna udikteta...

Kumlinganisha Khomeni mwenye dola na Zitto ambaye hana dola ni ujuha wa hali ya juu sana. Chama ni chombo ambacho mtu anaweza kuamua kuwepo au kutokuwepo hivyo hakuwezi kuwa na udikteta kama mtu anaamua mwenyewe kuwepo, kama hukubaliani na chama unaruhusiwa kutoka. Taifa ni tofauti kabisa, hata usipokubaliana na watawala utakuwepo tu maana huna jinsi.Ndiyo maana tunasema udikteta ni hatari sana kwa taifa.....

Hili ni la mwaka wa kwanza Chuo Kikuu kwenye aina ya mifumo ya Utawala duniani. Waalimu wenu hawakuwambia kwamba Udikteta ni nadharia inayotumika kwenye ngazi ya kitaifa tu ???
 
Hilo baadhi yetu tumeshawaambia sana lakini wapi! Watu wenyewe hawajielewi.

Baadhi yetu hatuna shida na kuongozwa na ccm. Miaka hii yote tumeongozwa na ccm na hata kuichagua. Wametuongoza kwa kiwango cha kuridhisha. Ndiyo maana demokrasia iliendelea kushamiri nchini. Wala hatutamani sana siku moja ccm ishindwe; tunachotamani ni ushindani utakaopelekea wenye madaraka kujiheshimu na kuwaheshimu wapigakura. Wazee wa ccm tuko nao huku mtaani nao wanajuta. Wengi wao wanasubiri tu muda upite. Ila baadhi yenu mngependa sana uovu wote unaolalamikiwa uelekezwe ccm badala ya rais. No way. Kinachosababisha kelele hizi ni sera za ccm kutelekezwa na katiba ya nchi kusiginwa. Na aliyefanya haya yote ni mtu aliyepewa mamlaka za kifalme na katiba yetu tukidhani atatumia kwa manufaa yetu sote na mengine kajiongezea mwenyewe kinyemela kwa maslahi yake binafsi. Ndipo Mzee mmoja wa ccm akamtaka aache kujitukuza yeye mwenyewe na badala yake apeleke sifa na utukufu ccm! Je, amefanya hivyo? Sasa ccm inatoka wapi hapa? Pambaneni wenyewe; ccm msiingizi kwenye vita vyenu vya utukufu binafsi!
 
Pamoja na Demokrasia ya Ethiopia Mheshimiwa unajua kwasasa kwa jina la demokrasia kuna mauuaji makubwa ya raia yanaendelea Ethiopia.

'Thousands flee' Ethiopia ethnic conflict

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli alikuwa na haki ya kutumia mkono wa chuma kurejesha nchi hii kwenye maadili aliyotuacha nayo baba wa taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi ni kichekesho cha kipekee, unaanzisha uzi kuhusu udikteta na unasomwa na watu!.

Nchi za kidikteta unaweza hata kuanzisha uzi na ukapata mrejesho wa jamii?.

Unashangaa nini, kwani hujawahi kuona ?
Unachochanganya wewe ni Freedom of Speech and Freedom after Speech. Kwenye nchi za kidikteta watu huwa wanaongea sana, lakini wanakipata cha mtema kuni baada ya kufanya hivyo.

Ndiyo maana leo nchi kama Korea Kaskazini ina maelfu ya wafungwa wa kisiasa. Uturuki ndiyo imeipiku hadi Uchina kwa kufungia waandishi wa habari.

Udikteta huwa hauzuii watu kuongea, watu kusema watasema tu. Bali udikteta ni kuwashughulikia watu baada ya kuongea sasa......
 
Hoja za Zitto kwa kifupi ni......

1. Vita dhidi Wafanyabiashara Wakubwa
2. Nepotism - Undugunazation katika teuzi
3. Kudhibiti vyombo vya habari
4. Kudhibiti vyama vya siasa.

Hayo ni maoni yake na mtazamo wake. Zitto anatakiwa kusema jitihada zake binafsi za siri alizofanya kujipendekeza kwa JPM baada tu ya uchaguzi Mkuu hadi Mwaka 2016 lakini aliposhindwa ushawishi wake ndio aliapa atampinga mwanzo mwisho.
Hizi ndo Siasa purely za Kinafiki.
 
Acha wongo, Hitler hakushinda dhidi ya Raisi Hindenburg mara zote mbili. Adolf Hitler alitokea bungeni baada ya chama chake kuwa kikubwa na chenye nguvu na kumfanya Herman Gōring kuwa kama spika: Wakaunganisha nguvu na vyama vingine kuwapinga wakomunisti.

Hitler aliteuliwa kuwa Chancellor "Waziri Mkuu" hakushinda uchaguzi wowote ule nchini Ujerumani.....

Wewe ni mwongo sana......
 
Huwezi kuwa unatukana viongozi wakubwa wa nchi halafu uachwe eti kwa kigezo cha uhuru wa kujieleza. Toa maoni ya kiungwana, hakuna atakayekugusa.
 

Sidhani kama hapa ni suala la IQ. Hapa ni maslahi tu. Siku hizi nadhani hata njia ya ya kulipia hayo maslahi imebadilika kutoka "in kind" kwa njia ya uteuzi kwenda "in cash". Ndiyo maana hata jambo liwe la hovyo kiasi gani watetezi watakuwepo tu alimradi haliwaathiri wao moja kwa moja. Kikokotoo tu ndiyo iliyokosa watetezi kwani kila mmoja aliguswa!
 
Hiyo dunia nzima ni yako wewe na ukoo wako ??? Hitler hakushinda uchaguzi wa Uraisi dhidi ya Hindenburg mara zote mbili. Wala chama chake hakikushinda. Wanazi walifanikiwa kupata siti nyingi bungeni tu.
Paul Hindenburg alikuwa na kura milioni 19 sawa na asilimia 50%, huku Adolf Hitler akiwa na kura milioni 13 sawa na asilimia 36.8% na Thälmann alikuwa na kura milioni 3 sawa na asilimia 10%. Sasa wewe hili la Chama cha wanazi kushinda uchaguzi umelitoa wapi ??

Chama cha wanazi kwenye uchaguzi wa mwaka 1932 kilishinda viti 196 sawa na asilimia 33.09% wakifuatiwa na Social Democrats walioshinda viti 121 sawa na asilimia 20.43% na mwisho kabisa Communist Party wakishinda viti 100 sawa na asilimia 16.86%. Wanazi walipata siti nyingi bungeni hadi wakaweka spika, lakini hawakushinda uchaguzi.....

Wongo wako peleka kwenu.....
 
Umenichanganya mkuu! Unazitaja Greek na Roman empire kama mifano ya demokrasia na kuiweka pia uchina. Je, kwa vigezo vya leo unaweza ukasema China ina demokrasia? Ni yale yale ya akina Zitto wanayokataa kwamba TZ hakuna Demokrasia. Demokrasia ya Greek na roman haikumaanisha vyama vingi. Hii ya akina Zitto inamaanisha vyama vingi, na kama hakuna basi demokrasia hakuna. Wakigomewa mambo yao huo ni udikteta.

Back to democracy, je, unafahamu kuanguka kwa Greek na Roman empire haikutokana na u-dikteta? Ilitokana na ustaraabu (Wa wakati huo). The recent long Ottoman empire nayo hivyo hivyo. UHuru wa kiuchumi wa China siyo ingredient ya demokrasia.
btw. Ulimuelewaje Zitto bungeni kuamini kwamba umaskini TZ ulipungua wakati wa utawala wa kikwete? Indicator yake ni idadi ya watu walioingia ktk kipato kikubwa, lakini hataji walioingia ktk umaskini. He is just another stupid pretender.
 
Siasa zinachukua mda wa maendeleo tunakaa tunalumbana badala ya kufanya kazi.CCM kupitia Rais Magufuri waliomba kura kupitia Irani yao hili wachaguliwe wakafanikiwa waachwe wafanye kazi..Uhuru wakujieleza ni mkubwa sana Tatizo letu badala ya kuelezo changamoto zinatukabili katika maeneo yetu tunaanza kutukana na kashifa juu.Toka Mkuu ameingia madarakani
amefanya kazi kubwa sana Kuanzia
huduma za afya miundombinu kununua
ndege na kununua meli ziwa Victoria
japo aijafika. Kasimamia maadili kwa
viongozi wa umma na serikali ukienda
kwenye madini kaboresha mikataba ya
ovyo kaongeza uwazi hayo anayosemwa
kwa mabaya ni propaganda.Mungu
azidi kumsimamia hii kazi sio ndogo..
 
Huwezi kuwa unatukana viongozi wakubwa wa nchi halafu uachwe eti kwa kigezo cha uhuru wa kujieleza. Toa maoni ya kiungwana, hakuna atakayekugusa.
Unachanganya mambo tena: Kuna wafungwa wa makosa ya jinai na wafungwa wa makosa ya jinai yatokanayo na shughuli za kisiasa. Huwezi kumdhuru mtu kwa kusema kwamba ununuzi wa ndege siyo kipaumbele, au kusema kupeleka SGR Rwanda ni kukosa mkakati wa kibiashara. Huyu Mzee hataki aambiwe ukweli, yeye amekuwa nani ?
 
Maana/Dhana ya DEMOKRASIA hasa ni ipi mkuu!
Demokrasia ni pana sana, lakini hasa iko katika nyanja kuu mbili. Mosi, nyanja ya kinadharia au kitunu. Pili, nyanja ya kimfumo.

Kwenye nadharia tunasema Democracy is a highest morality of aspiration which nations strives to reach, this value entails greater freedom, adherence to the rule of law and protection of human rights and civil liberties which enables the development of human faculties.

Kwenye mfumo wa kiutawala tunasema Democracy is a state that is governed/ruled by following democratic principles and values: And such system can be manifested through the Supremacy of the Constitution, Separation of Powers, Independence of the Judiciary and Parliamentary Sovereignty. Mfano Uingereza na Marekani.

Hivyo basi hata Ukomunisti unaweza kuwa ni nadharia na mfumo wa kiutawala pia.
 

Hivi Zitto, kati yako na Magufuli nani diktekta? Ndani ya chama cha ACT hakuna wa kukohoa mbele yako, mwenyewe unajiita 'kiongozi mkuu' , kila kitu wewe.
 
Emenena vizuri sana,
ILA NCHI HII ITABAKI KAMA ILIVYO MPAKA ITAKAPOPATA RAIS MZALENDO WA KWELI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wamebadilika na kuwa wana Demokrasia.
Nini maana ya Demokrasia ...maana kukosoa mnakosoa tena muda mwingine mnatoa kashfa na kukashifu ..na mnaishi vizuri tu ,labda milango ya madili ndio imefungwa
 
Ndugu, nazi party kilikuwa na majority kwenye German Reichtag (Bunge) kwanza unaelewa Uchaguzi wa Ujerumanina Kansela anavyopatikana, tuanzie hapo isije kuwa tunabishana wakati mambo ya msingi hayako sawa!
Wewe mimi siyo ndugu yako: Halafu aliyemchagua Hitler kuwa Chancellor ni Raisi Paul Von Hindenburg, January 1933. Cheo hiki siyo cha kuchaguliwa bali kuteuliwa ambapo chama chenye viti vingi ndiyo hupata nafasi.

Baada ya Raisi Hindenburg kufariki Hitler ndiyo akawa dikteta kamili, Mkuu wa Serikali na Mkuu wa nchi.

Hizi nyingine ni blah blah zake zisizo na maana yoyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…