#COVID19 Tanzania imewasilisha ombi la kujiunga na mpango wa kugawana chanjo dhidi ya Covid-19

Mungu atawahukumu siku moja liteendeeni taifa hili kama muaonavyo ipo siku mtalipa gharama,mtajutia uamuzi huu.

Nchi iko salama mnataka kuleta taharuki na kuangamiza vizazi vijavyo,ole wenu.

Ni nchi gani iko salama kwa sababu wamechanjwa? Hakuna uchungu na maisha ya Watanzania mnaendekeza pesa za mkopo?
Sasa tuwe watumwa kwa kipande cha mkate.
lazima mjue kilio cha wana wa Tanzania kitakapofiki kwenye kiti cha enzi ndo mtajua yuko Mungu aliyeumba mbingu na nchi.
wasikilizeni tu hao wanao wapotosha.
 
Chanjo ni hiari jombi. Wewe si ubaki na m*vi yako? Kwani umelazimishwa?
 
Hata kabla hatujawapelekea takwimu za maambukizi na vifo tayari wametuletea chanjo? Haraka ya nini?
 
Akili yako kidogo sana huwezi chambua mambo ndo maana unakimbilia matusi uliyozoea na wenzio kijiweni.

Pole kwa kudhani una uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kiasi cha kujifunga kimawazo:

1. Kubaki na m*vi si tusi bali nukuu rasmi toka kwa aliyekuwa rais wa nchi hii.

2. Kwamba chanjo ni hiari yamechambuliwa mno hayo kiasi hakuna haja ya uchambuzi zaidi.

Tulipo sasa ni kila mtu achukue njia yake. Wenye kuchanjwa tupo msiotaka chanjo mpo. Shida gani hapo tupigishane kelele?
 
Akili zako unazijua manyewe!
Furaha yako ni kuona Tanzania watu wanakufa kwa Corona...ndyo maana unahangaika Sana ww!

Kweli wewe ni michosho kama id yako ilivyo.

Wapi penye furaha yangu na mtu kufa achilia mbali watanzania?

Mbona mko hivyo? Lengo lenu tusichanjwe? Acheni kuchanjwa nyie lakini sisi tutachanjwa hapa hapa na wapendwa wetu kwa maisha yetu.
 
Pole kwa kudhani una uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kiasi cha kujifunga kimawazo:

1. Kubaki na m*vi si tusi bali nukuu rasmi toka kwa aliyekuwa rais wa nchi hii.

2. Kwamba chanjo ni hiari yamechambuliwa mno hayo kiasi hakuna haja ya uchambuzi zaidi.

Tulipo sasa ni kila mtu achukue njia yake. Wenye kuchanjwa tupo msiotaka chanjo mpo. Shida gani hapo tupigishane kelele?
Kwa vile umezidi kunituka bila sababu utapatwa na jambo baya sana tangu kuzaliwa,utajutia matusi yako haya,ili ujue kuwaheshimu watu.
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limepokea taarifa rasmi ya Tanzania kuomba kujiunga na mpango wa COVAX unaolenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo.

Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt Matshidiso Moeti amesema hii leo kuwa chanjo hizo zinaweza kuingia Tanzania katika kipindi cha wiki mbili.

"Tumepata taarifa kuwa sasa ni rasmi Tanzania ipo katika mchakato wa kujiunga na mpango wa chanjo wa COVAX," Dkt Moeti ameuleza mkutano wa waandishi wa habari hii leo.

Utoaji wa Takwimu za Corona kuipa Tanzania dola milioni 574
Hatua hiyo inaendana na mapendekezo amabayo kamati maalumu ya ushauri ambayo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan punde tu baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu.

Mwezi mmoja uliopita, Mei 17 kamati hiyo ilitoa mukhtasari wa taarifa yake na kushauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa covax ulio chini ya mwamvuli wa Gavi.

Mpango wa covax unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi. Mwamvuli wa Gavi unaundwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya Duniani na baadhi ya serikali za nchi tajiri duniani.

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud Mei 17 mwaka huu.

"Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi," alieleza Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili na Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Rais Samia amechukua mkondo tofauti na wa mtangulizi wake hayati John Magufuli katika kulishughulikia janga la corona. Wakati Rais Magufuli alikosolewa kwa kutokufuata moja kwa moja mapendekezo ya kisayansi yaliyothibitishwa na WHO, Rais Samia amejipambanua kutaka kuendana na ulimwengu katika kufuata njia zinazopigiwa chapuo na WHO.

Afisa Mwandamizi wa mpango wa chanjo wa WHO kwa kanda ya Afrika Richard Mihigo amewaambia wanahabari katika mkutano wa leo uliofanyika mtandaoni kuwa tayari Tanzania imekamilisha hatua za awali za kutuma maombi ya chanjo kutoka COVAX na inaandaa mpango wa kupokea na kugawa chanjo.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa hata hivyo hakukanusha au kuthibitisha suala hilo alipozungumza na BBC akisisitiza kuwa serikali itatoa taarifa rasmi kwa umma muda muafaka utakapofika juu ya suala hilo.

Chanzo bbc swahili
 
Kwa vile umezidi kunituka utapatwa na jambo baya tangu kuzaliwa,utajutia matusi yako haya,ili ujue kuwaheshimu watu.

Pole tena. Kwa kukuongezea tusitishane.

Wapi umetukanwa? Nukuu ya mzee baba si tusi. Au "kukutuka" ndiyo nini kwenye lugha yenu pendwa?

Habari ndiyo hiyo.
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa limepokea taarifa rasmi ya Tanzania kuomba kujiunga na mpango wa COVAX unaolenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo.
Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt Matshidiso Moeti amesema hii leo kuwa chanjo hizo zinaweza kuingia Tanzania katika kipindi cha wiki mbili.
"Tumepata taarifa kuwa sasa ni rasmi Tanzania ipo katika mchakato wa kujiunga na mpango wa chanjo wa COVAX," Dkt Moeti ameuleza mkutano wa waandishi wa habari hii leo.
Mtihani wa Rais Samia kudhibiti corona Tanzania
Utoaji wa Takwimu za Corona kuipa Tanzania dola milioni 574
Hatua hiyo inaendana na mapendekezo amabayo kamati maalumu ya ushauri ambayo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan punde tu baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu.
Mwezi mmoja uliopita, Mei 17 kamati hiyo ilitoa mukhtasari wa taarifa yake na kushauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa covax ulio chini ya mwamvuli wa Gavi.
Mpango wa covax unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi. Mwamvuli wa Gavi unaundwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya Duniani na baadhi ya serikali za nchi tajiri duniani.
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud Mei 17 mwaka huu.
CHANZO CHA PICHA, IKULU, TANZANIA
Maelezo ya picha,
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud Mei 17 mwaka huu.
"Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi," alieleza Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili na Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Rais Samia amechukua mkondo tofauti na wa mtangulizi wake hayati John Magufuli katika kulishughulikia janga la corona. Wakati Rais Magufuli alikosolewa kwa kutokufuata moja kwa moja mapendekezo ya kisayansi yaliyothibitishwa na WHO, Rais Samia amejipambanua kutaka kuendana na ulimwengu katika kufuata njia zinazopigiwa chapuo na WHO.
Afisa Mwandamizi wa mpango wa chanjo wa WHO kwa kanda ya Afrika Richard Mihigo amewaambia wanahabari katika mkutano wa leo uliofanyika mtandaoni kuwa tayari Tanzania imekamilisha hatua za awali za kutuma maombi ya chanjo kutoka COVAX na inaandaa mpango wa kupokea na kugawa chanjo.
Msemaji wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa hata hivyo hakukanusha au kuthibitisha suala hilo alipozungumza na BBC akisisitiza kuwa serikali itatoa taarifa rasmi kwa umma muda muafaka utakapofika juu ya suala hilo.
Chanzo bbc swahili.
Haya sasa jiandaeni kudungwa syringe za covax kwenye mabega mara moja.
 
Back
Top Bottom