Tanzania ina watu na ardhi: Tunafeli wapi katika mkakati wa uzalishaji na kupunguza utegemezi wa nje ?

Kwa hiyo wewe unachosubiri ni kulima hayo ma-kilomita ya mraba 900,000, ndipo ujuwe Tanzania kuna kilimo?
Kiufupi tu ni kwamba nimejiridhisha huna unachojuwa; huna tofauti yoyote na machizi wengi ninayokutana nayo humu JF.
jina lako linaonyesha wewe ni mweupe kichwani full stop
 
Mkoa wa Pwani uko mbali sana kwa viwanda
Hakuna mkoa wowote utakuja kuwafikia kwenye viwanda

1792072373841.png

1792072431339.png

1792072495579.png

1792072526226.png

1792072552696.png

1792072575214.png

1792072596841.png

1792072625884.png
 
Hujaelewa hoja yangu. Ili mkulima wa hapa nchini apate faida kwenye kilimo cha ngano inabidi bei anayouzia iwe juu kuliko bei ya ngano kwenye soko la dunia. Inabidi watanzania wanunue ngano ya ndani kwa bei ya juu kuliko wanayonunua sasa ngano kutoka nje. Sababu ni kuwa mkulima wa Marekani, Canada au Ulaya anazalisha hiyo ngano kwa bei ya chini sababu ya ruzuku.
Very interesting!

Na hili lingekuwa shina la mjadala kwenye mada muhimu kama hii.

Mkulima wa Marekani anazalisha ngano au soya, halafu anaiuza kwa bei nafuu zaidi kwenye soko la dunia kuliko mzalishaji wa Tanzania!

Najuwa siyo swala la ruzuku pekee, bali hata katika 'efficiency' ya uzalishaji na hata usafirishaji (chain nzima) anayotumia mzalishaji wa Marekani kulinganisha na wa hapa Tanzania.

Samia alikwenda China, nadhani ni mwaka jana; Xi Jinping kamwambia nenda kazalishe Soya, soko lipo hapa China bwerere! Mama wa watu hata hakujihangaisha hadi leo.

Kwani ni nini hasa kinachotafutwa na serikali kuhusu wananchi wake, kama siyo kuwasaidia wajikwamue toka kwenye umaskini.
Ni pesa kiasi gani zinazotapanywa tu na serikali katika matumizi yasiyokuwa na msingi wowote katika maisha wa watu; pesa ambayo ingeweza kutumika kuwasaidia kundi hilo la walima Soya kwa miaka miwili au mitatu ili na wao waweze kufikia kiwango cha kuuza soya yao China kwa bei inayokaribiana na ya mkulima wa Marekani. Hawa wakulima mwisho wa hiyo miaka miwili mitatu, kweli watakuwa bado hawajapata uelewa na kuweza kuonyesha mabadiliko katika hali zao za kimaisha na kujiendeleza wenyewe?

Nikirudi kule kwenye maelezo yako sahihi kabisa; na kujiuliza, maana yake ni nini kwa wakulima wa Tanzania? Kwamba kilimo chetu kiko 'doomed', kwa vile hatuwezi kushindana na mapapa ya uzalishaji duniani?

Mahindi yetu hapa yamenunuliwa mara nyingi tu hata na taasisi za dunia kulisha wakimbizi; na najuwa soko kwa majirani na kwenye ukanda huu hawatategemea soko la dunia kuliko soko la hapa hapa kwenye kanda yetu

Nimalize kwa mfano wa waChina na utengenezaji wao wa magari ambao sasa unatawala dunia na kuwaliza hao hao waliokuwa vinara wa sekta hiyo. Na siyo magari pekee; katika kila eneo la uzalishaji Mchina sasa ndiye kinara wa uzalishaji anayehofiwa duniani kote. Ni wajibu wetu na sisi kujifunza na kuwa mashuhuri zaidi katika nyanja tunazoweza kuzimudu vyema zaidi ya wengine.

Ni swala la uongozi tu, kuwasaidia waTanzania kutimiza wajibu wao katika kujiletea maendeleo wenyewe.
Gesi na madini lukuki yanayonadishwa hovyo, hizi ndizo zingekuwa nyenzo zetu muhimu za kujikwamua kama taifa toka kwenye umaskini huu tunaoushuhudia wa wananchi wetu.

"It can be Done", kama alivyosema Mwalimu.
 
Mkuu 'nusuhela'...
Nimesoma habari yako hii ya kusikitisha, na hitimisho ulilo liweka kuwahusu waTanzania; kidogo limenisikitisha.

Kwanza hii taarifa ya 'sister'wako, hii ni ya upande mmoja, upande wako. Hatujasikia lolote ambalo kama huyo 'sister' angepata nafasi ya kujieleza, pengine tungepata habari ya upande wake.
Kwa hiyo hapa ni vigumu kumlaumu 'sister' wako kutokana na jinsi alivyo lichukulia wazo lako.
Binafsi nahisi kuwa hukumshirikisha vizuri toka mwanzo, ulipojadili wazo hilo na mama yenu ili muweze kutoka na wazo la pamoja nini kifanyike.

Sasa hili la kuchukkulia mfano wa kifamilia, na kuuingiza kwenye uamzi wa kitaifa nalo ni tatizo kubwa.
Maana ya kuwa na uongozi imara na wenye lengo la maslahi ya waTanzania wote ni hilo la kuongoza na kueleza mipango kamili ya maendeleo, na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi mengi yanayohusu maendeleo yao. Uongzi siyo swala la kuagiza tuu watu wafanye nini

Kwa hiyo, bila ya kuandika mengi, sikubaliani kamwe na hizo lawama unazowatupia waTanzania. Walaumu watawala wasiojuwa wajibu wao wa uongozi wa taifa hili ni nini.
Mkuu ahsante kwa kuelewa. Ila lengo la kuleta hili ni kujaribu kuwaelewesha namna watanzania wanavyoishi kimazoea na sio kufanya vitu kwa tija.

Changamoto zinaanzia kwenye ngazi ya familia mpaka taifa. Imagine mtu kama sister ndo akepewa nafasi ya uongozi, unahisi kutakua na mabadiliko?
 
Nashangaa sana kuwa hukuelewa chochote katika hayo niliyoyaandika hapo; maana unarudia tu kama ulivyoanza mwanzo kabla sijakuandikia chochote.
Unao uhakika kuwa unaweza kusoma kitu na kukielewa vizuri?.

Kwa jinsi inavyoonekana hapa, nashawishika kuwa "siter" wako ni bora zaidi kuliko unavyomsagia hapa.
 
Yupo sahihi kabisa mkuu wala hujakosea. Huenda Mimi ndo mwenye changamoto
 
Ardhi ya Tanzania inamilikiwa na wakoloni, serikali ni dalali tu
Mwananchi anapagishwa na dalali.

Source: visiwa vinauzwa huko Zanzibar,ziwa Tanganyika na pwani ya dar es salaam
 
Yupo sahihi kabisa mkuu wala hujakosea. Huenda Mimi ndo mwenye changamoto
Kutokana na haya uliyoweka humu, nashawishika kabisa kukubaliana na wewe kuwa huenda ndie tatizo.
Tungebahatika kumsoma "sister" anayosema, tungeondoa shaka zaidi juu ya nani anayeweza kuaminika kati yenu.

Basi, hili tuliachie hapa, hakuna sababu ya kuliendeleza zaidi.
 
Nafikiri wewe umehamiwisha mada kutoka kwenye matumizi sahihi ya ardhi ili kujikwamua kiuchumi na kwenda kwenye persal issues.

Lengo langu lilikua ni kutoa mfano wa kwanini hatuwezi kutumia ardhi ikatunufaisha. Hoja zangu zilikua ni kutokua na taarifa sahihi pamoja na kutokua na ushirikiano.

Watu wanaishi kwa mazoea hawataki kubadilika. Hata umlete malaika hapa kwetu Tz kubadili akili zetu ni ngumu sana.

Issue ya sister ilikua ni mfano tu wa kwanini hatutoboi wala sio kumsagia kunguni kwasababu sijamtaja jina wala kuweka picha yake. Ulikua ni mfano wewe umekimbilia kuni attack.

Tena nimesema kabisa, Lana ng'ombe wa maziwa. Ili kuufanya mradi uwe na tija, malisho ni lazima yawepo sio kuhangaika kutafuta kwenye mifereji.

Kipi hukuelewa?
 
Wakuu,

Tunapozungumzia maendeleo ya nchi yetu, msingi mkuu wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuwa wazi: nchi inahitaji WATU NA ARDHI ili kujiletea maendeleo. Leo hii, miaka mingi tangu kuanzishwa kwa misingi hiyo, bado tunakabiliwa na kitendawili cha kuwa na rasilimali hizi mbili lakini bado tukategemea chakula na malighafi kutoka nje.

Nimeamua kuandika uzi huu kwa kuangalia kwa kina suala la kilimo, hasa uzalishaji wa ngano, tukizingatia nguvu kazi yetu (watu) na ardhi tuliyonayo.

Tuna Ardhi Kubwa, lakini kwa nini Tunashindwa Kujitosheleza kwa Ngano?

Hebu tuangalie zao la ngano.

Tanzania ina maeneo yenye mazingira yanayofaa kabisa kwa kilimo cha ngano, hususan katika nyanda za juu za kaskazini na kusini. Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Njombe, Mbeya na Rukwa ni miongoni mwa maeneo muhimu yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji.

Hata hivyo, mahitaji ya ngano nchini ni makubwa kuliko uzalishaji wetu wa ndani, na hivyo tunalazimika kuagiza kiasi kikubwa kutoka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa takwimu za biashara za kimataifa (World Bank/UN Comtrade) na ripoti za kiuchumi, Tanzania iliagiza ngano na meslin zenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 392.2 mwaka 2024, kiasi kilichofikia takribani tani milioni 1.344. Takwimu hizi kutoka mabenki na taasisi za kifedha zinatupa picha halisi ya fedha nyingi za kigeni zinazotoka nchini kila mwaka kununua zao ambalo lingeweza kulimwa hapa nyumbani na Watanzania wenyewe.

Hoja yetu si kuacha kuagiza ngano mara moja, bali ni kuwa na mkakati thabiti wa kupunguza utegemezi huo kwa kuongeza tija na ushindani wa uzalishaji wa ndani.

Kuangalia mifano ya nchi kama Saudi Arabia na Ukraine kunaweza kutusaidia kuona namna ambavyo rasilimali watu na ardhi zinavyoweza kutumiwa kwa ufanisi au kukabiliwa na changamoto:

Saudi Arabia: Hii ni nchi yenye asilimia kubwa ya jangwa, upungufu mkubwa wa maji, na changamoto za asili katika kilimo. Pamoja na hayo, imewekeza kwa nguvu katika teknolojia, mifumo ya kisasa ya umwagiliaji, na mikakati ya usalama wa chakula ili kulinda uzalishaji wake wa ndani.

Ukraine: Inajulikana kama moja ya vikapu vya chakula duniani (breadbasket). Licha ya changamoto kubwa za kiusalama na vita vilivyoanza mwaka 2022, nchi hiyo imeendelea kuonyesha jinsi sekta ya kilimo ilivyowekewa mifumo madhubuti ya uzalishaji na usafirishaji wa nafaka kimataifa.

Somo kwetu si kwamba nchi hizi hazina changamoto, bali ni kwamba usalama wa chakula ni suala la mkakati wa kitaifa, uwekezaji sahihi, na usimamizi wa rasilimali watu na ardhi.

Swali la msingi ni hili:

Tunawezaje kujenga mfumo utakaotumia kwa ufanisi ardhi yetu na nguvu kazi yetu kupunguza utegemezi huu?

Tatizo sio Ardhi Pekee; ni Tija na Mipango ya Uzalishaji

Mara nyingi tunajivunia kuwa na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo. Lakini kumiliki ardhi si sawa na kuwa na chakula mezani.

Kilimo chenye tija kinahitaji mchanganyiko wa mambo ya msingi yafuatayo:

Mbegu Bora na Pembejeo: Zinazopatikana kwa wakati na kwa bei inayomuduwa na wakulima wadogo na wa kati.

Umwagiliaji na Teknolojia: Kuacha kutegemea mvua pekee na kutumia mashine na zana za kisasa za kilimo ili kuongeza mavuno kwa hekta.

Utafiti na Wataalamu: Kuunganisha taasisi za utafiti na changamoto halisi za mashambani.

Ufadhili na Masoko: Mitaji yenye riba nafuu kwa wakulima na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mazao.

Kama tunataka kupunguza uagizaji wa ngano, tunahitaji mpango kazi maalum wa miaka 5 hadi 10 wenye malengo yanayopimika: eneo litakalolimwa, tani zinazotarajiwa kwa hekta, gharama za uzalishaji, na ushirikishwaji wa viwanda vya ndani vya kusaga ngano kununua mazao ya wakulima wa nyumbani.

Wataalamu Wetu na Nguvu Kazi: Tunawatumia Vipi?

Tanzania ina vyuo na taasisi bora zinazozalisha wataalamu wa kilimo, zikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na taasisi mbalimbali za utafiti.
Hata hivyo, kuna pengo kubwa kati ya elimu inayotolewa na mazingira halisi ya uzalishaji:

Wahitimu wengi wa kilimo wanajikuta wakifanya kazi nje ya taaluma zao kutokana na ukosefu wa mifumo inayowezesha kuanzisha biashara za kilimo au kupata ardhi ya uzalishaji kwa urahisi.

Vijana wetu wana nguvu kazi na maarifa, lakini mfumo unashindwa kuwakutanisha na mitaji, ardhi iliyopimwa kwa ajili ya kilimo cha kibiashara, na teknohama za kisasa.

Ukuaji wa uchumi na usalama wa chakula hauwezi kufikiwa ikiwa tutaendelea kulalamika kuhusu ukosefu wa ajira wakati rasilimali yetu kubwa (wataalamu na vijana) haijapewa nyenzo za kuzalisha mali kwenye ardhi yetu.
Hatuna siasa safi wala uongozi bora.

Siasa safi ni pamoja na kuheshimu mawazo ya watu, kuwapa wananchi uhuru wa majadiliano, kuimarisha utawala wa sheria na kuacha taasisi zifanye kazi bila kuingiliwa.

Uongozi bora ni pamoja na mchujo (vetting) mkali ili kupata watu wenye uwezo wa kiutendaji, kiuweledi,kimaadili na kuwapa nafasi za uongozi.
Pia mifumo ya kuwapata hao watu wa kuwa viongozi, ( uchaguzi na uteuzi) iwe ni mifumo bora inayolindwa kisheria na ya huru, haki na wazi.
 
Sisi wabongo ni wanafiki sana ,kwa Nini tuna act kuwa wananchi wenye Hasira Kali pale tunapomkamata kibaka mtaani kaiba mkate au kuku,huku mafisadi papa majuzi ya rasilimali za vizazi vinne vijavyo vya TAIFA,hayo majizi tunayapigia makofi na kuyasifu na kuya abudu,ili hali hata ripoti ti za CAG zinakuelezea ufisaidi.
Mbona wananchi wenye Hasira Kali wanaonea WANYONGE TU vibaka wadogo wadogo wanaokula kwa UREFU WA kamba Yao kuona mkate au kuku yale mapapa mafisadi yanayokula kwa UREFU WA kamba ndefu..hizo Hasira Kali kwao hazipo..mnawapigia makofi??
 
Attachments

  • 47490.jpeg
    47490.jpeg
    52.7 KB · Views: 4
Nafikiri wewe umehamiwisha mada kutoka kwenye matumizi sahihi ya ardhi ili kujikwamua kiuchumi na kwenda kwenye persal issues.

Lengo langu lilikua ni kutoa mfano wa kwanini hatuwezi kutumia ardhi ikatunufaisha. Hoja zangu zilikua ni kutokua na taarifa sahihi pamoja na kutokua na ushirikiano.

Watu wanaishi kwa mazoea hawataki kubadilika. Hata umlete malaika hapa kwetu Tz kubadili akili zetu ni ngumu sana.

Issue ya sister ilikua ni mfano tu wa kwanini hatutoboi wala sio kumsagia kunguni kwasababu sijamtaja jina wala kuweka picha yake. Ulikua ni mfano wewe umekimbilia kuni attack.

Tena nimesema kabisa, Lana ng'ombe wa maziwa. Ili kuufanya mradi uwe na tija, malisho ni lazima yawepo sio kuhangaika kutafuta kwenye mifereji.

Kipi hukuelewa?
Siyo kwamba sikuelewa ulichoandika toka mwanzo hadi sasa; na ni muhimu nisisitize tena, tatizo ni hii 'mentality' mbovu kabisa uliyonayo, ya kudhani wewe unajuwa zaidi kuliko hao wengine unaowarundika kwenye kundi la waTanzania wasioelewa chochote na kudiriki kuandika upuuzi kama huu hapa:
Watu wanaishi kwa mazoea hawataki kubadilika. Hata umlete malaika hapa kwetu Tz kubadili akili zetu ni ngumu sana.
Kama huwezi kujihoji na kuona upotofu wa maneno ya kipumbavu kabisa kama haya ni lazima utakuwa na matatizo kichwani mwako. Ndio maana niliposoma huo mfano wako wa huyo "sister" nikawa na wasiwasi juu ya tatizo linapoanzia. Tatizo ni wewe, siyo huyo "sister" wako.

Sitaki kuzungushana na wewe kama hutaki kuelewa. Tatizo siyo la waTanzania kukosa ufahamu wa wanachotakiwa kufanya kujikwamua katika hali zao za maisha. Tatizo ni hao watawala wanaolazimisha watawale wakati wakiwa hawana chembe hata ndogo ya kuwaongoza waTanzania ili wajiletee maendeleo yao.

Kwa mtu kama wewe bahati mbaya ukipewa nafasi ya kuongoza, sitegemei lolote la maana utakaloweza kulifanya kubadili chochote katika hali ya maisha ya waTanzania. Sioni tofauti yoyote na hawa watawala waliopo sasa hivi.
 
Wakuu,

Tunapozungumzia maendeleo ya nchi yetu, msingi mkuu wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuwa wazi: nchi inahitaji WATU NA ARDHI ili kujiletea maendeleo. Leo hii, miaka mingi tangu kuanzishwa kwa misingi hiyo, bado tunakabiliwa na kitendawili cha kuwa na rasilimali hizi mbili lakini bado tukategemea chakula na malighafi kutoka nje.

Nimeamua kuandika uzi huu kwa kuangalia kwa kina suala la kilimo, hasa uzalishaji wa ngano, tukizingatia nguvu kazi yetu (watu) na ardhi tuliyonayo.

Tuna Ardhi Kubwa, lakini kwa nini Tunashindwa Kujitosheleza kwa Ngano?

Hebu tuangalie zao la ngano.

Tanzania ina maeneo yenye mazingira yanayofaa kabisa kwa kilimo cha ngano, hususan katika nyanda za juu za kaskazini na kusini. Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Njombe, Mbeya na Rukwa ni miongoni mwa maeneo muhimu yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji.

Hata hivyo, mahitaji ya ngano nchini ni makubwa kuliko uzalishaji wetu wa ndani, na hivyo tunalazimika kuagiza kiasi kikubwa kutoka nje ya nchi.

Kwa mujibu wa takwimu za biashara za kimataifa (World Bank/UN Comtrade) na ripoti za kiuchumi, Tanzania iliagiza ngano na meslin zenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 392.2 mwaka 2024, kiasi kilichofikia takribani tani milioni 1.344. Takwimu hizi kutoka mabenki na taasisi za kifedha zinatupa picha halisi ya fedha nyingi za kigeni zinazotoka nchini kila mwaka kununua zao ambalo lingeweza kulimwa hapa nyumbani na Watanzania wenyewe.

Hoja yetu si kuacha kuagiza ngano mara moja, bali ni kuwa na mkakati thabiti wa kupunguza utegemezi huo kwa kuongeza tija na ushindani wa uzalishaji wa ndani.

Kuangalia mifano ya nchi kama Saudi Arabia na Ukraine kunaweza kutusaidia kuona namna ambavyo rasilimali watu na ardhi zinavyoweza kutumiwa kwa ufanisi au kukabiliwa na changamoto:

Saudi Arabia: Hii ni nchi yenye asilimia kubwa ya jangwa, upungufu mkubwa wa maji, na changamoto za asili katika kilimo. Pamoja na hayo, imewekeza kwa nguvu katika teknolojia, mifumo ya kisasa ya umwagiliaji, na mikakati ya usalama wa chakula ili kulinda uzalishaji wake wa ndani.

Ukraine: Inajulikana kama moja ya vikapu vya chakula duniani (breadbasket). Licha ya changamoto kubwa za kiusalama na vita vilivyoanza mwaka 2022, nchi hiyo imeendelea kuonyesha jinsi sekta ya kilimo ilivyowekewa mifumo madhubuti ya uzalishaji na usafirishaji wa nafaka kimataifa.

Somo kwetu si kwamba nchi hizi hazina changamoto, bali ni kwamba usalama wa chakula ni suala la mkakati wa kitaifa, uwekezaji sahihi, na usimamizi wa rasilimali watu na ardhi.

Swali la msingi ni hili:

Tunawezaje kujenga mfumo utakaotumia kwa ufanisi ardhi yetu na nguvu kazi yetu kupunguza utegemezi huu?

Tatizo sio Ardhi Pekee; ni Tija na Mipango ya Uzalishaji

Mara nyingi tunajivunia kuwa na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo. Lakini kumiliki ardhi si sawa na kuwa na chakula mezani.

Kilimo chenye tija kinahitaji mchanganyiko wa mambo ya msingi yafuatayo:

Mbegu Bora na Pembejeo: Zinazopatikana kwa wakati na kwa bei inayomuduwa na wakulima wadogo na wa kati.

Umwagiliaji na Teknolojia: Kuacha kutegemea mvua pekee na kutumia mashine na zana za kisasa za kilimo ili kuongeza mavuno kwa hekta.

Utafiti na Wataalamu: Kuunganisha taasisi za utafiti na changamoto halisi za mashambani.

Ufadhili na Masoko: Mitaji yenye riba nafuu kwa wakulima na miundombinu ya kuhifadhi na kusafirisha mazao.

Kama tunataka kupunguza uagizaji wa ngano, tunahitaji mpango kazi maalum wa miaka 5 hadi 10 wenye malengo yanayopimika: eneo litakalolimwa, tani zinazotarajiwa kwa hekta, gharama za uzalishaji, na ushirikishwaji wa viwanda vya ndani vya kusaga ngano kununua mazao ya wakulima wa nyumbani.

Wataalamu Wetu na Nguvu Kazi: Tunawatumia Vipi?

Tanzania ina vyuo na taasisi bora zinazozalisha wataalamu wa kilimo, zikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na taasisi mbalimbali za utafiti.
Hata hivyo, kuna pengo kubwa kati ya elimu inayotolewa na mazingira halisi ya uzalishaji:

Wahitimu wengi wa kilimo wanajikuta wakifanya kazi nje ya taaluma zao kutokana na ukosefu wa mifumo inayowezesha kuanzisha biashara za kilimo au kupata ardhi ya uzalishaji kwa urahisi.

Vijana wetu wana nguvu kazi na maarifa, lakini mfumo unashindwa kuwakutanisha na mitaji, ardhi iliyopimwa kwa ajili ya kilimo cha kibiashara, na teknohama za kisasa.

Ukuaji wa uchumi na usalama wa chakula hauwezi kufikiwa ikiwa tutaendelea kulalamika kuhusu ukosefu wa ajira wakati rasilimali yetu kubwa (wataalamu na vijana) haijapewa nyenzo za kuzalisha mali kwenye ardhi yetu.
Kama rais anakaa nyumbani kwa siku zote hizo bila kufanya kazi, tutegemee nini!
 
Changamoto yetu kuu ni moja.

A visionary leader.
 
Nafikiri wewe umehamiwisha mada kutoka kwenye matumizi sahihi ya ardhi ili kujikwamua kiuchumi na kwenda kwenye persal issues.
Hapana.
Kuhusu swala la "sister" wako nilikueleza wazi, hatujui ya upande wake yalivyokuwa. Wewe umetueleza yako, lakini hatujui kwa nini huyo "sister" wako hakuafiki; wewe unataka tuamini tu unachotueleza wewe. Sikukushambulia, nilikueleza.

Mbaya zaidi, ukataka kutumia mfano huo huo wa "sister" wako kuwahusisha waTanzania wengine. Sasa kama huoni upotofu wako hapa unataka nikueleze vipi ili uelewe?

Ndiyo maana imenilazimu nihitimishe kuwa wewe ndiye mwenye matatizo, kwa hii tabia unayoonyesha hata katika mjadala huu rahisi kabisa.
 
Yaani unataka usikie na upande wa pili kuhusu shamba 1 kugeuza kuwa malisho ya ng'ombe ambao tayari wapo?

Are you serious? Kwa taarifa tu ni kwamba tayari nililifikisha wazo kwa wakubwa zangu na tukaafikiana kupanda majani kwenye hilo shamba kwakua nilikua na figure ambayo inaenda vizuri na mradi unaenda vizuri sana.

Nimekupa mfano na sio hukumu. Ng'ombe wa maziwa mnao, mazizi mnayo, ardhi ipo ya kutosha lakini haijapandwa malisho. Usikilize nini upande wa pili wa mtu anayetaka aendelee na kilimo Cha jembe la mkono?
 
Back
Top Bottom