Rais wa kwanza wa Tanzania anawajibika huko aliko kwa maamuzi alochukua kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kisha kutuachia CCM na kudhoofisha mindset za waTanganyika.
Mimi niulize leo kama mTanzania, Mkuu wa Majeshi na Jeshi na TISS wanakaaje kimya kutazama jambo la kuangamiza kama hili likifanyika?
 
Sina uhakika, lakini huu mkataba unaongelea bandari zote nchini, itakuwa hawa jamaa ndo watajenga bagsmoyo port,, maana nimeona wanataja industrial zone,, nijuavyo dar hakuna space ya kuweka hizo vitu
 
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.

Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.

Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?

Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.

Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.

Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.

Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!

Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni

Kutoka kwa Malisa_gj
 
HAPA NDIPO WENGI MTAKUMKUMBUKA HAYATI JPM.
 
Watakuwa wanalambishwa tu asali
 
Mh. Rais, hili ni ombi langu na la watanzania wenzangu walio wengi kwako kwako, tunaimani na wewe na kwakweli tunakupenda.

Tafadhali sana Mama, hebu Jitokeze na uondoe taharuki iliyopo kwenye nyoyo za watanzanua juu ya Bandari ya Dar es salaam.

Kuna hofu na hasira isiyo kifani, ukimya juu ya Jambo hili unaweza kuingiza Taifa kubaya. Vinginevyo nakutakia afya njema na Mwenyezi Mungu akubariki sana.
 
Hawezi jitokeza. Hataki kuonekana anahusika moja kwa moja.

Mkataba ukipita na mambo yakawa mabaya huko mbeleni ataandikwa kama raisi ambaye...(weka maneno mwenyewe)
 
Bandar ipo kwetu ww unanufaika na nini hata ajira zake ni za michongo mimi nao sawa tu ibak kwetu au ichukuliwe poa tu
 
Tatizo kelele nyingi yan wanachowaza itakuaje ajira zao maana wengi ni waajiriwa na sio wafanya kazi ni watu wa kula mshahara tu bila kufanya kazi
 
Sasa si bora wasaini ushoga, ila hii ya bandari kuuzwa?? Mara mia wasaini ushoga uwe halali, kuliko huu mkataba wa kitapeliii.
Nilijua tu Coca na Mariposa lazima wakazie 😂bora upinde
 
kwani sahivi kuna mjombako pale bandarini? Wanakula watanzania wenzako we unapata nini, mbaya zaidi hawana ubunifu wowote. Kubinafsisha uendeshaji ni mfumo wa kidunia utakaoleta ufanisi zaidi.
Uko sawa kabisa atunufaiki na chochote na hii bandari
 
Ukweli mchungu, vikao visivyo na tija, uvivu na umbea kazini ndio wabongo tunaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda aje kikwete huyo hata haelewi alisaini nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…