Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
Rais wa kwanza wa Tanzania anawajibika huko aliko kwa maamuzi alochukua kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kisha kutuachia CCM na kudhoofisha mindset za waTanganyika.
Mimi niulize leo kama mTanzania, Mkuu wa Majeshi na Jeshi na TISS wanakaaje kimya kutazama jambo la kuangamiza kama hili likifanyika?
 
Sina uhakika, lakini huu mkataba unaongelea bandari zote nchini, itakuwa hawa jamaa ndo watajenga bagsmoyo port,, maana nimeona wanataja industrial zone,, nijuavyo dar hakuna space ya kuweka hizo vitu
 
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.

Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.

Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?

Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.

Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.

Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.

Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!

Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni

Kutoka kwa Malisa_gj
 
Rais wa kwanza wa Tanzania anawajibika huko aliko kwa maamuzi alochukua kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kisha kutuachia CCM na kudhoofisha mindset za waTanganyika.
Mimi niulize leo kama mTanzania, Mkuu wa Majeshi na Jeshi na TISS wanakaaje kimya kutazama jambo la kuangamiza kama hili likifanyika?
Watakuwa wanalambishwa tu asali
 
Mh. Rais, hili ni ombi langu na la watanzania wenzangu walio wengi kwako kwako, tunaimani na wewe na kwakweli tunakupenda.

Tafadhali sana Mama, hebu Jitokeze na uondoe taharuki iliyopo kwenye nyoyo za watanzanua juu ya Bandari ya Dar es salaam.

Kuna hofu na hasira isiyo kifani, ukimya juu ya Jambo hili unaweza kuingiza Taifa kubaya. Vinginevyo nakutakia afya njema na Mwenyezi Mungu akubariki sana.
 
Yaani sijui Kuna watu huwa wanafikiria Nini,mtu huna uchungu kabisa na nchi yako urithi wa taifa lako unautoa kihivi kweli,Kwanini tunafikiri pafupi hivi ,akili zetu zimeishia wapi.Ebu tuzinduke hata Kama Ni raia wa kawaida sauti zetu tusipaaze zisiishie kwny minong'ono tuseme ukweli.
Bandar ipo kwetu ww unanufaika na nini hata ajira zake ni za michongo mimi nao sawa tu ibak kwetu au ichukuliwe poa tu
 
Acheni ujima nyie,huko ulaya kwenyewe bandari zinaendeshwa na wawekezaji na sio serikali,hao DP world wanaendesha bandari nyingi tu ulaya yan mje kulalamika kwa iko kibandari chenu uchwara,ngojeni waje hao DP muone kama kuna meli itakaa bandarini siku 3 au wiki kule out anchor kusubiri kuingia bandarini,hao meli ndani masaa tu ishadischarge na kuondoka na nyingine inaingia,acheni upuuzi na ujuha
Tatizo kelele nyingi yan wanachowaza itakuaje ajira zao maana wengi ni waajiriwa na sio wafanya kazi ni watu wa kula mshahara tu bila kufanya kazi
 
Sasa si bora wasaini ushoga, ila hii ya bandari kuuzwa?? Mara mia wasaini ushoga uwe halali, kuliko huu mkataba wa kitapeliii.
Nilijua tu Coca na Mariposa lazima wakazie 😂bora upinde
 
kwani sahivi kuna mjombako pale bandarini? Wanakula watanzania wenzako we unapata nini, mbaya zaidi hawana ubunifu wowote. Kubinafsisha uendeshaji ni mfumo wa kidunia utakaoleta ufanisi zaidi.
Uko sawa kabisa atunufaiki na chochote na hii bandari
 
Watanzania uchapaji kazi ni wa chini mno na kupenda kuridhika plus kufanya kazi kwa mazoea .

Hapo bandari pnatakiwa kazi kazi masaa 24 ila wafanyakazi wenyewe ndo hao mara leo weekend mara mtu ana matatizo ya kifamilia ,yule wa kike kapata dharura mwanae anaumwa mara hivi wapo kweny vikao ,ikifika mda wa kutoka mtu bado kazi zipo ila anaondoka instead ya kunalizia kazi ,kutwa vikao watu hawakai ofisini ,kulindana na wizi kwa vile wote waswahili.

Naona ukiachana na hao wawekezaji wachanganye wafanykazi kama wachina ,wakenya , wahindi na watu kutoka ulaya na America kama sehemu ya wafanyakazi ndo watapata kujifunza jinsi ya kufanya kazi.
Ukweli mchungu, vikao visivyo na tija, uvivu na umbea kazini ndio wabongo tunaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh. Rais, hili ni ombi langu na la watanzania wenzangu walio wengi kwako kwako, tunaimani na wewe na kwakweli tunakupenda.

Tafadhali sana Mama, hebu Jitokeze na uondoe taharuki iliyopo kwenye nyoyo za watanzanua juu ya Bandari ya Dar es salaam.

Kuna hofu na hasira isiyo kifani, ukimya juu ya Jambo hili unaweza kuingiza Taifa kubaya. Vinginevyo nakutakia afya njema na Mwenyezi Mungu akubariki sana.
Labda aje kikwete huyo hata haelewi alisaini nini
 
Back
Top Bottom