Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Tatizo kama hili likitokea Uhamiaji, hivyo suluhisho ni kubinafsisha Uhamiaji?
 
Naona kama tunaenda kinyume na wenzetu.

Nchi za Afrika Magharibi mfano Mali, senegal, Bukinafaso zinakimbiza waizi wa raisilimali zao sisi tunapambana kugawa bandari yetu bure kabisa tena tunaigawa milele na milele hakuna cha time limit wala nini!

Hivi nani katuloga?
 
Hivi Mrusi hatonufaika na chochote pale?
 
Wameshapindua Several times huko kaka

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Afu kuna wapumbavu tupo nao humu jukwaani wanasema eti tumechelewa sana kuwagawia hawa DP kwa kisingizio kwamba eti hazitupi faida! Unakaa unajiuliza hivi watu wa hivi wanawaza kwa kutumia makalio ama?
 
Afu kuna wapumbavu tupo nao humu jukwaani wanasema eti tumechelewa sana kuwagawia hawa DP kwa kisingizio kwamba eti hazitupi faida! Unakaa unajiuliza hivi watu wa hivi wanawaza kwa kutumia makalio ama?
Wewe ndio Mpumbavu kutokukubali madhaifu yako, utaratibu wa Uwekezaji ni wa kawaida Duniani kote, huwezi kuwa huna uwezo wa kufanya jambo kwa ufanisi kisha ikapatikana room ya mtu mwingine kufanya kwa ufanisi kisha nawe ukanufaika halafu wakaza bichwa, Tumeleta makocha kwenye Nation Teams, tuna Contractors kwenye mabarabara, kule Rufiji dam/stiegler's Gorge kuna wa misri, SGR yuko Mturuki hata hapo bandalini alikuwepo TICTS wala hakuna ajabu yoyote, hivi kwanini hoja isiwe ibara au vifungu instead ya huyo unaemdharau DP World International?
 
Sasa kwani kuna sehemu hawa wanaopinga wanasema hawataki uwekezaji? Watu wanachokataa ni baadhi ya terms kwenye ule mkataba. Wanaotetea hawajui hili, wao kwa vile chama Chao kinasapoti basi na wao wanaingia kichwa kichwa bila kuhoji. Sasa upumbavu wangu hapa ni upi kama wewe sio msenge?
 
Msenge baba yako
 
Watanzania wasiwe wavivu wa kusoma. Chukua mkataba, soma vizuri, tafakari,,elewa au omba kueleweshwa alafu amua kutetea upande gani Kati ya wanao support na wanaopinga.
 
Tatizo kubwa ni kuwa haya yoote wanayo yaongelea hayako kwenye mkataba au MoU. Mkataba hautaji wanapewa gati gani, wana"invest" kiasi gani. Mkataba hauna malengo yoyote ya kupima mafanikio au mapungufu. Kilichomo ni ni kuwa TZ haiwezi kuuvunja mkataba hata kama kuna mapungufu au hasara. Maana yake ukiishaingia basi hautoki!
All the best, watanzania tulisubiri kwa muda mrefu sana juhudi kama hizi za kuboresha miundombinu muhimu kwa uchumi wa nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…