Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
Serikali hii iloyopania kuwekwa mfukoni na mabwanyenye wenyeji na mabeberu wa kimataifa wasijaribu kulazimisha suala la uwekezaji bandarini wa Dpworld. Watakua wamewakosea sana watanzania na watawajibishwa muda utakapofika. Pia wataliletea taifa hasara kubwa ya kudaiwa fidia maada mapambano ya kuwatimua hao mabeberu kwa uso wa waarabu lazima yataendeshwa hadi kufanikiwa.

Na kama hawa vibaraka wanabisha kwamba wananchi hawapingi huu uwekezaji waitishe kura ya maoni huru waone jinsi wananchi wanapinga. Haiwezekani eti baada ya miaka 60 ya uhuru na uwekezaji mkubwa wa umma kwenye bandari zetu na miundombinu yake eti tuwaite wageni kuvuna faida.

Hata hao dp tunaoambiwa kwamba watawekeza ni uhuni tu kwa sababu tayari kuna mkopo kwa serikali kwa ajili ya kuimarisha huduma za bandari. Ni wizi na dhuluma tupu inakwenda kufanyika kwa ushirika na vigogo waliyohongwa.
 
Tuendelee kukomalia mkataba mbovu na kudai haki zetu. Katiba mpya ni muhimu sana ili kuondokana na ushenzi mwingi nchini.
 
Jana niliandika kwa kirefu sana na nikisema DPW DEAL IS NOT REAL. Nikasema ni watanzania wenzetu wanataka kujimilikisha Bandari. Naomba kufafanua zaidi tuelewane.

Mkataba unatambua kuwepo kwa DPW itakayoanzishwa Tanzania as DPW Tanzania na itakuwa na affiliated companies na subsidiary companies kama project companies na hata individuals kama equity au wenye share kwa lugha rahisi. Lakini pia mkataba unasema DPW na zile affiliated entities, to mean affiliated companies and subsidiary companies na individuals kama investors. Na kwamba, affiliated entities watatambuliwa na mkataba huu sawa sawa na DPW atakavyotambuliwa. Yaani watapewa same treatment kama DPW.

Na kwamba, kwenye Ibara ya 4, kifungu kidogo cha 5 kinasema DPW na affiliates watakuwa na jukumu la kutafuta fedha na kufund miradi watakayokuwa wamepewakuitekeleza. This means, DPW atakaesajiliwa hapa hatafund miradi yote, atafund ile atakayokuwa anaendesha yeye. Zile affiliates na subsidiaries nazo zitalazimika kufund miradi zitakayokuwa zinaendesha. Na remember, affiliates kimsingi huwa huwa zina share kubwa kuliko parent companies. This means, DPW anaweza pia kutumia affiliated companies, yeye akawa na hisa tu. Simjuwi mnanielewa?

Kwa msingi huo, tutakuwa na kampuni nyingi za akina Rostam Azizi na wengine wengi watafungua kama alivyofanya Mkapa kwenye Meremeta. Kutakuwa na wanasiasa na viongozi wa Serikali kupitia migongo ya watu wengine watakuwa na share zao kwenye hayo makampuni.

Hii inamaanisha Bandari itakuwa inaendeshwa na makampuni ya wazawa, na hata lile kampuni litasajiliwa kama DPW Tanzania laweza kuwa jina tu kama ilivyo coca cola, Pepsi, KFC, Shelaton, na mengine mengi lkn wamiliki wake ni wabongo. Ndiyo maana viongozi wasema nchi haijauzwa, tuwaamini. Ni kweli haijauzwa kwa kuwa itakuwa ni wabongo wenyewe wanaendesha Bandari.

Sasa kwa nini IGA? Jibu ni rahisi. Ili kulinda investment zao. Siku tukigundua huo mchezo, tukaamua kuwafukuza na kutaifisha mali, mahakama ya Kimataifa itawaokoa.

Lakini pia kumbuka kwenye miradi ya phase 1, haihitaji heavy investments kwa kuwa mkopo wa world Bank umeendeleza sana hizo berths zilizotajwa.


Nafikiri sasa mmenielewa.
 
Jana niliandika kwa kirefu sana na nikisema DPW DEAL IS NOT REAL. Nikasema ni watanzania wenzetu wanataka kujimilikisha Bandari. Naomba kufafanua zaidi tuelewane.
a wanasiasa na viongozi wa Serikali kupitia migongo ya watu wengine watakuwa na share zao kwenye hayo makampuni.



Nafikiri sasa mmenielewa.
Wewe ndiyo hujajielewa, you have misconstrued everything. Bandari is critical, but so too is the Airport. Kuna kampuni inaitwa Swissport (Tanzania) PLC inamilikiwa 55% na kampuni ya Swissport AG ya Switzerland, 45% iliyobaki iko mikononi mwa Watanzania kupitia DSE Soko la Hisa. Bodi ina watu 5 three Swiss. Hizo ngonjera zako wala hatuzioni tangu 2012.
 
Wewe ndiyo hujajielewa, you have misconstrued everything. Bandari is critical, but so too is the Airport. Kuna kampuni inaitwa Swissport (Tanzania) PLC inamilikiwa 55% na kampuni ya Swissport AG ya Switzerland, 45% iliyobaki iko mikononi mwa Watanzania kupitia DSE Soko la Hisa. Bodi ina watu 5 three Swiss. Hizo ngonjera zako wala hatuzioni tangu 2012.
What's your point mkuu...?

Zaidi ya hiyo mistari miwili ya mwanzo ambayo umejaribu kugusia alichokiandika, hakuna cha maana ulichoelezea kuonesha kuwa OP alichokiandika sio sahihi.
 
Yaaanii me nashanga...wamegharamiikia kuongeza gati wamenunua na mshine za kisasa (ship to shore gantry crane) na hazijaanza ata kaziii ndo kwanzaaa zinamalizikia installation na wametumia gharama kubwa sana kununua izo mashine mpk walipeleka watu trainning ireland..leo wanabinafsisha kwelii?? dah
Kwa ufupi sisi Watanzania ni wapumbavu, tunajifanya kujua kila kitu wakati hatujui! Serikali imeshasema DP world anapewa sehemu ndogo tu ya bandari ili kutusaidia kupata uelewa mpana wa namna ya kuendesha bandari wakati huo huo sehemu inayobaki itaendeshwa na Serikdli sasa shida iko wapi? Wanasiasa wametujaza hofu sisi Watanzania! Serikali isimsikilize mtu katika hili!
 
Jana kupitia kituo kimoja cha redio kikubwa hapa nchini nilimsikia afsa mmoja kutoka serikalini akielezea kuhusu ukomo wa mkataba wa bandari. Kama nilimuelewa vizuri alisema mkataba utafika kikomo kama terms and conditions zikiwa violated. Jamani wajuzi wa haya mambo mtuelezee huu mkataba ni wa miaka mingapi?


FaizaFoxy
 
Mama samia asishupaze shingo katika swala hilo ni aibu kwa taifa kuwa na mkatba wa kihuni zama hizi za ukweli na uwazi na watu wzlioelimika, serikali mnatoa elimu kwa nani ambaye hajajuwa mapungufu ya mkataba huo! mnatoa elimu kudanganya taifa kwa faida zenu wenyewe sisi tumesema hapana kama serikali ya ccm imechoka basi iachie madaraka ! tanzania tupo milion 65 siamini kama tuna wztu wote wenye akili kama za wabunge wa ccm wanaotumbukiza nchi kwenye janga kubwa kama hilo.


Kuna kipindi nilisema mama hanampango wa kugombea 2025 maana amekamatwa mabega yote kulia na kushoto anaomba mungu amalize salaama 2025
 
Ufutwe haraka !!

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
hatijakataa wawekezaji tunawakaribisha ila maslahi yetu kwanza
 
Sijui itakuaje mana mwaarabu wanataka hela zao,hizi kelele zinawaharibia sifa kibiaahara hivyo wamepanga kuachana na uwekezaji huu.
 
Mama samia asishupaze shingo katika swala hilo ni aibu kwa taifa kuwa na mkatba wa kihuni zama hizi za ukweli na uwazi na watu wzlioelimika, serikali mnatoa elimu kwa nani ambaye hajajuwa mapungufu ya mkataba huo! mnatoa elimu kudanganya taifa kwa faida zenu wenyewe sisi tumesema hapana kama serikali ya ccm imechoka basi iachie madaraka ! tanzania tupo milion 65 siamini kama tuna wztu wote wenye akili kama za wabunge wa ccm wanaotumbukiza nchi kwenye janga kubwa kama hilo.


Kuna kipindi nilisema mama hanampango wa kugombea 2025 maana amekamatwa mabega yote kulia na kushoto anaomba mungu amalize salaama 2025
Safi
 
Back
Top Bottom