Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
La bandari Ni dalili tu. Kuna siku utasikia mkoa wa DSM unakodishwa kwa Waarabu.

Kuna siku tutaamka tutasikia wilaya na vijiji vimeuzwa Oman, na raia watatakiwa kuondoka haraka.

Mama alienda dubai na naambiwa , Sina hakika, kwamba ana vinasaba na Mzee Mwinyi , so Wana vinasaba vya kiarabu.

Walialikwa wabunge 30 kwenda Uarabuni, hatujui agenda ilikua Nini, leo tumejua kilichowapeleka.

Mwinyi aliuza loliondo, leo mnaweka lango la nchi rehani kwa muda usiojulikana.

Wauze tu sababu havina mwenyewe na hata kama yupo amelala.

Nb:Mpango wa Hawa Waarabu na Marekani Ni kuhakikisha bandari ya dar haipanuki zaidi na mpango mahsusi zaidi Ni kuikamata bandari ya dar na kuhakikisha bandari ya Bagamoyo haijengwi.

Kwasababu Bagamoyo ikijengwa maana yake mizigo yote ya Afrika kutoka china 80% haitapita Tena Dubai , Bali itakuja direct to bagamoyo port. Hivyo Dubai itakufa kiuchumi kwa sababu uchumi wake unategemea bandari.

Huu Ni mpango mkakati wa Waarabu na Marekani.
 
Nchi ina maamuzi ya hovyo hovyo kwenye vitu muhimu kabisa bila kushirikisha Wananchi aisee wanakua na haraka kwa mikataba ya muda mrefu mpaka unajiuliza hawa jamaa wana shida gani unaingiaje mkataba mrefu ambao ni wa vizazi na vizazi kwa kukurupuka kwa nini wasisubiri kama Nchi zingine wanavyofanya...
 
Tumekuwa na viongozi wabovu wasio kuwa na fikra ,yaani wanauza nchi asubuhi,kama waarabu wanataka kuwekeza waje tuwape mashamba walime, kwanini wakimbilie kwenye hot cake,waaje waanze chini huku, vijana wakilia ajira tunasema wakalime, waarabu tunawapa bandari hot cake,basi na vijana wasio na ajira tuwabinafsishie bandari waendeshe bandariwasomi wetu yaani wanasiasa wabongo ni HATARI, kesho watabinfsisha nini
 
Wauze tu, wabinafsishe kila kitu

Acha sisi tuendele kufatilia mambo ya simba yanga,singeli udaku wa maisha ya wasanii,betting inatutosha

Ova
 
La bandari Ni dalili tu. Kuna siku utasikia mkoa wa DSM unakodishwa kwa Waarabu.

Kuna siku tutaamka tutasikia wilaya na vijiji vimeuzwa Oman, na raia watatakiwa kuondoka haraka...
Bagamoyo ndio ulikuwa mpango mzima. kikwete yuko wapi aisee awape ushauri hao?
 
Wauze tu,wabinafsishe kila kitu

Acha sisi tuendele kufatilia mambo ya simba yanga,singeli udaku wa maisha ya wasanii,betting inatutosha

Ova
Hapa linatafutwa tukio la kuzima kelele, subiri tu soon utaona.
 
CHONDE CHONDE, TUACHIENI BANDARI YETU, TUACHIENI URITHI WETU, HATUTAKI MUWEKEZAJI nk KWENYE BANDARI YETU
 
Kuna wajinga walisema Mungu kaamua ugomvi, kumbe ni wao wenyewe!

Mungu akiamua ugomvi Taifa haliwezi kuwa na vilio na kuchanganyukiwa namna hii tena!

Ni lini Mungu akusudie kuwapeni furaha kama nchi, matokeo yake mmeanza vilio na kujilaumu?

Njia zenu za kishetani, kikombe hiki ni shariti kukinywea!

Na bado!
 
Kuna wajinga walisema Mungu kaamua ugomvi, kumbe ni wao wenyewe!

Mungu akiamua ugomvi Taifa haliwezi kuwa na vilio na kuchanganyukiwa namna hii tena!

Ni lini Mungu akusudie kuwapeni furaha kama nchi, matokeo yake mmeanza vilio na kujilaumu?

Njia zenu za kishetani, kikombe hiki ni shariti kukinywea!

Na bado!
Ndiyo hivyo
 
Mzuri wa Mpina kaendelea kuwa na misimamo yake ile ile ya kutetea maslahi ya Taifa, mtaji wa mwanasiasa yoyote ni msimamo wake usiotetereka.

Sasa siyo hawa wanasiasa wengine upepo wa kisulisuli ukipiga kidogo tu mambo yote hadharani

Hongera Mpina kuitetea TZ, utahesawabiwa.
 
Hapa inakuwaje jamani naomba elimu juu ya haya maamuzi, najaribu kujiuliza kwamba watu wote nchi hii tumeshindwa kabisa kuendesha bandari, au kwamba tunashindwa kukusanya fedha waje watusaidie? Miaka sitini ya Uhuru hatujaandaa wataalamu wa kusimamia na kuendesha bandari? Usalama was nchi yetu pia ukoje?
 
Back
Top Bottom