Mkuu ni kweli suala la vifurushi Mifumo inatofautiana baina yetu na yao, yote ina advantage zake, ila kusema tunatumia tech za miaka 21 iliopita si sahihi.
1.japo tumerudi nyuma suala zima la mobile network awamu iliopita, ila kabla ya Hapo tulikuwa ni viongozi even kwa level za Dunia, mwaka 2012 Tayari tuna 4g, wakati 4g ni changa, na sio tu tuna 4g Bali tulikuwa na Vifurushi vya Unlimited vya kutosha, mfano smile walishika sana maofisi mengi na 4g unlimited.
2.hatukuishia hapo tuliiupgrade 4g yetu kwenda lte advance, kuanzia Tigo, voda, Halotel etc zote ukawa unapata speed ya maana, na Tigo coverage yao ilifikia Miji yote Tanzania nzima.
3.kwenye 5g tumerudi nyuma, Nchi nyingi Hadi za Africa Nyengine zimetupita na hili linaeleweka.
4. Kuhusu Broadband za majumbani na wifi ni kweli tupo nyuma sana, fiber zinapatikana kwenye majiji makubwa tu, Tena katikati, ukitoka nje kidogo hakuna Access.
Nafkiri hao jamaa walidhani tunatumia Adsl ama dial up connection, tech ya kizamani ya mitandao ya simu,