Jick
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 1,327
- 2,041
Heshima yako yako Mkuu.Mkuu ni kweli suala la vifurushi Mifumo inatofautiana baina yetu na yao, yote ina advantage zake, ila kusema tunatumia tech za miaka 21 iliopita si sahihi.
1.japo tumerudi nyuma suala zima la mobile network awamu iliopita, ila kabla ya Hapo tulikuwa ni viongozi even kwa level za Dunia, mwaka 2012 Tayari tuna 4g, wakati 4g ni changa, na sio tu tuna 4g Bali tulikuwa na Vifurushi vya Unlimited vya kutosha, mfano smile walishika sana maofisi mengi na 4g unlimited.
2.hatukuishia hapo tuliiupgrade 4g yetu kwenda lte advance, kuanzia Tigo, voda, Halotel etc zote ukawa unapata speed ya maana, na Tigo coverage yao ilifikia Miji yote Tanzania nzima.
3.kwenye 5g tumerudi nyuma, Nchi nyingi Hadi za Africa Nyengine zimetupita na hili linaeleweka.
4. Kuhusu Broadband za majumbani na wifi ni kweli tupo nyuma sana, fiber zinapatikana kwenye majiji makubwa tu, Tena katikati, ukitoka nje kidogo hakuna Access.
Nafkiri hao jamaa walidhani tunatumia Adsl ama dial up connection, tech ya kizamani ya mitandao ya simu,
Kwa mara ya kwanza leo naomba nitofautiane na wewe kidogooo kuhusu hizi 3g na 4g.
Binafsi hizi 3g na 4g naona kwa hapa kwetu Tanzania kuna kiini macho kinachochezwa na network providers. Yaani nahisi kuna maeneo hawa voda na nduguze wanaandika 4g lkn in reality ni 3g au wanaandika 3g lkn in reality 2g.
Kwa nini??
Unaweza kuwa mahali(hata katikati ya miji) ukaona ni 3g lkn kunakuwa na ufanisi mdogo sana wa 3g. Kwa mfano unaweza kuwa na 3g lkn hata WhatsApp video calls zinakuwa zinakatakata na quality mbovu. Wakati mwingine hata hiyo 4g inakuwa na ufanisi kidogo sana.
Wakati mwingine unaweza usione tofauti ya 3g na 4g.
Mkuu kama utaweza kutufafanulia hiyo hoja yangu, basi ifafanue kwa lugha nyepesi ili hata Sisi walaji wa kawaida tuelewe.