Leo mchana Ruto anajindaa kwa kile kinacho aminika ni hotuba ya kupunguza baadhi ya mawaziri wake na kuunganisha baadhi ya wizara ili kubana matumizi ya pesa za walipa Kodi wa nchi ya kenya ambao ndio wanaoumia na mzigo mkubwa wa kuendesha Serikali.
======
View attachment 3034286
Kwa Tanzania hali ni tofauti, huku tunahimiza kulipa kodi ambayo sana inatumika kuendesha Serikali hasa hasa kununua Magari ya anasa.
Tuna hadi Naibu waziri mkuu cheo cha mchongo ambacho hakipo kikatba ila kimewekwa kwa sababu za siasa na mzigo tunabeba sisi.
Ukiachana na hayo bado tuna Baraza la Mawaziri kubwa sana na sana limekaa kimchongo sana.
Tanzania tuna Baraza kubwa sana la Mawaziri nazani kiliko hata Kenya ilivyo, na baadhi ya wizara zimekaa kimchongo hazina maana yoyote ile zaidi ya kuongeza mzigo kwa wananchi.
Huku tunahimizwa sana hata na mwigulu tulipe Kodi, Ila tusicho kijua hio kodi inatumika kugharamikia anasa za Watawala wa hili Taifa, huku wananchi wakiendelea kuwa masikini.
Na Watawala hawako tayari kupunguza Mzigo wa Baraza la mawaziri kwa sababu limekaa kisiasa hasa kulipana fadhila.