Tanzania inawezekana? Ruto asitisha ununuzi wa Magari ya Serikali kwa mwaka mzima, Mashirika ya umma 47 yafutwa hayana tija

Mkuu, ili jimbo liwe na haki ya kuwa na Mbunge lina takiwa like na vigezo vipi? katika kuzingatia eneo na idadi ya wananchi ndani ya jimbo husika.
 
MIMI NI MWANA CCM, JAMBO HILI LINAFIKIRISHA! 😈
 
JPM alipofanya hivyo tukasema ni dikiteta! Kwa nini tuwe vigeu gegu?
 
Hajafanya hayo kwa kupenda ,,,huku presha ya wananchi huku presha ya wanaodai mikopo,,,,angekua na hizo akili mapema asingefikia huko, hata ule muswada ulikua kutokana na presha ya madeni japo na wao walitaka wapite humohumo kula,,kwa sasa hana namna lazima apunguze bajet akwepe kufilisika maana deni pia ni kubwa
 
Watu wakiwa madarakani wanalewa madaraka
Hivi mtu kama ana afya ya akili iliyotimamu kweli anaweza toa pesa za serikali kujengea nyumba ma Rais wastaafu halafu na wenyewe wanazipokea bila aibu yoyote ==>Halafu mtu aliefanya ubadhirifu huo watu wanamwita Rais wa Wanyonge

Benefits za wenza wa viongozi wa nchi nazo zimekaaje ?

Magari, Magari Magari Magari. Magari Magari
Hivi Africa tumeambukizana ulimbukeni wa Magari ?
Kila nchi ya Africa unasikia huo ulimbukeni
Hivi Africa kweli ni watu TIMAMU ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…