Tanzania inawezekana? Ruto asitisha ununuzi wa Magari ya Serikali kwa mwaka mzima, Mashirika ya umma 47 yafutwa hayana tija

Kwanza Tanzania sio Nchi iliyofilisika kama Kenya.

Pia Tzn Haina mipango Wala matumizi ya kipumbavu kama Kenya,elewa hilo.
 
Hao ambao wanakosa nafasi hizo wanafanya kazi gani mtaani? Man hiyo ni very weak point
Pale wanaenda wawikilishi kuktatuw matatizo ya wananchi si kukaa bure tu
Hoja nzuri na ndio wanafanya hivyo wanawakikisha matatizo ya wananchi. Wale wa kuchaguliwa huwa hawatoshi maana wao ni ngazi ya jimbo wakati wa kuteuliwa ni wa mkoa mzima labda. Anasemea mkoa mzimaπŸ€”.
Hata wewe ungeteuliwa usinhekataa kuwawakulisha wananchi
 
Kwanza Tanzania sio Nchi iliyofilisika kama Kenya.

Pia Tzn Haina mipango Wala matumizi ya kipumbavu kama Kenya,elewa hilo.
Ni kweli kabisa maana Kenya hawana haya mashangi sijui LC200 Mara ghafla Lc 300 na hiyo ndio weakness yao. Kenya wako weak sana hata kwenye sarafu maana yao ni ndogo sana yaani yetu 20 ni sawa na yao 1 this is weakness.
 
Rais anayeweza kusikiliza Kero za Wananchi akaacha kutumia majeshi na Polisi huku akiwa na Rundo la Siraha na kuamua kuwa Muungwana.

Huyu ndio Rais Bora wa kwanza Afrika.

Haijawahi tokea.
 
Huna haja ya kulaumu viongozi bali jilaumu wewe keboard worier na watanzania wenzako
Unachokiona kenya ni juhudi za wananchi wa kenya na si takwa la viongozi
Viongozi wameshinikizwa
Mambo mazuri hayaji kwa kutaka huruma za viongozi hakuna mwenye huruma na wewe ikibidi hata ufe utakufa tu ili mambo ya watu yaende
Kinachotakiwa ni kupambana
 
Hapa yupo sahihi viongozi wetu ushamba unawasumbua wanapenda sana anasa kila kiongozi akiingia anataka gari jipya wakati nchi zetu zina mambo mengi ya muhimu kwa wananchi kama afya na miundo mbinu huo ni ushamba
 
Mkuu tuanze na ukubwa wa serikali,ni kubwa mno.
Wizara zisizidi 12.

Duplicate ya Shughuli za taasisi , iondolewe.
Ila mashirika ya umma ni muhimu hata kama yanatia hasara,ni kiasi cha kuyaboresha to meet the set requirements.

Bunge ni kubwa mno,tunahitaji kuwa na wabunge wasiozidi idadi za wilaya.
Mchangiaji apate angalau dakika zisizopungua 20 kuweka hoja zake.Kwa sasa ni comedy.

Itolewe mikopo nafuu kwa wajasili mali wa kilimo na viwanda vidogo vidogo ili kuongeza walipa kodi.

School, College, university caliculums ziboleshwa bila kumungunya ili ziende na hali ya uhitaji wa leo,kesho na keshokutwa.

Jeshi la Tanzania liwezeshwe na kuboreshwa mara tatu kama enzi za Mwalimu Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…