Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Wakidundana, tutarajie USA kumpa msaada mkubwa Egypt.
Egypt ndilo taifa la 2 nyuma ya Israeli kupokea misaada kutoka Marekani. Israeli ndio buffer zone, stabilizer katika Mashariki ya Kati. Uhai na ulinzi wa Israeli dhidi ya waarabu unalitegemea Egypt. Hivyo Egypt in silaha na ujuzi wa kufa mtu
 
Mkuu hata kuyasambaza maji ya ziwa Victoria kwenda mwanza, shinyanga, dodoma, tabora pia Ni makosa , tumevunja sheria hiyo ya 1919s, inawezekana siku tukapewa adhabu au kuambiwa acheni Mara moja.
 
Ethiopia Ni wabishi pia tangu enzi za Mfalme Menerik I, nitaifa ambalo halikutawaliwa, nitaifa la wabishi. Ni taifa kakamavu, Ni taifa la kupigana
 
Acha kufananisha mipaka na maji ni upuuzi ulip tukuka yani mto upite kwako usitumie maji eti kisa hayo maji yanaenda kwa jirani yako uwo si ujinga uwo maji tutatumia wote kama utaki nitumie yapitishe angani bac na sio kwenye ardhi yangu...
Malawi walitakaga kuleta huo usenge. Eti Ziwa Nyasa LOTE ni la kwao, kwamba hata upande ambako kuna pwani ya Tanzania ukitaka kupiga mswaki, kuvua au kuoga tu ziwani mpaka uombe kibali Malawi
 
Umeongea neno...!kwa maslahi mapana ya nchi, itabid tuwe upande wa Misri
 
Ethiopia Ni wabishi pia tangu enzi za Mfalme Menerik I, nitaifa ambalo halikutawaliwa, nitaifa la wabishi. Ni taifa kakamavu, Ni taifa la kupigana
watu wanawachukulia Ethiopia simple lkn hawajui kuwa kabla ya kufanya uamuzi wa kujenga bwawa tayari walikuwa wanajua nguvu ya misri ila wakajenga so kuna kitu wanajivunia

na kama miezi miwili iliyopita waliunda kikosi maalumu kwa ajiri ya ulinzi wa hilo bwawa wamechukua battalion nzima na imeanza kupewa bujeti yake
 
Ethiopia sio kama Tz, iko vizuri ni miongoni mwa base kubwa za jeshi la America duniani. Na kwa vita hawajambo kumbuka hawajawahi kutawaliwa na wakokloni
Mkuu katika dunia ya sasa hivi hizo mbwembwe na hadithi za zamani zilisha pitwa na wakati.
Narudia tena kiuhalisia Ethiopia hana ubavu hata kidogo wa kijeshi mbele ya Misri.
Jeshi la Misri ni kati ya jeshi la kisasa na lenye nguvu, mkuu lina silaha za kisasa ambalo Ethiopia ina hitaji miaka mingi kuwa na jeshi la namna hiyo.
Eti Ethiopia sio kama tz? hebu nitajie ni silaa gani aliyo nayo Ethiopia alafu Tz hatuna.
Jeshi la misri lipo kwenye levo za akina Uturuki ,Israel,Iran na sio nchi kama Ethiopia mkuu.
 

Upande wa Mashariki
 
Ethiopia msimbeze kivita yuko vizur sana
Mkuu hakuna anaye ibeza ila unatakiwa kuangalia mazingira ya hiyo vita, misri na Ethiopia hawa jashea mipaka kwa hiyo vita itakuwa ya angani.
Linapo kuja suala la jeshi la angani Ethiopia hana maajabu yeyote mbele ya Misri.
Misiri ni kati nchi yenye jeshi la anga la kisasa na lenye nguvu sana mkuu.
Lakini pia Misri ina meli za kivita kwahiyo ana uwezo pia wa kushambulia kutoka baharini.
Ninacho ona hapa Ethiopia inataka kutujazia wakimbizi tu japa na si kingine.
 
Ethiopia sio kama Tz, iko vizuri ni miongoni mwa base kubwa za jeshi la America duniani. Na kwa vita hawajambo kumbuka hawajawahi kutawaliwa na wakokloni
Mkuu umechanganya madesa. Kwa ukanda ule America ana base Djibout(Africom), labda base ya Ethiopia kaijenga leo baada ya kuanza haya mabishano
 
Ungetoa sababu za msingi za Tanzania kuegamia upande kati ya nchi hizo mbili.
 
Maji yangu unipangie jinsi ya kuyatumia.

Misri wapumbavu sana.

Kama wanashida ya maji wageuze bahari chanzo chao cha maji.

Waache Waethiopia wafanye watakacho. Mto Nile ni baraka ya Mungu. Hatuna mwenye mamlaka na huo mto.
... pia kingine ni wakati muafaka kwa Misri kuwa na proper birth control kuhakikisha population yao ni proportional na resources ya (sio za) maji waliyo nayo - The Nile. Wanajua the only water source waliyo nayo ni hiyo for everything drinking, industrial, irrigation, etc. whatever you name halafu kwa kuzaliana hawajambo; I think third in Africa after Nigeria and Ethiopia. Wawe na mpango wa makusudi wa kudhibiti ongezeko la watu vinginevyo soon itakula kwao hata ya kunywa watayakosa wakifanya mchezo.

Mkuu RTI kasema Ethiopia wasijitoe ufahamu kujipima kifua na Misri ni kweli, Misri wako mbali kijeshi kuliko Ethiopia, lakini hata wakipigwa leo hawatalala nao watakuwa na mpango wa muda wa kati na mrefu 25, 50, 100 years kuja ku-retaliate. Ni kama China, Iran, NK leo wanavyotunishiana misuli na US wakati miaka michache iliyopita walikuwa si lolote.

So, in the long run, millitary approach might not be useful for Egypt, badala yake mipango madhubuti ya kuendana na resources zitakazokuwa zinapatikana by then. Of course hii inahusu nchi zote sio kufyatua fyatua ovyo wakati unajua resources za kulisha na kunywesha watu wako ni finyu.
 
Wakati wanawekeza kwenye huo mradi walijuwa kuwa uko mkataba wa 1919s, lazima sio wajinga kiasi hiko
 
... kwa small scale for home and industrial use that might be possible. Shida ni kwenye irrigation; ku-treat maji ya bahari upate billions of liters per day kumwagilia mashamba tena kwa mazingira kame ya jangwani sio lelemama. Pia utahitaji nguvu kubwa mno kuyapandisha kutoka low altitude (baharini) kwenda high altitude (mashambani) wakati Nile ni "free fall" and fresh by nature; nature ni nature tu Mkuu.
 
Chanzo cha mto Nile kiko Ethiopia lakini hao Wapuuzi wa Misri hawataki Ethiopia ineemeke na neema hiyo. Mie naunga mkono Ethiopia kutumia chanzo cha mto huo vyovyote vile wapendavyo tena wamechelewa sana.

 
Kweli, utu na ubinadamu ndio uwe muongozo. Pia Misri anatakiwa kuacha vitisho akubali kukaa meza ya mazungumzo na Ethiopia.

Wote hao wakumbuke White Nile ndio yenye mchango wa asilia 72 katika kupatikana Great Nile.
... hapo kwenye red; Ethiopia naye mbishi ameombwa mara kadhaa ila kwa kuwa anajua kashika mpini analeta ubishi. Mara kibao ameitwa kwenye meza ya mazungumzo haendi.

... hapo kwenye blue; hapana, mchango wa White Nile unaoanzia L. Victoria ni roughly 15% only; share kubwa ni Blue Nile (Ethiopia) about 85%. Katika jiografia enzi hizo nakumbuka kulikuwa na swali maarufu la "why floods occur in lower Nile (Egypt) in the months of August and September?" Because, rain season in Ethiopia is in June to August so by August and September the Blue Nile waters reach Egypt. Nakumbuka kujibu hili swali kwenye papers ya mchujo FII miaka hiyo! Nashukuru liliniepusha kukariri darasa; haha haha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…