Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Maji yangu unipangie jinsi ya kuyatumia.

Misri wapumbavu sana.

Kama wanashida ya maji wageuze bahari chanzo chao cha maji.

Waache Waethiopia wafanye watakacho. Mto Nile ni baraka ya Mungu. Hatuna mwenye mamlaka na huo mto.
Ni kama UNESCO walivyotaka kutuzuia eti tusijenge bwawa Rufiji kisa urithi wa dunia, haha, hifadhi ni yetu na mto ni wetu, tusipangiane!
 
Ni bora upigwe ijulikane moja, lakini sio kupokwa haki, kwenye uonevu hakuna amani ya kweli, ni kudanganyana tu
Haaa ya kwamba bora uchakae lakini udai haki yako.
Mkuu mbona unaongea kiurahisi sana namna hii?
Hivi unakujua kuchaa?
 
Tatizo wanao takiwa kuidhibiti Misri ndio hao hao walio saini mkataba huo unao ipa haki Misri kuidhibiti huu mto ,nikimaanisha ni nchi za magharibi zenye uwezo wa kuidhibiti Misri.
Hakuna nchi ya kiafrika yenye ubavu wa kuidhibiti Misiri.
Basi nchi zote zenye haki na hayo maji, TZ ikiwemo, ishiriki kuidhibiti Misri
 
Mkuu Tz na nchi nyingine za kiafrika hazina uwezo wa kuisaidia Ethiopia hata kidogo .
Wenye uwezo wa kuibana Misri ni nchi za magharibi ambazo kimsingi wao ndio chanzo cha tatizo kwa sababu ndizo zilisaini mkataba huo unao ipa Misri nguvu ya kuimiliki mto naili.
Mkuu na kuhakikishia iwapo kutatokea vita Ethiopia itapigwa huku viongozi wa kiafrika wakitizama tu hakuna ataye jaribu kubweka.
Bwana limejengwa kwa wahandisi wa China,
 
Huu ugomvi wa maliasili ni mgumu sana.

Huwa nafikiria (theoretically tu) hivi Misri akitutaka tuzuie maji kutoka Victoria yasitiririke kwenda kwake, tutayapeleka wapi? Au tunachimba mto yaende Tanga? Baharini?
 
Katika vita una judge nani atashinda kutokana na uhalisia uliopo kwa wakati huo. Una jeshi la namna gani na liko equiped kiasi gani na utayari lilionao kwa mafunzo. Hivi vyote vinaibeba Misri unapoilinganisha na Ethiopia. Labda kama kuna teknolojia ya haraka na gharama reasonable waliyonayo Ethiopia kubadili yale ma Boeing ya Ethiopia Airlines yawe heavy bombers labda wanaweza kuchukua hata round kwenye ring na Mafarao
Mafarao walikuwa weusi, hao ni wakimbizi toka wanakokujua wenyewe, probably Arabia, tumia akili yako yote
 
Wakidundana, tutarajie USA kumpa msaada mkubwa Egypt.
Pia tegemea Sudan yote, Tanzania, Uganda na wengine wote wenye maslahi na Nile na ambao wanabinywa na huo mkataba prehistoric kuwaunga mkono watoto wa mfalme Solomon na malkia wa Shebba
 
Nadhani wanachokosea Misri ni kutumia vitisho katika hili ila kiubinadam nadhani nchi zinatakiwa kumuelewa maana hamna kitu essential kwa uhai na usalama wa Taifa kama maji. Sasa em fikria Nile ndo chanzo cha maji baridi kwa wananchi wa Misri halafu leo usikie kuna mtu anafanya shughuli zake zinazoweza kuathiri negatively flow ya maji ya mto husika kuja kwako. Utajisikiaje? Ulishawahi kupigwa na jua halafu ukakosa maji ya kunywa! Ndo wanachokihisi wamisri unapoingilia flow ya mto Nile.
Tutangulize utu na ubinadamu kulihukumu hili
Bwawa halijengwi kwenye Nile kuu, linajengwa kwenye tawi dogo ambalo chanzo chake niEthiopia kwenye Ziwa Tana, hivyo hawana hoja
 
Ata akimpatia, hautofikia msaada atakaopata Egypt, kuna UK nae yumo. Egypt ni very important ally wa western sasa ivi ili kuhakikisha usalama pale Israel.
Na kwa upande wa Ethiopia kuna Tanzania, Uganda, Sudan and probably South Africa
 
Hakika,

Hili suala waongee wafikie tamati, either Misri ampatie mchango Ethiopia wa Bwawa na watapatiana umeme au alipe Ethiopia asimamishe na kuchukua umeme kutoka Aswan, Misri.

Yote kwa yote, wasilete vita maana Afrika wakimbizi wanafakiria Tanzania tu.
Labda aipe Ethiopia umeme bure toka Aswan, na anytime akizizingua basi Ethiopia aruhusiwe kujaza bwawa lake
 
Kwani nani aliipangia Tanzania kuwa mmiliki wa mlima Kilimanjaro.
Nani aliipangia Tanzania kumiliki eneo kubwa la maji ya ziwa Victoria na Kenya iwe na eneo dogo, kwanini wasigawane asilimia sawa na Uganda.
Kwanini Rwanda, Burundi nao wasiwe na eneo la ziwa.
Kwanini Uganda wapo landlocked wakati Tanzania ina bandari kama tatu.
Kwanini DRC iwe kubwa sana na yenye mali nyingi wakati Rwanda na Burundi ni ndogo na hazina maliasili.

Hayo maswali na mengine mengi yanafatia kwenye swali lako.
Misri ndo hakujipangia mipaka yake. Waliopanga matumizi ya maji ndio waliopanga mipaka ya Tanzania. Mbona sisi tulipigana na Iddi Amin alipotaka kuibadilisha?
Kenya wakisema Kilimanjaro ni ya kwao utatumia vigezo gani kusema si yao ni ya kwetu. Utatumia vigezo vilevile ambavyo Misri wanatumia, MKATABA. Na nchi zote za Afrika zilikubaliana kuheshimu mikataba ya kugawana milki. Hata sisi Tz na Malawi tunagombea ziwa Nyasa, kitakachofanyika ni kusoma na kutafsiri mkataba unasema ziwa linagawanyika kivipi.
Mlima Kilimanjaro upo ndani ya mipaka ya nchi gani? Ziwa Tana na blue nike ipo ndani ya mipaka ya nchi gani? Jaribu kutumia akili yako yote next time
 
Ethiopia Ni chanzo kikuu Cha maji ya mto Nile, pamoja na Uganda na Tanzania kwa kiasi fulani. Misri na Sudan Ni nchi ambazo zinategemea maji ya mto Nile kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji na viwanda.
Nimeshawahi kuliongea hili siku za nyuma, na hapa narudia kuongea mawazo yangu yale yale yenye elements za Kibeberu, ambayo naamini hata ndugu yangu Kataskopos sometimes huwa anajiuliza "hivi huyu blaza sometimes huwa ankulaga ule mmea?"

The answer is YES, sometimes nakulaga ule mmea, na ndio maana bila aibu wala soni hapa narudia tena kwamba tunatakiwa kumuunga mkono Egypt na sio Ethiopia!!

Sio unamuunga mkono wazi wazi bali tunajifanya ni namna gani Tanzania tulivyo binadamu; na ni namna gani tunatakiwa kutanguliza ubinadamu kwa Egypt ambao hawana chanzo chochote cha maji cha uhakika zaidi ya Mto Nile!

Hapa tunajifanya kulia ni namna gani maisha ya Wamisri yanavyoweza kuvurugika pasipo na Mto Nile wenye maji ya kutosha!!

Kwamba, ujenzi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam utaiathiri sana Blue Nile na hivyo kuleta janga kubwa kwa Egypt inayotegemea tu Nile! Sio tu itaathiri Egypt Livelihood bali pia inaweza kuathiri mazingira!!!

Tukifanya hayo kwa uchungu usiomithirika:-

Dunia itatushangilia kwa "ubinadamu" wetu!

Wanamazingira watatushangilia kwa jinsi tunavyojali mazingira!!

Waarabu na wenyewe watatushangilia kwa jinsi tunavyosimama na Warabu wenzao;

Kumbe:-

Deep inside tunalenga tu kuhujumu ufanisi wa Grand Ethiopian Renaissance Dam!!

How come tuchekelee tu kumuona Ethiopia anajenga mbwawa mkubwa kama ule ambao kimsingi lengo lake ni kutaka kuuza umeme kwa nchi za Afrika Mashariki?!

Kule Lindi na Mtwara kuna gesi ya kumwaga ambayo na tukipata Visionary Leaders, itatuwezesha kuwa wauzaji wakubwa wa nishati ukanda huu wa Afrika!!!

Grand Ethiopian Renaissance Dam ni threat kwa hiyo fursa, kwahiyo mawazo ya kibeberu yanahitajika kuwahujumu Wahabeshi!!

Hapa hapa nilishauri "tuwaunge mkono" ndugu zetu Wakenya baada ya kuzuka taarifa kwamba Wachina wanataka kupokonya Bandari ya Mombasa ili kufidia deni lao!!

Kwamba tupinge uharamia huo wa Uchina wa kutaka kuwanyang'anya ndugu zetu Wakenya Bandari waliyoirithi toka kwa Mababu wa Mababu zao!!!!

Watu hawakunielewa! Hawakunielewa kwa sababu hawawezi kuelewa what would happen kwa Dar es salaam Port endapo Mchina atakuwa ndie operator wa Mombasa Port!!

Na kwahiyo sitashangaa na hapa tena nisipoeleweka kwa sababu si kazi ndogo kuelewa what will happen endapo Ethiopia anakuwa ndie Energy Giant kwenye ukanda huu wa Afrika!!

Energy can be used as a weapon in geopolitics!!

Leo KE anatufungia tu mpaka kwa sababu anaamini hatuwezi kumbabaisha!!

Kinyume chake, hata kama ONLY 10% ya Mombasa and Nairobi Residents depend on energy from Tanzania; hapo KE kabla hawajatufanyia unyang'au wowote watakuwa kwanza wanajiuliza "...lakini na hii mijamaa haitafunga zile valves zinazoleta gas Nairobi and Mombasa?!"

Tuwaunge mkono Misri!

Misri ni ndugu zetu! Ni ndugu zetu kwa sababu ni Waarabu! Waarabu ni ndugu zetu kwa sababu Zanzibar pia kuna Waarabu! Hata huku Tandika pia tunaishi na Waarabu lakini hakuna Mhabeshi hata mmoja!

NIMEMALIZA!!!!
 
Sijakuelewa labda unisahihishe umesema Ethiopia ni chanzo kikuu cha mto nile,kivp wakati tunajua souce kubwa ni ziwa victoria
Nile ina matawi mawili yanayoilisha, kuna dogo linatoka ziwa Tana Ethiopia, ndilo analojenga bwawa
 
Misri katumia ubavu gani kama wameita majadiliano na Ethiopia kagoma kushiriki. Mabavu gani yametumika wakati wanakaribisha mjadala mezani. Kuna mwanajeshi wa Misri kalipua bwawa, au lini wametishia kutumia jeshi.

Kwanza Misri alishabadili msimamo wake kwenye mjadala uliopita. Aliomba maji yajazwe kwa hatua, Ethiopia inataka kuyajaza kwa mkupuo jambo la hovyo kabisa. Pia Misri aliomba maji yasihamishwe mkondo maana yatapungua kwenye channel. Sasa ng'ang'ania alafu watumie jeshi uone Ethiopia anavyokaa asubuhi na mapema. Kwanza hakuna hata ya kupigana direct, kuna kabila la Wahoromo wakipewa silaha wanapigana wenyewe na serikali yao.
Lini Misri ilipangiwa namna ya kujaza Aswan dam?
 
Mkuu hata kuyasambaza maji ya ziwa Victoria kwenda mwanza, shinyanga, dodoma, tabora pia Ni makosa , tumevunja sheria hiyo ya 1919s, inawezekana siku tukapewa adhabu au kuambiwa acheni Mara moja.
Hivi unafahamu kwamba mkataba lazima uwe na time limit as in validity yake katika kuanza na pia kuisha? Leo nikikuletea mkataba uliosainiwa enzi za Yesu au pengine kabla ya Yesu, maybe 150 B.C, utaukubali? Yaani mkataba uliosainiwa miaka 150 kabla Yesu hajazaliwa, utaukubali? Mataifa ya Kiafrika karibu yote and infact nadhani ni yote tumepata uhuru baada ya hiyo 1919, hivyo ni vyema mikataba yote ya nyuma ambayo haimake logical sense tukaijadili na kuitengua, ni kama ule unaosema eti maji ya nyasa yote ni ya Malawi, that is nonsense!!!
 
Hakika Mkuu,

Ikifika wakati wa vita, haitokuwa vita ya Ethiopia na Misri, maana baada ya Ethiopia endapo Jamhuri ya Sudan ikihitaji kujenga Khartoum itazuiliwa, Sudan Kusini kujenga Juba itazuiliwa, Uganda kujenga Jinja itazuiliwa na Tanzania kuendeleza maeneo ya Ziwa Nyanza (Victoria) itazuiliwa.

Misri adhibitiwe mapema, lah sivyo atandelea na mchezo huu kwa yeyote mwenye kuhitaji kufanya maendeleo kutumia Nile.
Akileta ujinga maji yatakuwa poisoned yeye ashambulie na ndege zake tu ila asiyatumie kabisa
 
Back
Top Bottom