Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Tanzania iwe upande gani Kama Ethiopia na Misri zinapigania maji ya mto Nile?

Russia alienda kumsaidia Syria nchi njaa kali hamna mafuta wala nini just kwa kujimwambafai na swagger sababu alijua wa US anatajiingiza
Ethiopian akiongea vizuri na Putin na Xi
Mwarabu atapotezea ishu yote vita
Hapo umekosea kidogo, Russia hakwenda Syria Kama swaga, Bali pale Ni sehemu ya ulinzi wa bomba la gesi yake kwenda ulaya
 
Tanzania iwe upande wa Ethiopia hiyo mikataba aliikataa Nyerere baada ya kupata uhuru kila nchi inabidi kupata maendeleo kwa rasilimali ilizonazo hao misri waliwahi kufunga mfereji wa Suez canal walipogombana na Israel
Hao Egypt "waliudindia" hata mradi mkubwa wa Tz wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria Shy-Tabora-Singida-Dodoma.

Kwa hiyo hao maustadhi ni adui wa kila mwenye interest na maji ya Nile.

Hizi serikali zinatumia pesa kuhakikisha misitu na vyanzo vingine vinavyoleta maji kwenye vyanzo vya Nile haviharibiwi halafu hao jamaa mkitaka kuyatumia wanaibuka na mkataba wa 1919 wa mkoloni.

Upande wetu unajulikana,hata tusiposhiriki.
Mbali na kutoa maji ziwa victoria kwenda mikoa ya Shy na Tbr, tumefuta sharti la kuzuia matumizi ya maji chini ya ardhi bila kibali.

Kwa hili suala hata Idi Amini alimuunga mkono Mwl. Nyerere na kuwapiga mkwara Wamisri, kama wakimletea ujinga anaweka sumu kwenye mto nile.

'KAMA MBWAI NA IWE MBWAI'
 
Wewe inaonekana huzitakii mema nchi zetu yaani uweke sumu kwenye maji kabisa.
Mkuu hapo ndipo tutachakazwa tuchakae kwelikweli.
Yaani nakwambia tutapotea.
Kwahiyo wao kutushambulia kwa manuwari za kivita na mafighter jets unaona ni sawa tu, ila sisi kuwawekea sumu kwenye maji unashtuka?! Haha, kuna nati zinaanza kulegea kwenye Cpu yako
 
Kwani ilo bwawa baada ya kujaa maji si huendelea na mkondo kama kawaida....Nijuavyo mimi kufua umeme hakupunguzi maji bali lile bwawa hutumika kuyashape maji kutengeneza mechanism itakayozalisha umeme.Baada ya maji kutengeneza mechanism iyo maji huendelea na mkondo wake kama kawaida.Naruhusu kukosolewa
 
hii S-3000 bila shaka itakuwa inakava dunia nzima na baadhi ya sayari
Kumpiga mhabeshi misri itamchukua siku tatu tu ashaweka kambi somaliland na jibuti halafu misri wana mfumo wa kuzuia makombora wa thad na S 3000 unategemea nini
 
Kwani huo Ni mkataba au sheria? sheria anadumu hadi hapo itakapotenguliwa. Mfano, Kuna ipo sheria inayokataza baba kumuoa Binti yake, au kuzini au kusengenya. Inadumu tangu enzi na enzi. Leo hii ukimuoa Binti yako au mama yako unafungwa jela
Mto Nile kuwa wa Egypt ni mkataba au sheria?
 
Mzee kwani nuclear haiui kila kitu? Kwani hakuna biological weapons? Mbona sila hizo na zimetumika na hakuna aliyeshitakiwa?: Vita haina macho.
Huyo anaakili za kitumwa, Marekani akitutishia kutupiga bomu la nuclear ambalo linamadhara kwa maelfu na maelfu ya miaka (radioactivity) ataitwa mbabe wa vita, sisi tukitishiq kuweka sumu ya panya mto Nile anashangaa
 
Tanzania haitakiwi kuegemea upande wowote zaidi ijikite kushawishi nchi mbili hizi kufikia makubaliano mazuri namna ya matumizi ya Maji. Wanayogombania. Sema Misri ni watata sana kwenye Suala la kutumia maji ya mto Nile .
Hivi unagombaniaje mali iliyo ndani ya mipaka ya mwenzio, hapo hakuna kugombania, hapo ni kuporana, tofautisha
 
Chonde Chonde Chote. Naomba katika hili tuweke records sawa. TANZANIA SIASA YETU NI YA KUTOKUFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE . Tusije tukaacha reli bali tusimamie nafasi yetu ya upatanishi kwa kuona haki, changamoto na udhaifu wa kila upande ili kusadifu miafaka isiyo hila wala unafiki. HII NDIYO TANZANIA HALISI.
Mwahiyo wakati Ethiopia ananyolewa sisi tuanza kutia maji nywele zetu kusubiri na sisi tunyolewe, si ndio??!!!
 
Kwani ilo bwawa baada ya kujaa maji si huendelea na mkondo kama kawaida....Nijuavyo mimi kufua umeme hakupunguzi maji bali lile bwawa hutumika kuyashape maji kutengeneza mechanism itakayozalisha umeme.Baada ya maji kutengeneza mechanism iyo maji huendelea na mkondo wake kama kawaida.Naruhusu kukosolewa
Hapo ndio uone akili za hao nguruwe wakimbizi wahamiaji wa kiarabu zilivyo mbovu sasa
 
Misri inatumia ile mbinu ya kijeshi ya "jasho jingi kabla ya Vita damu kidogo wakati wa Vita". Inapiga mkwara mwingi ili watu wakae mbali na maji hayo. Inafahamu kabisa kuwa hayo maji yanaweza Kutiwa sumu na maadui zake Kama Vita ya maji hayo itatokea, inafahamu kuwa vyanzo vya mto huo vinaweza kuharibiwa kabisa na maji kupungua Kama vile ilivyopungua barafu ya mlima Kilimanjaro, inafahamu kuwa hakuna taifa linaweza kufa kiu huku wakiyaangalia maji yanaelekea Egypt.
 
Tuwe waangalifu tunapoikataa mikataba iliyowekwa na wakoloni wakati ukoloni. Mkataba uliowapa Misri haki ya kwanza kwenye utumiaji wa maji ya mto Nile uliwekwa wakati wa ukoloni na wakoloni kwa manufaa ya wakoloni, sawa na mipaka ya nchi zetu iliyoko Sasa.

Je, nchi zetu ziko tayari kuachana na mipaka ya wakoloni ili tuligawe upya Bara la Africa? Iko nchi itakubali kuwa mipaka ya wakoloni haifai tuanze upya. Hata Misri kwenye hili inawezekana kuwa Ina hoja
duuh hii mbona inaweza ikawa Vita mbaya mbaya saaana hii!!

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
utata upo hapo jinsi ya kulijaza hilo bwawa Ethiopia wanataka kulijaza kwa mkupuo yaani wachepusha maji mpaka bwawa lao lijae na ili hilo bwawa lijae linaweza kutumia miezi 6 mpaka mwaka 1

misri yeye anataka lijazwe kwa awamu kwamba maji kidogo yaelekezwe kwenye bwawa alafu mengi yaendelee to misri hii njia anayopendekeza misri itatumia miaka 3 au 5

all in all hawawezi kuingia vitani nadhani Ethiopia anatafuta tu kupewa offer nzuri na wamisri
Kwani ilo bwawa baada ya kujaa maji si huendelea na mkondo kama kawaida....Nijuavyo mimi kufua umeme hakupunguzi maji bali lile bwawa hutumika kuyashape maji kutengeneza mechanism itakayozalisha umeme.Baada ya maji kutengeneza mechanism iyo maji huendelea na mkondo wake kama kawaida.Naruhusu kukosolewa
 
utata upo hapo jinsi ya kulijaza hilo bwawa Ethiopia wanataka kulijaza kwa mkupuo yaani wachepusha maji mpaka bwawa lao lijae na ili hilo bwawa lijae linaweza kutumia miezi 6 mpaka mwaka 1

misri yeye anataka lijazwe kwa awamu kwamba maji kidogo yaelekezwe kwenye bwawa alafu mengi yaendelee to misri hii njia anayopendekeza misri itatumia miaka 3 au 5

all in all hawawezi kuingia vitani nadhani Ethiopia anatafuta tu kupewa offer nzuri na wamisri
Alaaa basi nikisanga hapo kwenye ujazaji
 
Mwahiyo wakati Ethiopia ananyolewa sisi tuanza kutia maji nywele zetu kusubiri na sisi tunyolewe, si ndio??!!!

Kutokuwa upande wowote hakumaanishi kupanga msururu. Ni fursa nzuri ya kusimamia uratibu wa kinachobishaniwa ili kuleta mtangamano sahihi wa haki kwa siyo pande zinazobishana tu, lakini pia na pande zingine zenye maslahi katika suala la aina ile ama lile lile.

Nilivyoelewa mimi, kama niko nje, nisahihishwe, Maana ya methali kwamba "mwenzio akinyolewa nywele zako tia maji", haina maana kwamba usubiri ujiandae kunyolewa. Bali ni tia maji kichwani ili usinyolewe!. Au vipi?
 
Sasa kama Egypt ni nchi ndogo sana duniani na ni kubwa Afrika, Ethiopia iko Asia?

Then Anwar Sadat hakuuwawa na wananchi wenye hasira kali. Au unamaanisha wananchi wa Misri wanaruhusiwa kumiliki assaurt rifles tena kwenye sherehe za kitaifa.
Mi sijazungumzia Ethiopia, mi nilikuwa namjibu mdau kuhusu Egypt na Israel kabla wewe hujaingia

Sadat aliuawa na Waislam waliokasirishwa na mkataba aliouingia na Israel na USA
 
Hata Egypt anafahamu Tanzania ndio taifa lenye nguvu kubwa ya kijeshi katika ukanda huu, takwimu wanazo. Hivyo kusaidia ujenzi wa Nyerere hydro sio kwa bahati mbaya. Inawezekana Ni strategy kuelekea Ethiopia. Kihistoria Egypt Ni rafiki yetu zaidi kuliko Ethiopia
Misri hawasaidii, wali apply tender Kama makampuni mengine yalivyo apply wao ndio wakachaguliwa, hakuna msaada pale
 
Russia alienda kumsaidia Syria nchi njaa kali hamna mafuta wala nini just kwa kujimwambafai na swagger sababu alijua wa US anatajiingiza
Ethiopian akiongea vizuri na Putin na Xi
Mwarabu atapotezea ishu yote vita
Nani kakudanganya Syria haina mafuta au haina chochote Cha kuinufaisha Urusi?
 
Chonde Chonde Chote. Naomba katika hili tuweke records sawa. TANZANIA SIASA YETU NI YA KUTOKUFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE . Tusije tukaacha reli bali tusimamie nafasi yetu ya upatanishi kwa kuona haki, changamoto na udhaifu wa kila upande ili kusadifu miafaka isiyo hila wala unafiki. HII NDIYO TANZANIA HALISI.
Kutofungamana na upande wowote ilikuwa Ni with respect to Cold War, West vs East, Tena by defacto ilikuwa East

Kwenye hili la Egypt na Ethiopia sio cold War.
Hakuna nchi ambayo haina upande Duniani
 
Back
Top Bottom