Tanzania Kinara wa Kupokea hela za msaada kutoka USAID Afrika nzima. Yasemekana tutaathirika sana

Tanzania Kinara wa Kupokea hela za msaada kutoka USAID Afrika nzima. Yasemekana tutaathirika sana

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Kisiwa chetu cha Amani chenye Rasilimali nyingi kinapokea misaada ya mabeberu na Mabepari takribani Milioni 512 Kila Mwaka. Imeelezwa.

Gazeti la Euronews limetaja kuwa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zitakazo athirika kutokana na Hatua ya Donald Trump na Elon Musk kusitisha misaada hiyo.

Gazeti hilo limeleza Tanzania yenye watu Milioni 65 linapokea kiwango sawa na Nigeria yenye watu 220Milioni.

Kalagha Bahooo........Hizi hela huwa zinaenda wapi mbona ni nyingi sana?
IMG-20250204-WA0000.jpg
 
Kisiwa chetu cha Amani chenye Rasilimali nyingi kinapokea misaada ya mabeberu na Mabepari takribani Milioni 512 Kila Mwaka. Imeelezwa.

Gazeti la Euronews limetaja kuwa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi zitakazo athirika kutokana na Hatua ya Donald Trump na Elon Musk kusitisha misaada hiyo.

Gazeti hilo limeleza Tanzania yenye watu Milioni 65 linapokea kiwango sawa na Nigeria yenye watu 220Milioni.

Kalagha Bahooo........Hizi hela huwa zinaenda wapi mbona ni nyingi sana?View attachment 3224545
Tanzania tulikuwa tunapata hela za directly kuingia Serikalini wakati wa JK via MCC ila tulishaondolewa pale ndiko tulijenga Barabara,umeme nk

Baada ya hapo ni stori za uongo na ukweli via NGOs which has no significance Kwa Government.

Mwisho hiyo ni Trilioni 1 tuu ,Sasa Tanznaia inashindwaje ku cover hela ndogo kama hiyo?
 
Unaifahamu bascket fund?unafahamu kampeni za chanjo,malaria etc zinatoka wapi?

Kimsingi ccm hawana uwezo wa kuendesha hii nchi bila misaada ya wazungu.
Nazifahamu lakini ni sehemu ndogo ya hela huko.

Mwisho kwani Trump akikata hizo pesa zote,Tutashindwaje Sasa ku cover Trilioni 1 tuu? Hela ndogo sana hiyo Wala haiwezi yumbisha Serikali
 
Tanzania ni mshirika muhimu wa U.S katika ukanda huu wa Afrika. Katika kipindi cha miaka 30 tumetembelewa na "active presidents" wa USA 3 (linganisha na nchi zingine za Afrika katika kipindi hicho).

Orodha ya viongozi wa U.S. (Rais & Makamu) waliowahi kutembelea Tanzania wakiwa madarakani (Chanzo: Mtandao)

1. Richard Nixon – 1969 (President)
2. Bill Clinton – 1998 (President)
3. George W. Bush – 2008 (President)
4. Barack Obama – 2013 (President)
5. Kamala Harris – 2023 (Vice President)

Mwaka jana 2024, PEPFAR iliadhimisha miaka 20 ya mafanikio katika kuisaidia nchi yetu kukabiliana na maradhi ikiwemo TB/HIV (Taarifa za tukio ziko mtandaoni, kasome).
 
Back
Top Bottom