Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na Mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , Mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
Walianzaje?

Learn from them

Don’t hate
 
Maisha hayalingani.

Binadamu wenye akili za kujitegemea Ni wachache.

Kuna baadhi ya watu kwao Maisha ya hayana kipaumbele.

Wanaweza kuwa na matatizo ya maji, ajira, umeme, afya lakini kwa mfano Mbowe anaweza kuwa na yeye ana tatizo lake la Ubunge, Ruzuku au madaraka.

Lakini huyu wa ajira, afya umeme hata ukimpa vitu vyake halafu Mbowe usimpe anachotaka, huyu mtu atakuona Hakuna Cha maana unachofanya.

Ila kama ukimpa Mbowe atakacho then, huyu mtu hata awe na shida Ton 50 atakuwa na Furaha tu.

Na hii ndio mbinu wanaotumia wanasiasa wanaozozana, kukaa pamoja kula ili kusiwe na kelele.

Leo, unaongelea familia ya Mwinyi, Kikwete lakini vyama vyote Tanzania vya siasa viko hivyo.

Penye maslahi hapaingiliki kirahisi.

Hivyo Ni vitega uchumi vya watu..

Psychology!
Hata hakieleweki ulichoandika.
 
Kwetu sisi hata si wavivu kabisa. Tuanaamka assubuhi mapema na jembe. Chai yetu ugali na mlenda ni kazi kwa kwenda mbele. Wanatuita wanyonge. Hatujui suti hatujui tiles na msouth, hatujui mboga tatu, bia haituimudu japo kazi tunapiga.
Hao wanatuambia kilimo ni uti wa mgongo kumbe sisi kinatupinda mgongo.
Siasa imewapaisha angani tukiwatazama kwa mshangao!!!!
Hata umeme na maji ya bomba nyumbani navyo vimekuwa anasa kwa wanyonge!
Poor you.
 
Hata hakieleweki ulichoandika.
Haliwezi kueleweka kwasababu ya "Cult".

Kama ambavyo wafuasi wa Mwinyi na Kikwete hawani tatizo ndivyo hivyo hivyo wafuasi wa Mbowe, Ndesamburo, Lissu, hawawezi kuona tatizo.

Hata sasa hivi Mbowe akimwachia James Mbowe au Dudley Mbowe huwezi Kuna tatizo, sana sana itatafutwa sababu nzito ya kuhalalisha uamuzi huo.

Easy!

Hata Museven, anataka kumwachia mwanue Urais, na wafuasi wake hawaoni tatizo.
 
Kama hupendezwi na anayofanya Mbowe leo CHADEMA si kesho tu unahama chama , unaenda ACT, CCM, TLP n.k kama Hupendezwi na anayofanya Rais au wanaotawala nchi utahama nchi? Hoja yako haiunganiki kwa sababu unalinganisha machungwa na makande.

Ngojea tuendelee kupambana siku moja asubuhi njema itatuwasilia
 
Kila mtu ana haki ya kufuata ndoto zake hakuna dhambi kufuata nyayo za wazazi provided unapanda daraja kwa vigezo sahihi.

Na mtoto wa mwanasiasa yeyote ambae mmbunge ameingia kwa kushindana na wengine kwenye kura za maoni na akashiriki uchaguzi mkuu kwa kushindana na wapinzani, kumsema vibaya it’s just personal hatred.

Shida ni sehemu mbili kuna baadhi ya watoto wa viongozi wachache wanaodhani kuongoza nchi ni haki yao, na baadhi ya wastaafu au wenzawao (sio watoto zao) wasiotosheka mtu kama Salma Kikwete unashida gani ya ubunge si uwaachie na wengine wale.

Watu kama Tibaijuka, Nchimbi, Makinda na wengineo waliokaa bungeni muda mrefu wameachia majimbo wakiwa na uwezo wa kuyatetea kirahisi tu au Regina Lowassa alivyopewa viti maalum na CDM akawaambia hapana hiyo fursa anastahili mtu mwingine; lakini kuna wengine wao awatosheki sio kwamba wana shida na huo mshahara au unaongeza chochote kwenye maisha yake ni tamaa tu.
 
Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na Mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , Mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
Mkuu mbona njia iko wazi kwa kila mtanzania,chukua kadi ya chama uanze kuutafuta uraisi,penye nia pana njia...
 
Umenena vema. Sio hao wahuni wanaona kama kuna mtu anapata wivu.

Kila raia awe na nafasi sawa,ili mradi anaouwezo.

Ikibidi pia kuweka some restrictions ili kuzuia ubebanaji.

Kwa mfano ukiwa rais, walau wanafamilia wako wasipate hizo nafasi za ubunge ama zile za uteuzi kwa kipindi fulani.
Ufumbuzi ni hapa tu mkuu:

"Pigani katiba mpya itakoyotoa fursa kwa yoyote mwenye talents na jitihada"

Mengine yote ni kujilisha upepo tu.
 
Wakati Mstaafu anatengeneza mtandao tangu akiwa chuoni wengine wakawa busy kutenegeza GPA…kila mtu atakula alipopeleka mboga
Mtandao una gharama zake boss....

Rejea ule wa mwaka 2003-2005 ulihusisha wakubwa kutoka pande muhimu kuanzia siasa,utumishi mpaka dini.

Hii mitandao ya kwetu huku chini inatusaidia Sana kutukwamua kwenye hali ya kimaisha tunayopitia huwezi kuifananisha na hiyo ya hao wakubwa.
 
Kama hupendezwi na anayofanya Mbowe leo CHADEMA si kesho tu unahama chama , unaenda ACT, CCM, TLP n.k kama Hupendezwi na anayofanya Rais au wanaotawala nchi utahama nchi? Hoja yako haiunganiki kwa sababu unalinganisha machungwa na makande.
Nawahurumia walimu uliopita mikononi mwao.
 
Back
Top Bottom