Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
Mwenye nacho anaongezewa mkuu.
 
kaka utaambiwa umekuja ki majungu majungu 🙂🙂🙂
 
jiulize pia kwanini Walalahoi wanakubali kuhongwa na kuchagua wahongaji na kuacha kupigia Kira walalahoi wenzao
Walala hoi wanakubali kuhongwa na kuwachagua wahongaji kwa sababu ya kukosa uelewa wa athari za rushwa kwa maisha yao! Ndio maana ccm always capitalizes on the ignorance of the majority of the population for its survival!
 
hawaelewi athari ya Rushwa wakati wa uchaguzi ila baada ya uchaguzi hao hao walalahoi wanalalamika kukithiri kwa Rushwa serikalini?

Tafuta pesa ndugu yangu vinginevyo utakufa na mastress bureee, kuna watu wala huwajui na wana maisha ya ulaya kabisaaaaa , wala hujawahi kuwasikia majina yao wana biashara zao na maisha yanasonga, hata mimi mbeba boksi huku ughaibuni nina maisha mazuri sana sitegemei kuwa chawa wa mtu na mkwanja natumia familia yangu vile vile, ukikaa kufuatilia mambo ya watu utakwama na wao wanaendelea kupeana keki ya taifa kiulainiiii. Ila pole sana
 
hawaelewi athari ya Rushwa wakati wa uchaguzi ila baada ya uchaguzi hao hao walalahoi wanalalamika kukithiri kwa Rushwa serikalini?
The majority of them hawalalamiki because of ignorance but suffer in silence! Wanaolalamika kwa sababu ya njaa waliotengenezewa na mfumo inawabidi washiriki vitendo vya rushwa japokuwa wanazijua athari zake!
 
Maisha hayalingani.

Binadamu wenye akili za kujitegemea Ni wachache.

Kuna baadhi ya watu kwao Maisha ya hayana kipaumbele.

Wanaweza kuwa na matatizo ya maji, ajira, umeme, afya lakini kwa mfano Mbowe anaweza kuwa na yeye ana tatizo lake la Ubunge, Ruzuku au madaraka.

Lakini huyu wa ajira, afya umeme hata ukimpa vitu vyake halafu Mbowe usimpe anachotaka, huyu mtu atakuona Hakuna Cha maana unachofanya.

Ila kama ukimpa Mbowe atakacho then, huyu mtu hata awe na shida Ton 50 atakuwa na Furaha tu.

Na hii ndio mbinu wanaotumia wanasiasa wanaozozana, kukaa pamoja kula ili kusiwe na kelele.

Leo, unaongelea familia ya Mwinyi, Kikwete lakini vyama vyote Tanzania vya siasa viko hivyo.

Penye maslahi hapaingiliki kirahisi.

Hivyo Ni vitega uchumi vya watu..

Psychology!
Nimekulewa mno[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Ila kwa mida ya kesho mchana, unaweza kupita pale BREAKPOINT FAST FOOD. Kutakuwa na zawadi yako pale.
KATI
Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
KATIBA mpya ndo inaandikwa hivyo, Wananchi wapendekeze MFUMO mzuri wa kupata VIONGOZI ktk Ngazi mbalimbali za uongozi.

Watengenezwe viongozi Kwa ELIMU Bora mashuleni, Pia viongozi waliozaliwa na KARAMA hizo wapewe usaidizi kufika DESTINY zao, MARUFUKU uongozi wa MBELEKO ktk Nchi yangu nzuri TZ. Amen
 
dunia haijawahi kuwa na usawa mbona wengine wafupi, wengine warefu, wengine maskini wengine matajiri, wengine madem wengine mameni, wengine weusi kama lami wengine weupe peee, wengine wamejazia wanatingishika wengine wamepigwa pasi wengine wanaimba wengine wananengua, wengine vilaza na vichaa wengine vichwa, wengine wachawi wengine waganga , wengine wanatufurahisha wananchi kwa kufunga magoli mengi na kutetema (Mayele) wengine butu (Boko na Kagere ).

Mbona boss hulalamiki bongo kuna koo za vilaza na koo za wasomi na kuna koo za matajiri na koo za maskini huo ni mjadala mpyaaaa! !

Ukiona nchi inaendeshwa kifalme raia wamekubali otherwise CDM anzisheni mijadala kupinga na mgombee nafasi pamoja na wao msiwaachie fursa na kubaki kulalamika!

KATIBA mpya kiukweli ni suluhisho mkuu sasa wewe imekugusa zaidi ya wengine endesha kampeni ya kudai katiba mpya haraka maana ukikaa kimya wanaokula bata wanajua umekubali mfumo na watajikita kuzidi kunyonya nchi yako sasa akitoka babu anakuja baba, mtoto kisha mjukuu kitukuu kilembwe na kilembweni bila kusahau binamu, mawifi, baba mkwe na mama mkwe, shemeji, shangazi na mjomba wote ni kula kuku kwa mrija tu!!

kama mkuu huna hasira na unataka zikujae na upasuke nenda nyumba wanapoishi hao wafalme wa bongo utashangaa kuona VX zilizojaa uwani na zote zina madereva wamekaa tu na pia kuna wapishi wanaume kibao na kuna walinzi askari sasa mkuu uwe mtulivu usiulize wote hao wanalipwa na nani na wako viongozi wangapi nchini waliojaziwa vibarua hao majumbani!!

tafuta hela mkuu!!
 
Back
Top Bottom