Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Mkuu...mimi sisemi kwa ubaya...Napenda sana shirika letu li perform

Lakini uliza challenge wanazopata mashirika ya ndege siku hizi hapa Tanzania

Ni kwamba watu hakuna ...wanaowezesha wao kufanya biashara endelevu especially kwa Safari za ndani
Mkuu naelewa husemi kwa ubaya ,ila naamini pia hakuna kinachoshindikana ,kila biashara ina changamoto zake na ukiona mtu au taasisi wameamua kuifanya basi risk assessment pia watakua wamefanya ,Ukweli baishara ya ndege ni pasua kichwa nilimwonea huruma Shirima alipotaka kuiweka precision (PW) kwenye mufulisi kisa KQ waliingia nae ubia unao muumiza na sijui hili limeishia wapi
 
Hivi hii ID inatumiwa na watu wangapi?? Maana kwenye utaalamu wa kiswahili upo, uchumi na biashara upo, utabibu upo, siasa na utawala upo, jeshi na ulinzi upo, ukabila upo, ubaguzi wa rangi upo.. Mnaitumia wangapi au we ni mtaalamu wa kila kitu
 
Huwezi amini moja ya route ambayo Air Tanzania ilikuwa inapata pesa sana enzi hizo ni route ya Dar-Mtwara... Sasa hivi barabara ziko safi nchi nzima wapanda ndege wamepungua sana..
Hata kwa sasa kuna Route kama Dar Mwanza Kigoma lakini labda mara mbili kwa wiki

Ya mtwara ni Potential hadi sasa kwa sababu ya mambo ya Gesi...Makampuni ya gesi yana wafanyakazi wengi huko ambao pia wana ofisi dar
 
Barabara zilikuwa mbovu kwahiyo watu ambao walikuwa na kipato kidogo waliopt kusafiri kwa ndege kwa kujibana hivyo hivyo.. Sasa hivi barabara zinapitika nchi nzima kwahiyo kama sio safari ya haraka mtu anaopt kutumia basi au usafiri binafsi
Kama tatizo ni barabara mkuu nadhani Heathrow ,au LAX zingekua zimeshafungwa siku nyingi mkuu ,nadhani kwa usafiri wa usalama zaidi ni ndege kuliko vitu vyombo vingine vyote
 
Hela ya ESCOROW peke yake tungekua na Boeing mbili 767-300ER basi tu ,priority zetu tumeweka kwenye tumbo tu
Matokeo yake kampuni inatarajia kununua videge vidogoo visivyo na uwezo wa kubeba japo abiria 100
 

Mkuu, umesema sawa hii ni biashara isiyotaka mchezo; ina "margin of error" finyu sana. LAKINI kuiweza ni mikakati na utendaji makini tu.

K.m. Ethiopia ni nchi masikini kuliko yetu lakini shirika lao linaongoza kwa kupata faida Afrika. Soko wanalotegemea ni Afrika nzima. Wametengeneza mtandao mkubwa unaounganisha majiji makubwa duniani na majiji mengi ya Afrika kupitia Addis Ababa kama kiungo kikuu "transit hub".

Ingekuwa kutegemea soko la ndani naamini hata sisi tuko njema zaidi; tuna watu wengi zaidi wenye uwezo wa kusafiri kwa ndege. Lakini huwezi kuendesha biashara hii kwa kutegemea soko la nchi yako tu ukafanikiwa. Mashirika makubwa duniani yanahangaika kujijenga kwenye masoko ya nchi nyingi iwezekanavyo. Ni kama bandari. Ni transit traffic ya nchi nyingi za jirani ndiyo huwezesha mafanikio ya biashara hiyo.
 


Air Tanzania haiwezi kushindana na FastJet hata iweje kwa maana FastJet ni shirika la Ulaya na wana Cash kubwa sana, inamilikiwa na mabilionea wa Ulaya, hivyo kuna mambo ambayo tunaweza kufanya ili ndege yetu isimame aidha kwenye upendeleo wa kodi au hata kuwalazimisha kushare njia lkn kama soko likiachwa huria Air Tanzania haiwezi kusimama mbele ya Fastjet hata iweje!

Hivyo ni lazima hatua za makusudi zichukuliwe na hili sio geni kwa mfano huwezi kuwekeza Uchina bila ya kuingia ubia na Kampuni ya kizawa, sasa ni kwa nini wanafanya hivi? Ni kwa sababu wanataka kulinda vyao visimalizwe na Ushindani ktk nje ya nchi, Ulaya na Marekani hufanya hivi pia kwa namna yao!

Hivyo ili ATC isimame ni lazima tuipiganie na hii ni pmj na kuondoa au kupunguza ushindani wa Kigeni!
 

Lets hope for the best

Shirima walimuingiza mkenge ili KQ waweze ku I manage competition toka PW....hadi sasa wana struggle...All they do ni ku repay loans....wana ripoti losses....
 

I partly agree with you...Huwezi kuacha huria iwe huria
 
Matokeo yake kampuni inatarajia kununua videge vidogoo visivyo na uwezo wa kubeba japo abiria 100
Yaani mimi sijui ni nini Mungu katunyima ,hivi hiyo migodi ya dhahabu peke yake ingekua umewekwa mpango kwa mfano mapato yake yatumike kwenye uchukuzi na barabara peke yake ,tungekua na ndege ngapi mpaka sasa hivi ??? Badala yake tunamwachia Bush achimbe na udongo asafirishe ,
 
Tunatatakiwa tufanye study ya kitaalamu ya kutosha kabla ya kuanza hiyo biashara kujua kama mradi utalipa, siyo kukurupuka tu kama tulivyofanya mabasi ya kasi, mpaka leo watu wanashindana nauli iwe ngapi, kitu ambavyo kilitakiwa kijulikana hata kabla ya kuanzisha mradi, ili wajue kama utalipa.
 
Yani jamani tuna matatizo makubwa mnooo. Sijui ni kutojiamini au ni vipi mi hata sielewi
 
Lets hope for the best

Shirima walimuingiza mkenge ili KQ waweze ku I manage competition toka PW....hadi sasa wana struggle...All they do ni ku repay loans....wana ripoti losses....
Mara ya mwisho naskia waliomba serikali iwa bailout sijui kama kuna walichofanya serikali yetu hii
Na hela yenyewe ilikua nadhani 20M usd
 

Mkuu,

You have a very valid concern Drifter

Ethipian airways wana ndege ngapi? kwetu sisi ni kwamba tunaanza...na kwenye kuanza usitegemee sana ku beat international market kwa haraka...You need sometime....kujenga reputation.....Pamoja na ndege za kutosha.......

Ndio maana ninachokiona ni kwa sisi kuweza kuitumia local market vizuri ku build muscles.....Sijui unatumia criteria gani kusema tuna watu wengi wenye uwezo wa kusafiri kwa ndege...Usitumie Mfano wa Fast Jet kwa sababu wao wanatumia Price penetration strategies kwa sababu mother company ina muscles tayari
 
Mara ya mwisho naskia waliomba serikali iwa bailout sijui kama kuna walichofanya serikali yetu hii
Na hela yenyewe ilikua nadhani 20M usd

Serikali Ilikataa......If I correctly remember this
 
Naheshimu huu mchango wako. Keep it up!
 
Alafu kuna uzi fulani humu nyumbu wamechachamaa wakati Membe alishindwa kurudisha mjusi kutoka Ujerumani! viva Magufuli #HapaKaziTu
 
Yani jamani tuna matatizo makubwa mnooo. Sijui ni kutojiamini au ni vipi mi hata sielewi
Mimi nadhani tumbo ndio linatudanganya sana yaani mtu mmoja anaona ni bora awe na nyumba sabini ,narudia tena 70 tena mafanyakazi wa serikali ,ambazo ukifuatilia sana hela yote hiyo ni ya wizi ,sasa kama huyo mmoja kafanya hivyo ,wakifanya watu 100 ?? Huo mtaji wa serikali kujiendesha utatoa wapi kama kodi imegeuzwa swala la kitoto ,halafu hapo hapo anatokea kiongozi wa serikali anasema Magufuli awaendee vizuri wafanya biashara ,kama unalipa kodi stahiki kuna mtu atakusumbua ?? Kodi ndio kila kitu kwenye serikali yeyote kama hatukusanyi ipasavyo tutaendelea kulia kama Jakaya aliye ulizwa kwanini Tanzania ni maskini akasema hajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…