ILAN RAMON
JF-Expert Member
- Sep 10, 2013
- 9,698
- 4,488
Ndege gani flamingo au Tai?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu naelewa husemi kwa ubaya ,ila naamini pia hakuna kinachoshindikana ,kila biashara ina changamoto zake na ukiona mtu au taasisi wameamua kuifanya basi risk assessment pia watakua wamefanya ,Ukweli baishara ya ndege ni pasua kichwa nilimwonea huruma Shirima alipotaka kuiweka precision (PW) kwenye mufulisi kisa KQ waliingia nae ubia unao muumiza na sijui hili limeishia wapiMkuu...mimi sisemi kwa ubaya...Napenda sana shirika letu li perform
Lakini uliza challenge wanazopata mashirika ya ndege siku hizi hapa Tanzania
Ni kwamba watu hakuna ...wanaowezesha wao kufanya biashara endelevu especially kwa Safari za ndani
Hivi hii ID inatumiwa na watu wangapi?? Maana kwenye utaalamu wa kiswahili upo, uchumi na biashara upo, utabibu upo, siasa na utawala upo, jeshi na ulinzi upo, ukabila upo, ubaguzi wa rangi upo.. Mnaitumia wangapi au we ni mtaalamu wa kila kitu
Kama hilo linapaswa kufanyika ili Shirika letu likuwe na kume basi na iwe hivyo, Dunia nzima wanafanya hivyo!
Hivi unafahamu ni kwa nini Mashirika ya Uarabuni kama Emirates, Qatar &Co. yanashamiri? Unafikiri yanafwata kanuni za kibiashara?
Yanashamiri kwa sababu yanaendeshwa na ruzuku kubwa ktk Serikalini yaani hayajiendeshi jambo ambalo halitakiwa kulingana na taratibu za WTO na ndio maana Umoja wa Ulaya unataka kuwapiga faini hasa kwenye njia zao za Ulaya!
Amka wewe Dunia haiendi hivyo, kila mtu anatetea chake, hata Wazungu wanalinda vyao kuua washindani wageni, unafahamu ni kwanini Mkulima wa Ulaya analipwa fedha na Serikali yake?
Ni kwa sababu aweze kushindana na bidhaa za bei rahisi ktk nje, yaani maziwa kama yalipaswa yauzwe shili 1000 yanauzwa 300 halafu Serikali yao inamlipa shilingi 700 zilizobakai, sasa hii utaiita ni nini?
Hata kwa sasa kuna Route kama Dar Mwanza Kigoma lakini labda mara mbili kwa wikiHuwezi amini moja ya route ambayo Air Tanzania ilikuwa inapata pesa sana enzi hizo ni route ya Dar-Mtwara... Sasa hivi barabara ziko safi nchi nzima wapanda ndege wamepungua sana..
Kama tatizo ni barabara mkuu nadhani Heathrow ,au LAX zingekua zimeshafungwa siku nyingi mkuu ,nadhani kwa usafiri wa usalama zaidi ni ndege kuliko vitu vyombo vingine vyoteBarabara zilikuwa mbovu kwahiyo watu ambao walikuwa na kipato kidogo waliopt kusafiri kwa ndege kwa kujibana hivyo hivyo.. Sasa hivi barabara zinapitika nchi nzima kwahiyo kama sio safari ya haraka mtu anaopt kutumia basi au usafiri binafsi
Matokeo yake kampuni inatarajia kununua videge vidogoo visivyo na uwezo wa kubeba japo abiria 100Hela ya ESCOROW peke yake tungekua na Boeing mbili 767-300ER basi tu ,priority zetu tumeweka kwenye tumbo tu
Jamani jamani...Biashara ya Ndege ni ngumu sana...Hao KQ wenyewe wana survive kwa sababu wana ndege nyingi....Precision wanapumulia mashine
Hii biashara inahitaji watu wengi wenye uchumi wa kati...wanaoweza ku afford....kama economy haina hao watu...usitegemee kusafirisha watu wa nchi za wenzako...........
Je...Tanzania ina hao watu wa kuwezesha shirika letu li survive?
Kuondolewa kwa fast jet sikubaliani na ushauri huu
serikali inafanya kila linalowezekana kumpunguzia mwananchi gharama
za maisha,ni ukweli usiopingika kwamba fastjet imetusaidia sana
hasa wakazi wa kanda ya ziwa na Mbeya kwa kutoza nauli ndogo,
sasa pamoja na uzalendo wa kuipenda nchi yetu,siungi mkono wema wa mshumaa.
tumeona viwanda vya cementi vilivyotutesa kwa kuweka bei juu
na kupiga kelele cement isiletwe kutoka nje
sasa angalia baada ya viwanda kuongezeka mbona bei ya cementi imeshuka
wakati hakuna jambo lililobadilika.ATCL ilete ndege lakini ipate
washindani,La sivyo hakuna haja ya kulifufua shirika hilo kama linaogopa ushindani
ambao unaleta faida kwa mlaji/mtumiaji.
Mkuu naelewa husemi kwa ubaya ,ila naamini pia hakuna kinachoshindikana ,kila biashara ina changamoto zake na ukiona mtu au taasisi wameamua kuifanya basi risk assessment pia watakua wamefanya ,Ukweli baishara ya ndege ni pasua kichwa nilimwonea huruma Shirima alipotaka kuiweka precision (PW) kwenye mufulisi kisa KQ waliingia nae ubia unao muumiza na sijui hili limeishia wapi
Hahaha na kweli ndio maana kina Liyumba kazi ilikua kuhonga vigari vyekundu kwa dada zetuUmesahau...Na kwenye Ngono
Air Tanzania haiwezi kushindana na FastJet hata iweje kwa maana FastJet ni shirika la Ulaya na wana Cash kubwa sana, inamilikiwa na mabilionea wa Ulaya, hivyo kuna mambo ambayo tunaweza kufanya ili ndege yetu isimame aidha kwenye upendeleo wa kodi au hata kuwalazimisha kushare njia lkn kama soko likiachwa huria Air Tanzania haiwezi kusimama mbele ya Fastjet hata iweje!
Hivyo ni lazima hatua za makusudi zichukuliwe na hili sio geni kwa mfano huwezi kuwekeza Uchina bila ya kuingia ubia na Kampuni ya kizawa, sasa ni kwa nini wanafanya hivi? Ni kwa sababu wanataka kulinda vyao visimalizwe na Ushindani ktk nje ya nchi, Ulaya na Marekani hufanya hivi pia kwa namna yao!
Hivyo ili ATC isimame ni lazima tuipiganie na hii ni pmj na kuondoa au kupunguza ushindani wa Kigeni!
Yaani mimi sijui ni nini Mungu katunyima ,hivi hiyo migodi ya dhahabu peke yake ingekua umewekwa mpango kwa mfano mapato yake yatumike kwenye uchukuzi na barabara peke yake ,tungekua na ndege ngapi mpaka sasa hivi ??? Badala yake tunamwachia Bush achimbe na udongo asafirishe ,Matokeo yake kampuni inatarajia kununua videge vidogoo visivyo na uwezo wa kubeba japo abiria 100
Yani jamani tuna matatizo makubwa mnooo. Sijui ni kutojiamini au ni vipi mi hata sielewiYaani mimi sijui ni nini Mungu katunyima ,hivi hiyo migodi ya dhahabu peke yake ingekua umewekwa mpango kwa mfano mapato yake yatumike kwenye uchukuzi na barabara peke yake ,tungekua na ndege ngapi mpaka sasa hivi ??? Badala yake tunamwachia Bush achimbe na udongo asafirishe ,
Mara ya mwisho naskia waliomba serikali iwa bailout sijui kama kuna walichofanya serikali yetu hiiLets hope for the best
Shirima walimuingiza mkenge ili KQ waweze ku I manage competition toka PW....hadi sasa wana struggle...All they do ni ku repay loans....wana ripoti losses....
Mkuu, umesema sawa hii ni biashara isiyotaka mchezo; ina "margin of error" finyu sana. LAKINI kuiweza ni mikakati na utendaji makini tu.
K.m. Ethiopia ni nchi masikini kuliko yetu lakini shirika lao linaongoza kwa kupata faida Afrika. Soko wanalotegemea ni Afrika nzima. Wametengeneza mtandao mkubwa unaounganisha majiji makubwa duniani na majiji mengi ya Afrika kupitia Addis Ababa kama kiungo kikuu cha kupitia "transit hub".
Ingekuwa kutegemea soko la ndani naamini hata sisi tuko njema zaidi; tuna watu wengi zaidi wenye uwezo wa kusafiri kwa ndege. Lakini huwezi kuendesha biashara hii kwa kutegemea soko la nchi yako tu ukafanikiwa. Mashirika makubwa duniani yanahangaika kujijenga kwenye masoko ya nchi nyingi iwezekanavyo. Ni kama bandari. Ni transit traffic ya nchi nyingi za jirani ndiyo huwezesha mafanikio ya biashara hiyo.
Mara ya mwisho naskia waliomba serikali iwa bailout sijui kama kuna walichofanya serikali yetu hii
Na hela yenyewe ilikua nadhani 20M usd
Naheshimu huu mchango wako. Keep it up!Sawa...lakini hilo soko lipo?
Kumbuka Fastjet waliingia kwa Price Penetration strategies....Je Air TZ itatumia strategy ipi?
Pia kumbuka Hio strategy ilikuwa ina work vizuri kwa Fastjet kwa sababu Mother Company iliyopo UK inatengeneza faida hivyo kuweza kuzibeba subsidiaries kama hii ya huku
Economy ina middle income class ya kutosha ku endesha shirika letu....
Ikumbukwe hii ni kati ya Industry ngumu Duniani
Mimi nadhani tumbo ndio linatudanganya sana yaani mtu mmoja anaona ni bora awe na nyumba sabini ,narudia tena 70 tena mafanyakazi wa serikali ,ambazo ukifuatilia sana hela yote hiyo ni ya wizi ,sasa kama huyo mmoja kafanya hivyo ,wakifanya watu 100 ?? Huo mtaji wa serikali kujiendesha utatoa wapi kama kodi imegeuzwa swala la kitoto ,halafu hapo hapo anatokea kiongozi wa serikali anasema Magufuli awaendee vizuri wafanya biashara ,kama unalipa kodi stahiki kuna mtu atakusumbua ?? Kodi ndio kila kitu kwenye serikali yeyote kama hatukusanyi ipasavyo tutaendelea kulia kama Jakaya aliye ulizwa kwanini Tanzania ni maskini akasema hajuiYani jamani tuna matatizo makubwa mnooo. Sijui ni kutojiamini au ni vipi mi hata sielewi