Tanzania kutokuwa na Corona katika taarifa za dunia kumewachengua wazungu

Tanzania kutokuwa na Corona katika taarifa za dunia kumewachengua wazungu

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
678
TANZANIA KUTOKUWA NA CORONA KATIKA TAARIFA ZA JANA ZA DUNIA KUMEWACHENGUA WAZUNGU.

Leo 18:30hrs 16/11/2020

Leo nilizungumza na Wachina waliokatazwa na nchi yao ya China kurudi kwao China kwa sababu huu ni msimu wa baridi China na kama mtakumbuka mwezi huu ndio kicorona kilianza uko China, Wachina hao wapo Kariakoo wanadunda washasahau hata kuvaa barakoa, nao pia wanashangaa kwa nini wenzao China wanakufa, na uko Marekani,

Leo pia nikakutana na Wazungu sita kutoka Poland, Ujerumani, Marekani na Uingereza wazungu waliniuliza hali ilikuwaje mwezi March na April wakati wa corona nikawaambia tulikuwa hivi hivi mnavyotuona.

Wazungu hao wakasema tuliambiwa mngekufa kama kuku barabarani maana Marekani walikuwa wanakufa hadi yakatengenezwa masemitrella pembeni ya barabara mtaani kuweka maiti, nikawaambia maneno yanaumba, sisi Rais wetu John Magufuli alisema Mungu aliyetuumba atatulinda. Sifa na shukrani tunamrudishia Mwenyezi Mungu aliyetulinda hata corona ikatushindwa, wakafurahi wakavua barakoa zao na kuanza kukumbatia wabongo Kariakoo,

Mdada wa kizungu mjamzito wa miezi 3 kutoka Marekani yeye alisema anatamani waendelee kukaa Zanzibar maana kwao ni kufungiwa tu anatamani ajifungulie Tanzania, tatizo Visa yake ni ya wiki mbili tu, God is real here, God has favoured Tanzania, Tanzania is another Israel niliwasikia wakiongea huku wakitafakari sana juu ya Mungu alichowatendea Watanzania.

Ndugu zangu Mungu anaweza, Mungu anajibu Maombi, tulimuomba Mungu atulinde na corona na hakika ametulinfa na leo kila kiumbe duniani kinaishangaa Tanzania, Ndugu zangu imani yetu isiwe tu baada ya Maombi kujibiwa na Mwenyezi Mungu, tuamini kabla, sasa na tuendelee kuamini Mungu anaweza kila kitu kwa kuwa ndiye aliyetuumba.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 
Bwana Pascal Mayalla inasemekana pana mwenzako huku.

Amekamilika kila idara: pambio la kusifu, verified user na hakusahau namba ya simu kwa mawasiliano zaidi.
Naona kwenye huu uzi amesahu kutaja elimu yake kwamba ana bachelor of business Nini, master public nini, na nini . Nimekuona mzee napendekeza jina lake. Ila huyu Mayala umri umeenda
 
Naona maandalizi ya vijana kuja kuwang'oa wazee, yameanza na moto!

Abood 2025, utamng'oa!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
99% ya verified members ni watu wa kusifia tu...

Namba za simu ni za nini sasa kama sio kutaka kutambulika na mamlaka ya teuzi!

Acheni kujikombakomba, mtaumbuliwa kama yule aliyetuma ujumbe "Hongera mheshimiwa Rais,umeapa vizuri"

Hata mkeo atakudharau!
 
mchezaji wa simba mkenya kashindwa kuchezea harambee star, kutokana na kuwa na ugonjwa wa korona aliotoka nao Tanzania
 
C-19 imepaishwa sana. Si kali wala hatari kama tulivyoaminishwa.

Ingalikuwa kweli ni kali na hatari, basi ingejulikana tu.

Watu walio wagonjwa hawawezi kufichika.

Shule zimefunguliwa toka mwezi gani vile?

Kampeni za uchaguzi zilianza mwezi gani vile?
 
This statement is from an empty mind, jitu linalojikomba lichjaguliwe... Rubbish! Talk science, not Magufuli, what was the science behind the current situation we are seeing with regard to corona virus spread/containment.
At any rate ukishakuwa verified user lazima kichwa kiwe hivi

View attachment 1627872
Wewe katika watu ambao ni idiot umewazidi wote. Mwenzako amejenga hoja na kutoa ushuhuda wa wazungu. Kwani unakataa Mungu hajatulinda na Corona? Kwani sisi TZ corona imetusumbua kiasi hicho kama nchi zingine? Jibu kwa hoja siku kumtukana tu mleta mada!!
 
Back
Top Bottom