TANZANIA KUTOKUWA NA CORONA KATIKA TAARIFA ZA JANA ZA DUNIA KUMEWACHENGUA WAZUNGU.
Leo 18:30hrs 16/11/2020
Leo nilizungumza na Wachina waliokatazwa na nchi yao ya China kurudi kwao China kwa sababu huu ni msimu wa baridi China na kama mtakumbuka mwezi huu ndio kicorona kilianza uko China, Wachina hao wapo Kariakoo wanadunda washasahau hata kuvaa barakoa, nao pia wanashangaa kwa nini wenzao China wanakufa, na uko Marekani,
Leo pia nikakutana na Wazungu sita kutoka Poland, Ujerumani, Marekani na Uingereza wazungu waliniuliza hali ilikuwaje mwezi March na April wakati wa corona nikawaambia tulikuwa hivi hivi mnavyotuona.
Wazungu hao wakasema tuliambiwa mngekufa kama kuku barabarani maana Marekani walikuwa wanakufa hadi yakatengenezwa masemitrella pembeni ya barabara mtaani kuweka maiti, nikawaambia maneno yanaumba, sisi Rais wetu John Magufuli alisema Mungu aliyetuumba atatulinda. Sifa na shukrani tunamrudishia Mwenyezi Mungu aliyetulinda hata corona ikatushindwa, wakafurahi wakavua barakoa zao na kuanza kukumbatia wabongo Kariakoo,
Mdada wa kizungu mjamzito wa miezi 3 kutoka Marekani yeye alisema anatamani waendelee kukaa Zanzibar maana kwao ni kufungiwa tu anatamani ajifungulie Tanzania, tatizo Visa yake ni ya wiki mbili tu, God is real here, God has favoured Tanzania, Tanzania is another Israel niliwasikia wakiongea huku wakitafakari sana juu ya Mungu alichowatendea Watanzania.
Ndugu zangu Mungu anaweza, Mungu anajibu Maombi, tulimuomba Mungu atulinde na corona na hakika ametulinfa na leo kila kiumbe duniani kinaishangaa Tanzania, Ndugu zangu imani yetu isiwe tu baada ya Maombi kujibiwa na Mwenyezi Mungu, tuamini kabla, sasa na tuendelee kuamini Mungu anaweza kila kitu kwa kuwa ndiye aliyetuumba.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854