Tanzania kutokuwa na Corona katika taarifa za dunia kumewachengua wazungu

1. Nimezungumza na WACHINA
2. Pia nilikutana na WAZUNGU 6. Kutoka Poland, Ujerumani, Marekani na Uingereza.
3. Namba zangu za Simu ni.......

Nina uhakika hata mamlaka za uteuzi zikisoma bandiko lako watagundua kuwa UMETUNGA TU.
 
Naomba kama Taifa tufanye na maombi ya nchi isiwe na rushwa
 
Vp wewe umeipata au, nauliza tuu?
 
Kwani Zambia,, Congo,, Botswana,, Namibia,, Zimbabwe,, Mozambique,, Somalia ipo Corona
 
Naomba kuelimishwa, hivi tanzania hakuna ugonjwa wa corona au hakuna takwimu za wagonjwa wa corona? Maana kuna tofauti kati ya kutokuwa na mgonjwa/ugonjwa na kutokuwa na yakwimu za ugonjwa
 
Kwani ukimwi upo haupo? We unao? Me kutokuwa nao sio kwamba haupo mkuu...tumia hiyo kichwa vizuri hujapewa kichwa ufugie nywele man!
Comment hii mwenye akili atakuwa kakuelewa.
Huwezi kusema ugonjwa haupo simply kwa sababu hujaugua.

Tuseme CANCER haipo coz mimi na familia yangu hatujaugua...

Everyday is Saturday...😎
 
Weeks 46??
 
Kinga ya mwili ndio imefanya kazi sababu ina experience na magonjwa na mazingira magumu na sio vinginevyo.

Pia huwezi ukasema hawaumwi wakati hukuwapima.
Mwafrika anaweza kuwa anaumwa then anapona mwenyewe bila kujua considering africans sio watu wa kucheck afya.

Pia huwezi ukaona tanzania kwenye hizo taarifa sababu Tanzania yenyewe haitoi taarifa.

Ni vizuri kwa mwafrika kujua kwamba pia wazungu nao ni wajinga sio kama mnavyoaminishwa.
Ni wazungu wachache waliobadilisha mataifa yao na sio wote.

Africans msiwe inferior.
 
Wazungu na mataifa mengine ya Africa wanajichetua tu akili, wanaona aibu kuiga kutoka kwa chuma JPM, kitu kikubwa alichofanya chuma JPM ni kututoa hofu, wazungu kinachowaua sio Corona ni hofu tu. Waachane na ujinga wa kupimana Corona hovyo hovyo waone kama maisha hayataenda.
 
Hata huko ulaya kuna wachezaji mpira wanapata corona kila siku, sio hatari kwao. Inawezekana hata mimi na wewe tumewahi ipata ila hatujijui sababu ni vijana wenye Afya.

Hili halisababishi lakini tusiwe na hofu ya wapendwa wetu, kuna watu wengine pia wana haki ya kuishi, tofauti na Malaria ambayo kila mtu ana chance, kuna makundi fulani ya Watu kwao corona ni asilimia kubwa wanasepa,

Mimi binafsi nimepoteza ndugu kama 6 toka ianze, watano round ya 1 kabla hatujafunga mipaka na mmoja hivi karibuni.
 
Huku tanzania sisi maisha yanaendelea kama kawaida. Hata waliokuwa wanasema wawtanzania wanakufa sana kipindi cha kampeni nao hawakuvaa barakoa baada ya kugundua Corona kweli siyo big issue.
Ni jambo la kushurukuru tu hatuishi wa mashaka.
 
Umeandika vizuri ila kwenye sifa tu zinakotakiwa ziende umekosea, huu ni uchochezi.
 
Corona ni hatari sana ukiikuta iko kwenye nchi ambayo Serikali yake inapaniki paniki. Trump kwa mfano kama angekuwa amepaniki kuhusiana na Corona, Marekani wangekuwa na hali mbaya mno kuliko ilivyo sasa. Kukwepa kupaniki kunasaidia sana kuondoa makali ya Corona. Niliwahi kumsikia Trump siku moja anamfokea mwenzake kwenye debate ya kampeni zao anasema "I do not wear masks like him...." Trump aliidharau sana Corona, mimi namsifu sana katika hilo
 
We are science-oriented people, umeleta ushahidi, very fine. Si kuwa hakuna infection, ni kuwa infection ni very low/low..... Magufuli did nothing to contain the spread, his approach was very dangerous indeed had nature not being on our side! He opted for serendipity/nature to take its course!
Pili, hapa la uchaguzi umekuwa kama wenzako, nilitaka nikuone mtu reasonable, kwa kukiri ukweli kuwa this election was extravagantly rigged. Sasa kama unasema kulikuwa na uchaguzi, basi, siku njema, maana ukiona mtu anasema katika normal mathematics/natural maths kuwa 1+1=3, then huyo usibishane naye....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…