Mkuuuu!! Hapo kwenye wages me nmeshindwa kuelewa kidogo hiyo minimum wage wanayoandika 100,000 au 130,000 kwa mwezi ni mshahara wa MTU kweli kwa nyakati hizi au me ndo sielew
Kila sekta ina kima chake cha chini mkuu kwa mujibu wa Tamko la Serikali la kima cha chini cha mishahara ya kisekta; Tamko Namba 196 la mwaka 2013.
Mfano sekta ya kilimo 100,000
Shule binafsi (nursery, primary na secondary)140,000
Sekta ya afya 132,000
Sekta ya mawasiliano 400,000
Taasisi za fedha 400,000
Mkandarasi daraja la kwanza 325,000
Mkandarasi darala la pili hadi la nne 280,000
Mkandarasi daraja la tano hadi la saba 250,000
Sekta ya biashara (trade, industries and commerce) 100,000
Utangazaji, mass media na courier services 150,000
Wafanyakazi wa ndani walioajiriwa na diplomats na potential businessmen 150,000
Wafanyakaz wa ndani employed by entitled officers 130,000
Wafanyakaz wa ndani wengineo lakini hawalali kwa mwajiri wao 80,000
Wafanyakazi wa ndani wengineo lakini wanalala kwa mwajiri 40,000
Hotel za kitalii na hotel kubwa kubwa 250,000
Medium hotels 150,000
Restaurant, guest house and bars 130,000
Kampuni za ulinzi binafsi za kimataifa na kubwa kubwa 150,000
Kampuni za ulinzi ndogo ndogo za ndani nchini 100,000
Sekta ya nishati kwa makampuni ya kimataifa 400,000
Sekta ya nishati kwa kampuni ndogo ndogo 150,000
Aviation services 300,000
Clearing and forwarding 300,000
Inland Transport 200,000
Kampuni zenye leseni ya uchimbaji na utafutaji wa madini 400,000
Kampuni za madini zenye leseni ya uchimbaji mdogo mdogo (PML) 200,000
Kampuni za madini zenye leseni ya Dealers Licence 300,000
Kampuni za madini zenye Brokers Licence 200,000
Fishing and Marine services 200,000
Sekta nyinginezo ambazo hazijatajwa ktk muongozo/tamko hili 100,000
NB: hizi zilizotajwa hapa ni minimum standards, mwajiri anaruhusiwa kulipa above hiki kilichooneshwa hapa ila haruhusiwi kushuka below hicho kiwango.
Kwa hiyo mpaka pale utakapotolewa muongozo mpya, kwa sasa unaotumika ndio huu.