Kiongozi naomba nichangie kwa kupitia haya maswali yako
1. Masaa ya kufanya kazi kwa juma.
2. Mfanyakazi kufungiwa nje baada ya kuchelewa kufika kazini.
3. Mfanyakazi kupangiwa kazi siku za wikendi.
Tutatumia sheria zifuatazo kujadili ili sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004, kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 na Minimum wage order 2013
sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 15 (1) kinaweka wazi kwamba mkataba unatakiwa kuanisha masaa ya kufanya kazi
sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 19 (2) kinachanganua suala la masaa ya kazi inatakiwa kwa wiki ni siku 6 na masaa 45 kwa wiki yote sasa
Sasa ikitokea muajiri anamtaka mfanyakazi aafanye kazi masaa ya ziada sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 19 (5) anatakiwa kukulipa sio chini ya 1 na nusu ya mshahara wa siku moja kwa masaa ya ziada na pia sio lazima ni makubaliano baina ya pande zote mbili
Mfanyakazi kupangiwa kazi siku za weekend mfano jumamosi na jumapili kwa jumamosi ile nusu siku tunahesabu kama siku ya kawaida ila yakivuka masaa yale ya nusu siku tunaanza kuhesabu kama ni masaa ya ziada na kwa jumapili huwa tunahesabu ni siku nzima kama kama siku ya ziada na huesabiwa masaa 8
cha kuangalia hapo je mmweweka makubaliano ya aina ipi kwenye malipo ila inategemea sana unafanya kazi ya aina gani ila ni vyema kujua iyo kazi je kisheria mshara wake wa kima cha chini sasa hapa unatumia minimum wage oder ya 2013 kujua kima cha chini cha mshara kw a sekta uliyopo
Kilimo 100,000
Afya 132,000
Mawasiliano 400,000
ulinzi kuna 150,000 na 100,000
ujenzi 250,000 mpaka 325,000
mining hapa inategemea lesseni ila ni 200,000 mpaka 400,000
elimu 140,000
sekta ya fedha 400,000
hizo ni baadhi tu itakusaidia kufahamu
Mfanyakazi kufungiwa nje baada ya kuchelewa kufika kazini. kwenye ili wapo sahihi kama tu utaratibu na sheria mlisomewa kwamba ukichelewa baada ya muda fulani wanafunga geti hili wameweka ili kupata urahisi wa mienendo mibaya ya wafanyakazi haswa swala la nidhamu kama KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 inavyohitaji muajiri kukabiliana na muenendo mbaya wa mfanyakzi kwa kuweka taratatibu nasheria na kuhakikisha mfanyakzi anazijua na anazifuata na nini kitatokea zikivunjwa