Wadau naomba kujua sheria ya kazi inasemaje kwasasa hivi kuhusu
1.Notice of termination.
2.severance pay.
Swali lako nitalipa ufafanuzi kama ifuatavyo na wajumbe wengine watachangia pale nitakapopungukiwa
masuala yote ya kazi yanasimamiwa na sheria na kanuni zinazojulikana kama (
SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2004 na KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2007) sasa tuanze kufafanua kwa mujibu wa maswali yako.
Notice of termination.
Kwa kutumia
Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya Mwaka 2004 kifungu cha 41 kinaeleza wazi ni siku 28 ndio pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa za Notice of termination. ikieleza sababu na muda pia kuna masharti ya utoaji wa Notice of termination haiwezekani mtu yupo likizo alafu umpe Notice of termination pia mfanyakazi hutakiwi kukataa kufanya kazi kipindi cha Notice of termination
Lakini katika Notice of termination kwa mfano una mkataba wa muda maalumu Notice of termination itatolewa ikikupa taarifa kwamba hautaongezewa mkataba pindi pale mkataba wako utakapofika mwisho maana yake mkataba wako utakoma wenyewe pale muda utakapofika mwisho hii ni kwa mujibu wa
KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 kifungu cha 4
Notice of termination hutegemea sababu maana yake kuna sababu kama 4 za kupewa Notice of termination na kila sababu inautaratibu wake wa kufatwa 1. Mwenendo mbaya 2. Kutohitajika 3. Kupunguzwa kazini 4. Kutokuwa na uwezo au kukosa uwezo baada ya kuajiriwa hizi sababu zote Notice of termination hutolewa kwa kufatwa taaribu tofauti tofauti sasa hapo inategemea wewe umeangukia wapi
severance pay
Hii kwa kiswahili tunaita kiinua mgongo mahesabu yake huwa ni mshahara wa siku 7 kwa idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika mfano mshahara wako kwa siku ni 10,000 na umekaa kwenye kampuni miaka 2 itakuwa hivi 10,000*7*2=140,000 hivyo kitakachobadilika ni iyo idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika sasa sheria ipoje ili uweze kupata
SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2004 kifungu cha 42 ipo hivi unatakiwa kutumikia angalau miezi 12 kampuni husika, pia usiwe umeachishwa kazi kwa mwenendo mbaya kama Wizi na makosa mengine ya utovu wa nidhamu
Ila unapolipwa kiinua mgongo unatakiwa malipo mengine uwe umeshalipwa bila kupunjwa kama likizo na je kuachishwa kazi kwako kulifatwa taaratibu halali za kisheria
Natumaini hata wengine watakuja kuongeza nilichochangia mimi natanguliza shukrani