KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Hivi huwa vinalinganishwa vitu gani?..Uchumi wa Tz bado ni mdogo kulinganisha na wa Kenya.
- Kodi zinazokusanywa?
- Mauzo yanayofanywa?
- Pato la kila mtu?
- Mali zinazozalishwa na faida inayopatikana kubaki nchini, au kupelekwa nje ya nchi?
-Wingi wa matajiri, au maskini?
Katika vigezo hivyo, kuna uhakika wowote wa usahihi wa takwimu zinazotumika?
Kwa mfano:
Mwaka 2015/16 GDP ya Ethiopia ililipotiwa kuwa imeipita ile ya Kenya kwa mara ya kwanza, na imekuwa hivyo kwa miaka kadhaa hadi mwaka jana, 2019, ambapo inasemekana GDP ya Kenya imepanda zaidi na kuipita ile ya Ethiopia, na kwa hiyo Kenya kuwa kinara tena katika eneo hili la Mashariki kwa kuwa na pato kubwa, nadhani kwa kuwa na GDP ya $99 Billioni, huku ile ya Ethiopia ikibakia kuwa $91 Billion!
Na wakati huo huo, kila mwaka tokea 2015 uchumi wa Ethiopia ukiwa unakuwa kwa wastani wa zaidi ya asili mia 7, na ule wa Kenya haujazidi 5.6?
Hapo ndipo huwa natokwa na maluilui katika uelewa wa haya mambo ya hizi takwimu za uchumi!
Sina tatizo na uelewa wa takwimu, kwa sababu huzitumia mara nyingi sehemu zinazonihusu, lakini hizi za uchumi, naona ndio kiboko yangu.