Salaam.
Wakuu, ukisoma maswala ya Babeli kwenye Biblia Mwanzo 11:1-9, unaambiwa kwamba, "Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale" .
Ukisoma 7 unaambiwa.. "Haya, na tushuke chini na kuivuruga lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” Mwisho wa kunukuu. Nchi yetu sasa hivi tunashuhudia kila Mwenye Cheo anaongea lugha yake.
Ni wakati wa kuombea taifa ili watendaji na wale wenye Mamlaka watende haki katika kutimiza Majukumu yao.
Katika kuleta usawa, tusiangalie huyu ni Sukuma gang mwenzangu, au huyu ni wa kaskazini tumsingizie kuua Viongozi wa Serikali , au Huyu anatokea Nungwi sisi tunatokea Nangurukuru hivyo hatuhusu, au huyu anatupigia kelele tukiwa tunakula Keki ya taifa tumpe kesi ya Ugaidi ili tufaidi nchi kwa raha.
Ni jukumu la kila Mtu kwa nafasi yake kuhakikisha anatenda haki kwa wote. Vyama vya Siasa vipo kuleta Demokrasia sio chuki na Uhasama..
Wafu ambao hawajaacha maandishi, kuwalinda na kuwatetea na kukumbukwa ni ngumu sana. Hata Nyerere anaishi kwa Vitabu vyake.
Nani asimame Nchi ipone?
#Katibampya.
View attachment 1896416