Tanzania: Mihimili mitatu ya Dola na mwingiliano unaokanganya

Tanzania: Mihimili mitatu ya Dola na mwingiliano unaokanganya

Kinadharia, Tanzania ina mihimili mitatu ya utawala, SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA.

Kuanzia awamu ya 5, kimamlaka, mihimili yote mitatu imekufa, umezaliwa mhimili mmoja tu, wa RAIS.

Ndiyo maana unasikia Rais ametoa hela, Rais ameiagiza mahakama, Rais amilikemea bunge.

Ukiona kuna mradi mzuri umejengwa kuwahudumia wananchi, ujue ni Rais.

Ukiona watu wasio na hatia wanapigwa virungu, ujue ni Rais.

Ukiona watu wanafutiwa kesi za kubambikiziwa, uje ni Rais.

Ukiona watu wanabambikiziwa kesi na kusoteshwa mahabusu, ujue ni Rais.

Ukiona viongozi wakubwa au wanafungwe au kusoteshwa mahabusu, ujue ni Rais.

Uhuru wa mahakama umeachwa kwa wezi wa kuku, vitunguu na nyanya.

Uhuru wa Bunge, umeachwa katika kuipongeza Serikali tu!

Rais aliagiza akina Rugemarila, wakae ndani, wakaa ndani. Rais mwinhine akaagiza akina Rugemarilla watolewe, wakatolewa. Kama tungekuwa na mahakama, Rugemarilla na wenzake ama wasingesoteshwa mahabusu, au kama wangekuwa wana kesi, basi wasingetolewa kwa vile tu Rais amebadilika.

Kwa sasa hakuna linalofanyika, liwe jema au baya, bila hiari ya Rais. Na juzi jaji mkuu akakazia kuwa majaji wanapotoa hukumu wasiangalie tu sheria inasema nini bali waangalie pia mahitaji ya mihimili mingine, na kwa vile mihimili yote practically imekufa, alimaanisha majaji waangalie Rais anataka nini.

Mbowe atafungwa au kuachiwa, kutegemea Rais, kama mhimili, atataka nini. Majaji na mahakimu wamekuwa visemeo tu vya mhimili mpya, wa RAIS.

Taifa lipo kwenye hali ngumu sana kwa sababu lipo kwenye maamuzi ya mtu mmoja ambaye kikatiba wala siyo miongoni mwa ile mihimili mitatu, yeye ni kiongozi tu wa mhimili mmoja.

Tupiganie tupate katiba mpya au tuishi kama mbwa au paka anayependwa au kuchukiwa na bwana wake.
 
Ukweli wa kusikitisha, ni kweli yalishafanyika mengi mabaya ila lile la jana ndio limepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la haki nchini.

Sitaki kuamini mateso yote waliyopata watuhumiwa, maumivu, na makovu waliyosababishiwa na watesi wao, ukiukwaji wa sheria wa makusudi.

Lakini pamoja na yote bado jaji Siyani akaona vyote ni ujinga na kuipotezea mahakama muda wake kama asante yake kwa cheo alichopewa katikati ya kesi.

Hili linaonesha sasa kama taifa tunahitaji kuamka kwa pamoja, tusitegeane na kunyoosha vidole kwa taasisi moja kama vile hiyo taasisi pekee ndio ina majibu ya kudumu ya shida zetu, na kama tukizidi kuchelewa, tujiandae kwa maumivu makubwa yatakayokuja siku za mbeleni miongoni mwetu.
 
Mkuu, hivi hizo hoja ni ujinga mtupu!!?? Hata kama kila mtu ana haki ya maoni lakini kwa hoja hizo ni bora ungepita kimya kuliko kusema ujinga mtupu...

Hamatan
Hoja za aina hii zilitakiwa zianze wakati wa hukumu ya Sabaya afu ndo wangemalizia katika hii hukumu ya Mbowe. Ila isiwe ile ya kunya anye kuku afu kwa bata ionekane kaharisha.
 
Serikali (excecutive) imepora mamlaka ya Mahakama na Bunge, Taifa limekosa check & balance... muhimuli mmoja ndiyo unafanya overall rulling ya nchi.
Rais amegawa cheo kwa Jaji (Transitional promotion) katikati ya shauri kwa tafsiri ni kwamba limeathiri mwenendo mzima wa kesi zima.
 
Hoja za aina hii zilitakiwa zianze wakati wa hukumu ya Sabaya afu ndo wangemalizia katika hii hukumu ya Mbowe. Ila isiwe ile ya kunya anye kuku afu kwa bata ionekane kaharisha.
Sabaya mwenyewe alikiri kutenda makosa aliyoshtakiwa nayo akijitetea kwamba alitumwa.Sasa mtu aliyekiri kutenda makosa unaanzaje kumtetea?

Yaani wewe ukiri umeiba halafu sisi wapambe wako tuanze kukanusha hukuiba.Si tutaonekana vichaa!
 
Hoja za aina hii zilitakiwa zianze wakati wa hukumu ya Sabaya afu ndo wangemalizia katika hii hukumu ya Mbowe. Ila isiwe ile ya kunya anye kuku afu kwa bata ionekane kaharisha.
Hata hukumu ya Sabaya, imetolewa kwa maagizo, ndiyo TiSS maana akapewa nafasi ya kuhukumu. Kutokana na maelezo ya wengi, na kauli yake mwenyewe, Sabaya ni mhalifu, lakini shauri lake lilistahili kupita kwenye mfumo huru wa mahakama, si kama alivyotendewa.
 
Kenge kweli, kumbe unavyomuita Mbowe gaidi unakuwa msukule wa nani? Sabaya!
Acha ungese wee shoga au unataka niweke picha zako zaidi ya hii ambazo zinaonesha dhahiri ukiwa umepakatwa? Ni wapi nilipoandika mbowe gaidi? Au lile tobo la uchafu linawasha pimbi wee. Siku nyingine uwe unasoma vizur kabla ya kujibu.

images (39).jpeg
 
Ukweli wa kusikitisha, ni kweli yalishafanyika mengi mabaya ila lile la jana ndio limepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la haki nchini.

Sitaki kuamini mateso yote waliyopata watuhumiwa, maumivu, na makovu waliyosababishiwa na watesi wao, ukiukwaji wa sheria wa makusudi.

Pamoja na yote bado jaji Siyani akaona vyote ni ujinga na kuipotezea mahakama muda wake kama asante yake kwa cheo alichopewa katikati ya kesi.

Hili linaonesha sasa kama taifa tunahitaji kuamka kwa pamoja, tusitegeane na kunyoosha vidole kwa taasisi moja kama vile hiyo taasisi pekee ndio ina majibu ya kudumu ya shida zetu, na kama tukizidi kuchelewa, tujiandae kwa maumivu makubwa yatakayokuja siku za mbeleni miongoni mwetu.
Ni aibu kubwa sn kwa mahakama
 
Ww ndiyo unaonekana mjinga, kwenye suala ya haki ktk nchi wote tunatakiwa kuwa kitu kimoja, bila haki au nchi kuwa na maamuzi ya mtu mmoja tutafika? Tuache ujinga katiba mpya ni lazima
Ulichoandika ni ujinga mtupu. Sema ndo hivyo unalinda kibarua chako kisiingie mchanga.
 
Back
Top Bottom