Wadau nadhani kwakuwa wote tumeshapata picha kuhusu hizi idara mbili. Sasa hebu tuangalie wamefaulu vipi ktk kazi zao. Nitoe mfano tu wa Marekani ambapo CIA na intelligence organisations zingine zimefanikiwa kuifikisha Marekani hapo ilipo na kuwa Taifa lenye nguvu na sauti zaidi hapa duniani.wamefanikiwa hata kuiangusha dola kubwa iliyokuwa Hasimu wake mkuu yaani USSR. Hata hivyo kuna sehemu idara hizo za kijasusi za USA zilifanya makosa hata kugharimu maisha ya watu. Mfano tukio la Sep 11.
Sasa kwa hapa kwetu, mtizamo wangu ni kwamba Hizi idara zetu zimefanya mengi makubwa sana hasa hali ya usalama na Amani iliyopo kwa miaka mingi sasa, umoja wa kitaifa na Jeshi lenye Nidhamu kubwa sana ambapo hata baadhi ya nchi zilishasikika zikitamani kuwa na Jeshi lenye nidhamu kama Tz. Kwasababu inaaminika kuwa ni mara chache sana kukuta nchi masikini ikawa na jeshi lenye nidhamu. Mifano ipo mingi sana. Sasa yote hii ni kazi ya idara zetu hizi.
Success ingine ya idara zetu hizi ni ushindi ktk vita ya kagera. Kuna msemo kuwa ukiwa na MI imara basi ni rahisi kushinda vita hata kama adui ana silaha kuliko zako. Hata hivyo pamoja na success ya zaidi ya 90% lakini pia kuna sehemu kulifanyika mistakes. Mfano:-
1. Kushindwa kuzuia mashambulizi kwenye ubalozi wa Marekani. Jukumu la Tiss
2. Mabomu ya gongo la mboto na mbagala. Jukumu la MI. Walipaswa ku fore see.
3. Kutoroka kwa kanali Seromba. Kinachodaiwa kuwa sio raia wa Tz na ni Mrwanda. Kama ni kweli basi Vetting ya kujiunga na Jeshi is questionable kwani hadi kufikia cheo hicho ni kwanini hakubainika. Yamkini kuna wengine wengi wamebaki bado. Na kama ni kweli alikuwa ni raia wa nchi jirani basi ujasusi wao ni wa hali ya juu kuzidi wa kwetu kwani wameweza kumuingiza mtu akiwa na umri mdogo hadi anapata vyeo vi kubwa karibia na retirement age.
INGAWA MENGI YALIYOFANYWA NA IDARA ZETU NI MAZURI NA YALIYOTUKUKA LAKINI WANATAKIWA KUWA MACHO ZAIDI