Mkuu
H.S
Nilitegemea post yangu itakuwa "as short as a mini-skirt but to cover the essential parts" lakini imeshindikina. Mtaniwia radhi. Nimesoma hoja yako na imejikita zaidi kwenye madhara ya sheria hii mpya ya madini kwa wawekezaji wa kigeni. Nitaongelea kwa ujumla kama hii sheria mpya italeta mabadiliko yaliyokusudiwa kwenye sekta ya madini whether, kwa wawekezaji wa kigeni, wachimbaji wadogo wa madini, wazawa na kwa Watanzania kwa ujumla.
Hivi karibuni, nchi nyingi za Kiafrika, zikiwemo Zambia, Mali na Tanzania, zimefanya mapitio ya sheria za madini zilizotungwa miaka ya 1990s. Kwa upande wa Tanzania, serikali ilianza mchakato wa kuzifanyia mabadiliko sheria za madini tokea mwaka 2000. Kwa hiyo, imechukua takribani miaka 10 mpaka ilipopitishwa Sheria ya Madini ya mwaka 2010.
Sababu kuu ya mchakato wa kuzifanyia marekebisho sheria hizo ilikuwa ni kuongeza mapato ya moja kwa moja kutoka kwenye sekta ya madini. Sababu nyingine ilikuwa ni kuongeza ajira kwenye sekta ya wachimbaji wadogo wadogo (the artisanal and small-scale gold mining (ASGM) sector) kwa sababu makampuni makubwa ya madini yamekuwa yakitoa nafasi chache za ajira hasa kwa wazawa wanaozunguka maeneo yenye madini. Pia kulikuwa na suala la uharibifu wa mazingira na wazawa kuondolewa kwa nguvu kwenye maeneo ya madini na wakati mwingine kupewa fidia ndogo au kutopewa kabisa pamoja na kuwa wazawa hao walikuwa wanamiliki maeneo husika kimila.
Lakini kabla ya kuongelea Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ni itakuwa siyo vibaya kughusia walao kwa kifupi sheria zilizopita na matatizo yake, hasa kuhusiana na sekta ya ASGM. Sheria ya Madini ya mwaka 1979 ilitoa fursa kwa sekta ya ASGM kupewa permits za kuchimba madini sehemu ambazo hazikuhitaji gharama kubwa na zana za hali ya juu.
Katika miaka ya 1980s, serikali ilianza kuwaunga zaidi mkono ASGMs baada ya kupungunza mamlaka ya STAMICO (State Mining Corporation) katika kuhodhi shughuli za uchimbaji wa madini na mauzo ya dhahabu. Sera ya ASGM ya mwaka 1983 iliwahimiza wananchi kujiongezea kipato chao kwa kujihusisha zaidi kwenye shughuli za madini.
Katika miaka ya 1990s, serikali, kupitia mradi wa Benki ya Dunia (Mineral Sector Technical Assistance Project) ilianza mchakato wa kisera na kisheria ili kuwavutia wawekezaji wa nje hasa kwenye sekta ya madini. Madhumuni mengine yalikuwa ni kuitambua rasmi na ku-integrate sekta ya ASGM kwenye Mpango wa Taifa wa Madini.
Ili kufikia malengo hayo, serikali ilifanya mapitio ya sera na sheria za madini na kuja na sera mpya ya madini ya mwaka 1997, Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997 na Sheria ya Madini ya mwaka 1998.
Wakati inapitisha Sheria ya Madini ya mwaka 1998, serikali iliweka kipaumbele zaidi kwa wachimbaji wakubwa wa madini kama moja ya mikakati yake ya kiuchumi. Hii ilisababisha makampuni makubwa ya kigeni kumiminika Tanzania na kupewa ardhi kubwa kwa ajili ya kufanya shughuli za madini.
Serikali ilifanya hivi kwa kutarajia kuwa uwekezaji wa makampuni ya nje kwenye sekta ya madini ungeifanya Tanzania isitegemee tena misaada kutoka nje. Kwa mfano, kwenye Sera ya Madini ya mwaka 1997, serikali ilitegemea kuwa mpaka kufikia mwaka 2025, madini yangekuwa yamechangia asilimia 10 ya GDP. Lakini mpaka kufikia mwaka 2010, madini yalikuwa yamechangia asilimia 2.3 tuu ya GDP.
Hii ni tofauti na nchi nyingine kama Papua New Guinea and Botswana, ambazo mapato yatokanayo na madini yamewezesha nchi hizi kulipa madeni yao yote ya nje na pia kuwezesha Botswna kuwa a middle-income country. Kwa upande wa Tanzania imekuwa ni kinyume. Pamoja na madini yote, bado tunategemea misaada kutoka nje na deni la taifa linazidi kuongezeka.
Kati mwaka 1998-2008, asilimia 90 ya total value of the exports ilienda kwa makampuni ya madini ya nje. Mwaka 2002, mapato ya serikali kutoka seven major mines yalikuwa Dola za Kimarekani milioni 36.2 tuu!
Annual reports za kampuni ya AngloGold inayochimba dhahabu Geita zinasema kuwa mwaka 2006, kampuni hiyo ilichimba ounces 308,000 za dhahabu. Kati ya mwaka 2006 hadi katikati ya mwaka 2007 kampuni hiyo ilitengeneza gross profit ya dola za kimarekani milioni 93 kutoka machimbo ya Geita peke yake. Lakini kampuni hiyo ililipa Dola za Kimarekani milioni moja tuu kama corporate income tax na kudai kuwa italipa tena corporate tax mwaka 2011, ambapo ni miaka 11 baada ya kuanza operations.
Pia Barrick Gold iliripoti a net income ya Dola za Kimarekani milioni 97 kati ya mwaka 2004 na katikati ya mwaka 2007, lakini ilikuwa bado haijaanza kulipa corporate income tax. Kwa kipindi hicho, mrahaba ndiyo ulikuwa kipato kikuu cha serikali.
Kati ya mwaka 2002 na 2006, makampuni ya madini yalipeleka nje dhahabu yenye dhamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.9. Katika kipindi hicho, serikali ilikusanya dola za Kimarekani milioni 17.4 tuu kwa mwaka kama mrahaba, charged at 3% of the net back value of gold exports:
TWN Africa, et al, (2009) Breaking the Curse: How Transparent, Taxation and Fair Taxes can turn Africa's Mineral Wealth into Development.
Sababu inadaiwa ni matokeo ya Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 ambayo iliweka mrahaba wa asilimia 3 tuu na kutoa likizo za kodi (tax holidays) kwa makampuni ya madini. Inadaiwa pia kwamba "Mining companies… are granted too many tax subsidies and concessions" and "there is high incidence of tax avoidance by mining companies conditioned by such measures as secret mining contracts, corporate mergers and acquisitions, and various ‘creative' accounting mechanisms." -
TWN Africa, et al, (2009) Breaking the Curse: How Transparent, Taxation and Fair Taxes can turn Africa's Mineral Wealth into Development.
Haya yote ndiyo yalifanya watu wengi waanze kulalamika kuwa makampuni ya madini ya nje yalikuwa hayana manufaa yoyote kwa taifa. Pia watu walianza kulalamika wakitaka ASGMs nao wapewe ardhi kuchimba madini na pia kurahisisha ASGMs kupata leseni kwa usawa na haki kama ilivyokuwa kwa wachimbaji wakubwa.
Kutokana na malalamiko mengi kwenye sekta ya madini hasa kuhusiana na mapato madogo, migogoro kwenye sekta husika, nk. Rais Kikwete aliunda Tume ya Bomani. Ripoti ya Bomani ilisizitiza umuhimu wa kuzifanyia marekebisho sheria na sera za madini ili kuwapa Watanzania nafasi ya kunufaika zaidi na kujihusisha kikamilifu kwenye sekta ya madini.
Nakukumbuka kulikuwa na mjadala mkali sana bungeni wakati serikali ilipoleta hii sheria kama mswada. Wanasema "the Mining Act 2010 was probably one of most hotly debated Bill in the previous Parliament. Some 84 MPs contributed to the Bill, which was debated for two days. While 23 MPs had an opportunity to contribute on the floor, 61 sent their views in writing. It thus became the most debated Bill during the 19th parliamentary meeting.."-
http://allafrica.com/stories/201004240013.html
Serikali ilidai kuwa sheria hii mpya ingeongeza mapato yatokanayo na kodi, ASGMs na fidia kwa wale watakaondolewa sehemu za madini. Wabunge walidai kuwa sheria haikwenda far enough. Hata hivyo, mjadala uliishia kujikita zaidi kwenye kuanzisha Mamlaka ya Madini (Tanzania Mining Authority – TMA).
Swali ambalo nimekuwa nikijiuliza ni kama sheria hii mpya italeta mabadiliko yoyote kwenye sekta ya madini. Kwanza kabisa inabidi tujue kuwa matatizo yanayotokana na makampuni makubwa ya madini hayasababishwi na vifungu vya sheria pekee. Kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko ya rushwa kwenye sekta ya madini. Malalamiko hayo yanahusisha maafisa wa ngazi za juu kitaifa na pia huko yanakochimbwa madini.
Mikataba ya madini bado ni siri. Wananchi hawajui kinachokubaliwa na kusainiwa. Hakuna transparency. Mpaka kulikuwa na tuhuma kuwa mkataba mmoja wa madini ulisainiwa kwenye chumba cha hotel London ambapo ni mbali kabisa na macho ya Watanzania. Environmental Impact Assessments (EIAs) inafanyika kabla ya large-scale projects kuanza, lakini baada ya hapo hakuna monitoring and evaluation na sehemu ya tatizo ni siasa na rushwa.
Watu hasa wale wanaosihi karibu na sehemu zenye madini wanaadhirika sana na rushwa na uongozi mbaya. Kuna matatizo kwenye mining and acquisition of lands na pia malipo ya fidia. Mifano ipo Kahama, Geita, Simanjiro, na kwingineko.
Hata kama kiini cha tatizo la ASGM kinatokana na sheria ya nyuma, bado sheria hii mpya haitambui diversity ya ASGM na complexities za ajira kwenye hiyo sekta. Serikali inasizitiza umuhimu wa kuwapa leseni watu lakini the reality is that landlords and licence holders often lease out land to unlicensed groups. Primary Mining Licence system inawa-favour zaidi wealthier entrepreneurs kuliko mwananchi wa kawaida. Kama ilivyo sheria ya zamani, sheria hii mpya haitoi maana ya "artisanal" mining. Pia tofauti na Primary Mining Licence system ambayo ni more restrictive, sheria haitoi options nyingine za leseni kwa ajili ya ASGM workers.
Pamoja na hayo, inategemewa kuwa sheria hii mpya ya madini italeta uwekezaji mpya kwenye sekta ya madini, itaiongezea serikali mapato, itatoa mazingira mazuri kwa wachimbaji wadogo wa ndani, na itaongeza fidia kwa wale wanaohamishwa. Lakini kama nivyosema awali kiini cha tatizo siyo sheria yenyewe.
Kama alivyosema Terry Karl, "it is a great challenge to undo the political and institutional distortions that have emerged in mining countries, and changing legislations may not be enough. It is a task for the coordinated efforts of all stakeholders." -
Terry Karl, "Ensuring Fairness: The Case for a Transparent Fiscal Contract" in Humphreys, M. et al (eds), Escaping the Resource Curse (Columbia University Press, 2007) 256–85.
Kwa hiyo, kama alivyosema Siri Lange kwenye article yake titled
"Gold and Governance: Legal Injustices and Lost Opportunities in Tanzania" (2011) African Affairs, Vol. 110/439, 233–252, "With governance problems unresolved – particularly corruption, which has proved a central problem up to now – it remains to be seen whether the 2010 mining act will make a difference, or whether we will still find that people have legal rights but no justice in the rapidly expanding mining areas of Tanzania."
Mwisho kabisa kwa wale wanaoikosoa sheria hii kuwa haiwalindi wawekezaji wa nje na pia kwa wale wanaounga mkono sheria hii kuwa inawalinda wachimbaji wadogo wa madini, inabidi kwanza wajiulize kama sheria hii inawalinda wao binafsi na familia zao kwa kusoma kifungu cha 18(1) cha sheria hiyo.
Kifungu cha 18(1) kinasema kuwa "…no person other than a mineral right holder, a licensed dealer, or licensed broker shall have in his possession, or dispose of, any mineral or minerals, unless as an employee, agent or contractor, he has acquired and holds the mineral or minerals for or on behalf of a mineral right holder, licensed dealer or a licensed broker."
Kwa hiyo basi kama unajichimba choo chako cha shimo au unapalilia maharage kwenye ardhi unayoimiliki kisheria halafu bahati nzuri ukakuta kipande cha Tanzanite hutaweza hata kukimiliki kisheria kama huna leseni. Kifungu hiki kinakunyang'anya haki, fursa na hata bahati yako kama mzawa kumiliki madini (ispokuwa chumvi na chokaa) bila leseni. Tafakari.