Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sharia ndo ile mambo ya kukatana mikono?Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.
Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia.
Sharia haijaacha kitu katika mfumo wa maisha ya mwanaadam ya kila siku, kama hatujaifuata sharia ya Mwenyezi Mungu basi tusitegemee mafanikio maisha.
Watanzania tusiopenda ufisadi, wizi na ubadhirifu tuungane na tuitake katiba yetu iwe kwa mfumo wa sharia.
Tujadiliane.
Ndo iyo iyo sasa faiza hana exposure ila anataka iwepo uku ye aende tu afghanstan one year kwa wale mandevu afu alete mrejesho co kujificha mexico ya k kooSharia ndo ile mambo ya kukatana mikono?
Simple.Nyie watu waovu mno. Hamna wakati serikali ya JMT imekuwa na itikadi ya kutoamini uwepo wa Mungu. Marais wetu wote hawakuficha imani zao na walikuwa waendaji wazuri wa makanisani na misikitini. Siku zote katika JMT itikadi yetu imekuwa serikali haina dini lakini raia na wakaazi wote wa nchi hii wana dini yao. Kwa sababu hiyo, hamna raia wala mkazi atayehukumiwa au kupewa haki kwa msingi wa dini yake nje ya sheria zilizotungwa na Bunge lenye waumini wa karibu dini zote zilizopo. Ndio maana mtu atakayefumaniwa hatapigwa mawe mpaka afe bali anaweza kupelekwa katika vyombo vya sheria ambako kama atapatikana na hatia ya kuvuna sheria iliyopo atahukumiwa inavyopaswa.
Hicho mnacholamikia kuwa mnadhibitiwa ni kuhakikisha kuwa mnawatendea haki waumini na wasio waumini wa dini zenu kwa kusingizia kuwa imani zenu zimeruhusu. Ndio maana katika nchi yetu mkimuua mtu aliyehama dini yenu kuingia nyingine ( apostacy au riddah) kama inavyotakiwa katika imani yenu, sisi tutakukamata na ukipatikana na hatia utanyongwa.
Aidha, ukimuua binti yako au mwanamke yeyote kwa sababu unaamini ni muasherati, ukipatikana na hatia utanyongwa.
Uovu wenu unajionyesha katika namna mnavyolipa uzito suala la uasherati kuliko suala lingine lolote.
Kwa kifupi nchi hii sio yenu peke yenu. Hatutaki Sharia na hamna siku Sharia itachukua nafasi ya nchi yetu. Ukiona hauwezi kuishi katika nchi inayokukataza kumuua binti yako aliyepata uja uzito nje ya ndoa hamia nchi nyingi tu ambazo zinafuata Sharia. Huko utaishi kwa amani na utafaidi maendeleo makubwa waliyo nayo.
Amandla...
Kwa wezi ndio, lakini kabla ya kumkata mkono inatakiws mjiridhishe kuwa alipatiwa fursa ya kujichumia kipato chake kihalali. Mfano, anafanya kazi serikalini, anapokea mshahara halafu hapo hapo anaiba, huyo ni wa kukatwa mkono tu, au unaonaje?Sharia ndo ile mambo ya kukatana mikono?
Faiza acha udini!Wengi tunaongelea katiba mpya sasa hivi, lakini hatuongelei iweje.
Mimi nashauri tena nasisitiza, hakuna katiba yoyote bora iliyotungwa na itakayotungwa na binaadam. Muumba wetu anatuelewa ubora wetu na mapungufu yetu ndiyo maana akatuwekea Muongozo ulio bora kabisa. Sharia.
Sharia haijaacha kitu katika mfumo wa maisha ya mwanaadam ya kila siku, kama hatujaifuata sharia ya Mwenyezi Mungu basi tusitegemee mafanikio maisha.
Watanzania tusiopenda ufisadi, wizi na ubadhirifu tuungane na tuitake katiba yetu iwe kwa mfumo wa sharia.
Tujadiliane.
Mbona kuna wengi wanafuga ndevu Tanzania?Mana wew hujakaa vizuri na ozo njemba afghanstan ivo credibility ya performance ya sharia huna inabid ukakae afghanstan mwaka mmoja na zile mandevu then ndo uje na mrejesho wa performance ipoje ya sharia kutatua matatizo
Sheria izi izi tu ni kupata viongozi wa kuzisimamia vizur mfano fisadi akamatwe afungwe na mali zake kutaifishwa pia mahakama iwe na nguvu ya kushitak viongoziNini ufumbuzi wako kuhusu matatizo ya ufisadi Tanzania?
Report za CAG kila mwaka zinatoka, kiongozi gani amechukuwa hatua?Sheria izi izi tu ni kupata viongozi wa kuzisimamia vizur mfano fisadi akamatwe afungwe na mali zake kutaifishwa pia mahakama iwe na nguvu ya kushitak viongozi