Tanzania Motorbike Road Trip - Tanga | Safari ya Tanga

Safi sana. Umeelezea vizuri mno. Asante kwa ku share safari yako.

Vipi kuhusu upepo njiani, haukuwa kero??
 
Kwa hapo Dar es Salaam unaweza jua Honda xr 125cc yaweza kua bei gani? Iwapo Kuna duka linauza new bike
Sijui bei yake XR, ila xl 125 inakuwaga arround 6.9M kama saba tu.
Xr125 na Xl125 hazitatofautiana sana nahisi.
 
Essentials
 
Na mm nina mpango nikirudi home IRINGA niende mbeya nina boxer BM 150 mdomo wa bata....hiyoo itakuwa from IRINGA twn......munogage ukooo
 
Kwa kukazia zaidi, chukua Honda Ace 125cc au Yamaha ybr 125. Hizi zote ni imara, mafuta zinatumia kidogo pia huchoki kuendesha na zina afya zaidi. Kama ni mpenzi wa 5 speed ni vema ukachukua hii Yamaha ybr 125 gearbox yake ni 5 speed.
Sawa Mkuu najichanga hapa nitanunua hiyo Yamaha ybr
 
Hahaha mkuu uoga huo.. Bagamoyo hapo karibu tembea ata ufanye utalii wa ndani tu
 
Sio mm mkuu ...
Upo sahihi umbali mrefu huo kwa pikipiki ni risk sana...

Chalinze nilienda mwezi uliopita... ila bagamoyo nishaenda sana kama mara 5 ivi....
Hivi mkisema risk ni nini? Mimi kiukweli kusafiri kwangu na pikipiki sijaona risk yoyote sasa sijui nyie mnasema risk gani?

Nachojua Risk ni wewe na uendeshaji wako only that.. nyie mnasema risk gani hiyo?
 
Hivi mkisema risk ni nini? Mimi kiukweli kusafiri kwangu na pikipiki sijaona risk yoyote sasa sijui nyie mnasema risk gani?

Nachojua Risk ni wewe na uendeshaji wako only that.. nyie mnasema risk gani hiyo?
Mkuu risk zile njia zenye traffic kubwa wakati mwingine wenye magari hawaheshimu pikipiki. Unaweza kuwq upo upande wako kabisa lakin akakuletea hukohuko sasa kidogo unakuwa mwangalifu na ndio hapo inakuwa risk.

Mfano imewahi nitokea kwenye mapishano ya morogoro road pale jangwani ilipo yard ya mwendokasi. Mimi natoka fire naenda magomeni jamaa yupo na corolla anatoka magomeni akatishe kwenda jangwani kule ilipo jengo la Yanga. Sasa kikawaida ilipaswa asuburi nipite kabla yeye hajakunja kuja kuingia barabara yangu.

Licha ya kumpa warning kwa kuwasha taa na kupiga horn lakin nikastuka huyu hapa tayari kashaingia. Nikifunga brake kali lakin haikuzuiwa kuanguka japo sikuu hata kidogo naye hakuumia. Nilivunja indicator ya pembeni.

Mara nyingine ilikuwa barabara ya bandari mi natoka Kigamboni jamaa atoka bandari ndani aingie barabarani same mistake anaforce aingie kama nyoka tu.
 
Uh pole sana Mkuu na Mungu Mwema kwa kuwa ulipona Salama..

Siku zote napokaribia katika makutano huwa napunguza mwendo ata kama gari hakuna (kutokana na uwezo wangu wa kuona) hivyo ni muhimu sana kwenye makutano yoyote upunguze mwendo na kumbuka kumpa kipaumbele anayetoka Mkono wako wa kulia.

Hii ya kipaumbele wa kulia kwako ni better zaidi sababu itakufanya uwe salama barabarani na kisheria
 
Nilivyokuwa Tanga Nikaenda Mapango ya Amboni (Amboni Cave) pia nikaenda Makumbusho ya Tanga.

Naomba nieleweke sifanyi Biashara ila najaribu kuwaonyesha watu Pikipiki ni Usafiri Mzuri na Salama kuliko ata Gari (Endapo utakuwa Makini na Kuzingatia Sheria za Barabarani)

NB: Nimefanya kile nakipenda kwenye Moyo wangu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…