ahsante
Future president tujipange,tutafika.
Habari yako Mheshimiwa Raisi.
Kuna siku moja niliwaza kama ningebahatika kuwa Raisi wa TFF ningefanyaje tuwe na timu Bora kama za wenzetu?
1:Nilifikirria namna ya kuita wataalamu waweze kutufanyia Tathmini ya kuanzisha Academy kwenye Kanda zetu za nchi hii.(Kanda ya kati, Pwani, kaskazini,Kusini,nyanda za juu kusini magharibi n.k) NIlifikiri tuwe walau na Academy Kumi hivi.
2.Baada ya Tathmini na Gharama zote kujulikana,Zoezi la pili lingekua Kufanya fund raising ya kuhakikisha tunapata fedha za kuanzisha hizo Academy na kuziendesha.Ingefanyika kwa wadau, makampuni serikali na wapenda soka na hata fifa wenyewe.Tuwaonyeshe mpango kazi wetu kwani wangeweza kutuchangia..
3.Tungeagiza wataalam wa Scouting, kutafuta vipaji kuanzia Vijijini,wilayani,mikoani hadi Kanda husika.Kwani huko ndiko kuliko na vipaji.Baada ya kupata hivyo vipaji tuseme,tumepata vijana 1000,Tungeanzisha ligi za michujo huko wanakotoka kisha tukapata idadi ya wale tunaowaahitaji kwenye Academy zetu za Kanda.
4.Tungewasajili vijana wetu Rasmi kwenye Academy na kuanza mafunzo Rasmi.Baada ya Muda kama wa Mwaka mmoja, Tungeanzisha mashindano rasmi ya hizi academy kuweza kuchuja na kupata Top cream,ambayo tungeiweka kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa.
Nadhani hapa tungepata timu nzuri kabisa ya Taifa, sio kama hii ya Simba na Yanga.Nakumbuka Zambia baada kupoteza wachezai wake kwenye ile ajali walifanya Scouting nchi nzima na kupata kikosi kipya ambacho baada ya muda ndio kimekuja kuchukua Kombe la Africa.